Zitto Kabwe: Takwimu za Pato la Taifa kwa robo iliyoishia Juni 2017 si sahihi, ZIMEPIKWA! (PDF attached)


Francis12

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Messages
7,026
Likes
18,835
Points
280
Francis12

Francis12

JF-Expert Member
Joined Sep 30, 2016
7,026 18,835 280
Pato la Taifa la Tanzania lilisinyaa kati ya April na June 2017 tofauti na Taarifa ya Serikali. Fuatilia Press Conference Mbunge Zitto Kabwe kuanzia saa sita kamili mchana.
======

UPDATES..

Waandishi wa habari kutoka Vyombo mbalimbali vya utangazaji wameshafika Makao Makuu ya ACT Wazalendo. Sayansi - Kijitonyama. Tutakuwa live muda mfupi ujao baada ya wahusika kufika.
---------

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Zitto Kabwe tayari ameshafika..

View attachment 619056


Zitto ameanza kuongea..

Oktoba 20, 2017, Kamati ya Uongozi ya ACT Wazalendo ilifanya kikao Dar kujadili hali ya kisiasa na kiuchumi ya Taifa letu.

Kamati ya Uongozi ilitaarifiwa juu ya shaka ya kitakwimu za Ukuaji wa Pato la Taifa zilizotolewa BoT kati ya Aprili – Juni 2017.

Pato la Taifa la Tanzania lilisinyaa (contraction) kati ya Aprili na June 2017 tofauti na taarifa ya Serikali.

Tumetumia taarifa za takwimu za Serikali kuchambua hali halisi, hatuvunji Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2015.

"Shaka iliyokuwapo juu ya kupikwa kwa takwimu za ukuaji wa GDP ni halali, ni ya kweli na sasa tuna ushahidi".

Taarifa ya mwisho ya Mapato ya Serikali iliyotolewa na TRA ni ya kupikwa haina uhalisia. Nafahamu uchumi una lugha isiyo rafiki kwa walio wengi lakini nitajitahidi kutumia maneno rahisi ili wote tuelewane.

Pato la Taifa (GDP) ni jumla ya mapato ya watu wote waliopo katika nchi au taifa husika katika kipindi maalumu,hususani mwaka 1. GDP ni kipimo cha uhai wa Uchumi wa Taifa kwani ukuaji au uporomokaji wake hutumika kupima shughuli za kiuchumi za Taifa husika. Ukisikia GDP ni (+) maana yake kuna shughuli za uchumi zimeongezeka, Na (-) maana yake ni kuwa shughuli za uchumi zimepungua.

Kwa Tanzania, tuna utaratibu wa kutoa takwimu za GDP kila baada ya miezi mitatu ambapo huita robo. Mwaka mmoja una robo nne.

Tafiti zinaonyesha kuwa ili kuondoa umasikini wa Tanzania, uchumi wetu unatakiwa ukue zaidi ya 10% kwa miaka kama 5 mfululizo. Uchumi wa Tanzania haujawahi kukua kufikia 10% wakati wa utawala wote wa CCM. Kwa muda sasa, wastani wa ukuaji umekua ni 7%.

Thamani ya bidhaa zilizouzwa kwenye nchi nzima hupatikana Kwa kuzidisha wastani wa bei na mzunguko wa bidhaa (transactions). Nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitano (5) iliyopita, mzunguko wa fedha umekuwa ni kati ya asilimia 0.5 na 1.5.

Je, Pato la Taifa kwa mwaka 2015 na 2016 lilikuaje? Wananchi wanalalamika "Vyuma vimekaza. Ni wajibu wa mchumi kujiuliza inakuwaje tuna GDP inayokua wakati wananchi wanalia?

Takwimu za makusanyo ya kodi za serikali kutoka TRA zinaacha mashaka makubwa mno kwani ni takwimu za kutengenezwa.

