BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,082
Zitto Kabwe: Sinunuliki
na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Kabwe amesema hanunuliki kwani hana bei, na kamwe hatofumba mdomo kukemea ufisadi unaofanywa na viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali za wananchi.
Zitto alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki mjini Tanga alipokuwa kwenye mkutano wa hadhara baada ya mkazi mmoja wa mjini humo kumuuliza kama kuteuliwa kwake katika kamati ya kuchunguza masuala ya madini kulikuwa na nia ya kununuliwa na kuukacha upinzani.
Akijibu swali hilo, alisema hawezi kununuliwa kwa sababu yeye ni mwanamageuzi, na anataka kuona watendaji wa serikali wakiwajibika kwa wananchi waliowateua, badala ya kuwanyenyekea matajiri na wawekezaji wachache ambao wanazifanya rasimali za taifa kuwa mali zao.
Alisema kuteuliwa kwake katika kamati hiyo na Rais Jakaya Kikwete, ilitokana na kelele zake na za wananchi kuhusu unyonyaji unaofanywa na wawekezaji katika sekta ya madini, ambayo imekuwa ikiwanufaisha zaidi wageni.
Jamani asiwadanganye mtu kuwa mimi ninaweza kununuliwa, kwani bei yangu haijulikani, na sitegemei kunyamaza kwa wote wanaoshiriki katika kutafuna rasilimali za nchi, alisema Zitto.
Alisema kama utaratibu wa kuwanunua wapinzania utashamiri, basi taifa litapoteza mwelekeo zaidi, kwani upinzani ndio unaoleta chachu kubwa katika maendeleo ya taifa lolote hapa duniani.
Zitto alisema katika kipindi ambacho upinzani, hasa NCCR- Mageuzi iliyumba, ndipo watendaji wa serikali walipojitwalia jukumu la kutafuna rasilimali za nchi kwa kuwa hakuna watu waliokuwa wakiwapiga kelele.
Alisema miaka 10 ya kulegalega kwa chama hicho ni pigo kubwa kwa wapinzani ambao hivi sasa wanaelekea kufanya vizuri zaidi katika kusimamia serikali, licha ya kuwapo kwa watu wanaorudisha nyuma juhudi za wapinzani hao.
Kuna juhudi kubwa za kuudhoofisha upinzani, hasa kwa watu wanaoshiriki vitendo vya ufisadi ili waweze kuendeleza ufisadi wao, na kama tusipokuwa makini tutaingia katika mkenge wa hao mafisadi, alisema Zitto.
Aidha, Zitto alisema ni vema Watanzania wakawa wanapiga kura kimkakati ili wasije kuibiwa kura zao na watu wanaotaka kujitwalia madaraka kwa njia za mlango wa nyuma, ambazo mara kwa mara zimekuwa zikifanywa na CCM.