Zitto Kabwe: Shilingi 2,000,000,000,000 zinatoroshwa kila mwaka kukwepa kodi.

Money Stunna

JF-Expert Member
Aug 9, 2011
13,070
2,000
Bunge limeelezwa zaidi ya Dola za Marekani 1.25 bilioni sawa na Sh2 trilioni hutoroshwa na kupelekwa nje ya nchi kila mwaka kwa lengo la kukwepa kodi.
Taarifa hiyo imetolewa wakati wingu zito likiwa limegubika uwasilishaji wa ripoti ya kikosi kazi cha Serikali kilichochunguza sakata la Sh315 bilioni zilizofichwa na Watanzania katika mabenki nchini Uswisi.
Takwimu hizo zilitolewa juzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe.
Zitto alisema taarifa mbalimbali zinaonyesha kuwa Tanzania inapoteza kila mwaka mapato hayo ambayo ni sawa na asilimia tano ya Pato la Taifa kupitia uhamishaji huo haramu.
“Uhamishaji huu haramu wa fedha kupelekwa nje ya nchi hufanywa kwa lengo la kukwepa kulipa kodi au wahusika kuepuka kukamatwa na fedha walizopata kwa kupokea rushwa,” alisema Zitto.
Kamati hiyo imependekeza Bunge kutunga sheria itakayodhibiti uhamishaji haramu au ufichaji wa fedha nje ya kwa lengo la kuogopa kukamatwa na rushwa, kufanya ufisadi na kukwepa kodi.
Zitto alisema hayo ni moja ya maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa 10 wa Jumuiya ya Kamati za Hesabu za Serikali za Mabunge (Sadcopac) ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc).
Alisema katika mkutano huo uliofanyika Septemba 2 hadi 7, mwaka huu Jijini Arusha, wajumbe waliazimia kuhamasisha mabunge ya nchi zao kutunga sheria kudhibiti uhamishaji huo wa fedha.

Wiki iliyopita, mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina (CCM), alikaririwa akisema bungeni ‘hapatatosha’ kama ripoti ya mabilioni ya Uswisi haitawasilishwa katika Bunge hili.
Mpina alisema yeye ni miongoni mwa wabunge waliohojiwa baada ya kutamka bungeni kuwa zaidi ya Sh11.9 trilioni zimetoroshwa kutoka Tanzania kati ya mwaka 1970 na mwaka 2008.
“Nilipolisema hilo jambo niliikabidhi Serikali kupitia Bunge taarifa za tafiti mbalimbali ili ifuatilie. Baadaye Zitto akaja na hoja ya bilioni 314… tunataka taarifa hatutanii,” alisema.
Ripoti hiyo ilikuwa iwasilishwe Bunge la Aprili lakini Serikali ikaomba muda zaidi na kuahidi kuiwasilisha katika Mkutano wa 14 wa Bunge unaoendelea Mjini Dodoma.

----Mwananchi
 
Jagarld

JF-Expert Member
Apr 7, 2011
2,023
2,000
Jamani si jana tu tumekubaliana tujifunze kusameheana! Hawa walioficha vijisent vyao tuwasamehe tu halafu life isonge,tujifunzeni kusamehe.
 
Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761

Hata hivyo, Mpina alionyesha shaka kama ripoti hiyo itawasilishwa akisema hata ratiba ya Bunge haionyeshi suala hilo wala katika kikao cha kupeana taarifa cha wabunge suala hilo halikugusiwa.

Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema alipoulizwa endapo kikosi kazi anachokiongoza kimekamilisha kazi yake alisema: “Bado kazi inaendelea na ni ngumu… tunaendelea na uchunguzi”.

Agosti 15 mwaka jana, kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, iliitaka Serikali kuwataja kwa majina viongozi na wafanyabiashara wakubwa walioficha Sh315.5 bilioni katika mabenki nchini Uswisi.

Wakati huo huo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Hesabu za Serikali Kuu na Mashirika ya Umma (PAC), imefichua udanganyifu na mianya mikubwa ya ukwepaji kodi katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema), aliliambia Bunge mwishoni mwa wiki kuwa pamoja na TRA kufikia malengo kwenye makusanyo ya kodi katika mwaka wa fedha wa 2011/12, bado kumekuwapo na udanganyifu na mianya ya ukwepaji wa kulipa kodi katika maeneo kadhaa.