Kusinyaa kwa ukuaji wa uchumi kutokana na sera mbaya za Serikali, kumesababisha makusanyo ya Mapato ya Serikali kushuka mno.

Baada ya maelezo haya, mtakubaliana nami kuwa takwimu za Pato la Taifa Kwa robo inayoishia Juni 2017 si takwimu sahihi. ZIMEPIKWA!
-----------

*Nyaraka za ushahidi zimeambatanishwa katika mfumo wa PDF
 

Attachments:

kibwenzi

kibwenzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Messages
2,500
Likes
1,324
Points
280
kibwenzi

kibwenzi

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2015
2,500 1,324 280
Tuko Pamoja
 
djzm70

djzm70

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2014
Messages
4,104
Likes
1,904
Points
280
djzm70

djzm70

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2014
4,104 1,904 280
Pato la Taifa la Tanzania lilisinyaa kati ya April na June 2017 tofauti na Taarifa ya Serikali. Fuatilia Press Conference Mbunge Zitto Kabwe kuanzia saa sita kamili mchana.

Livestream Act Wazalendo na Zitto Kabwe pages.

Pia mwananchi online, azamtv online, JamiiForums online na wengine wengi.
======UPDATES
Takwimu zake aangalie vizuri, atoe tu mtazamo wake na si kupotosha takwimu za serikali
 
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
14,085
Likes
13,804
Points
280
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
14,085 13,804 280
Zitto tangia wizara ya nishati na madini zipate wateule naona akili zimemrudia
Wanachama wengi wa ACT wazalendo wamehama chama hana watu wa kuwahutubia ndio maana anawaita waandishi wa habari awahutubie ili a steam out frustration zake za kukosa hadhira ya kuhutubia
 
K

KIBST

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2017
Messages
480
Likes
1,878
Points
180
K

KIBST

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2017
480 1,878 180
Siasa kitu cha ajabu sana..Zitto inawezekana anajazwa UJINGA na mtu aliye ndani ya SYSTEM AMBAYE ANAMWAMINI KABSA ili hali kumbe wanamchezea mchezo asioujua yeye....Zama zimebadilika mzee funga mdomo wako usijifanye unajua kila kitu..UJUAJI WAKO UONYESHE KWENYE KUIFANYA ACT tishio...UTAUMBUKA KAKA YANGU unajazwa data za uwongo na huyo anaekupa..WATAKUUMBUA WENZIO...Kuwa na akiba ya maneno na kuwa makini sana utamkalo...Maana kuna kesho pia UNGEPENDA ZAIDI watu waendelee kukuamini...sasa ukiharibu leo nani atakuamini kesho???
 
A

artch2311

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2016
Messages
600
Likes
271
Points
80
Age
42
A

artch2311

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2016
600 271 80
Zitto tangia wizara ya nishati na madini zipate wateule naona akili zimemrudia
hapana issue sio uteuzi
issue kubwa kwa zzk sasa hivi ni kupoteza wanachama muhimu,
1. Anna Mghwira
2. Kitila Mkumbo
3. Samson Mwigamba
4. Mwampamba na wafuasi wake..
wote hawa ndio potentials ndani ya ACT na wengine wameondoka juzi tu.
kimsingi ilibidi tutafakari
KULIKONI......??/
1. Kweli ACT ni CCM b
2. Au yeye ZZK ni dkteta kiasi watu wanamkimbia?

haya ndio mambo yanayomuumiza ZZK, sasa ili kufunika ndio kila siku anakiki headline watu waachane na suala la wanachama wake wanaoisha ACT..
 
kasulamkombe

kasulamkombe

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Messages
2,256
Likes
2,407
Points
280
kasulamkombe

kasulamkombe

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2017
2,256 2,407 280
Hivi kuna watu bado wanamsikiliza huyu Banyamulenge!! Leo tupo bize na mechi ya mnyama. Awekeze nguvu kwenye ACT yake!
 

Forum statistics

Threads 1,237,407
Members 475,533
Posts 29,287,333