Aliyataja maeneo hayo kuwa ni kusitishwa kwa matumizi ya mita za kupima ujazo wa mafuta yanayoingia nchini kupitia kituo cha kupakulia mafuta cha Kurasini, jijini Dar es Salaam.

Alisema kamati yake imeitaka Serikali kulieleza Bunge sababu za msingi za kusitisha matumizi ya mita hizo na TRA kuainisha athari katika ukusanyaji wa mapato itokanayo na kusitishwa kwa matumizi ya mita hizo.

Alisema mpaka sasa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) baada ya kusitishwa kwa matumizi ya mita hizo inatumia vijiti vya kupimia ambavyo vipimo huchukuliwa wakati mafuta yako kwenye meli na baada ya kuwekwa kwenye matangi ya wafanyabiashara walioyaingiza mafuta hayo.

Alisema Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika taarifa yake ya 2010/11 alihoji kuhusu sababu za kusitisha matumizi ya mita kupima ujazo wa mafuta katika bandari za Tanga na Dar es Salaam na hivyo kusababisha hasara kwa Serikali kwa kufanya manunuzi yasiyo na tija.

Alifafanua kuwa kamati yake iliwahoji maofisa masuuli wa TPA aliyeeleza kuwa mita hizo zilinunuliwa mwaka 2004 na TPA na kufungwa katika kituo cha kupakulia mafuta cha Kurasini (KOJ) mwaka 2004 na kuanza kutumia mwaka 2005 kwa lengo la kupima kiwango cha mafuta yanayoingizwa nchini kupitia Bandari za Tanga na Dar es Salaam.

Hata hivyo, alisema ilipofika Februari 2011, Wakala wa Vipimo nchini (WMA), iliyoridhia awali matumizi ya mita hizo, iliwaandikia TPA kusitisha matumizi ya mita hizo kwa sababu zimethibitika kutoa vipimo visivyo sahihi hivyo kusababisha walipa kodi kulalamika.

Zitto alisema wakati TPA ikisema mita hizo hazina matatizo yo yote na zinaweza kuendelea kutumika, WMA wanasisitiza kuwa mita hizo hazitoi vipimo sahihi vya ujazo wa mafuta na kusababisha malalamiko mengi kutoka kwa TRA na wafanyabiashara ambao wamekuwa wakilipa kodi kubwa kutokana na vipimo visivyo sahihi vya ujazo wa mafuta vinavyosomwa na mita hizo.

Hata hivyo, alisema TRA walishindwa kuieleza Kamati jinsi ambavyo usitishaji wa matumizi ya mita hizo umeathiri upatikanaji wa mapato yatokanayo na kodi ya kuingiza mafuta nchini.

Maeneo mengine yenye udanganyifu ni mkataba wenye utata wa leseni za udereva, ambapo mkataba wa utengenezaji wa leseni za udereva uliingiwa kati ya TRA na kampuni ya M/s Track Innovations Ltd (OIT) ya Israel.

Alisema kamati ilibaini kasoro kadhaa katika baadhi ya vipengele vya masharti ya mkataba ambazo zinaiweka Serikali katika hatari ya kupoteza mapato makubwa.

Alisema mkataba huo ulihusu kubuni na kutengeneza mfumo wa kielektroniki wa utengenezaji wa leseni za udereva na makubaliano yalikuwa ni kutengeneza leseni za udereva 800,000 na tayari hadi kamati inakagua Machi, mwaka huu, leseni 681,850 zilikuwa zimetengenezwa na mkataba ulitegemewa kukamilika mwezi uliopita.

Alisema eneo lingine la upotevu wa kodi ni katika sekta ya mawasiliano kama TRA kukokotoa Kodi ya Ongezeko la Thamani na ushuru wa bidhaa kwa kutumia taarifa zinazotolewa na kampuni za simu pekee bila kuoanisha na taarifa za Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano (TCRA).

Alisema kwa mfano, katika mwaka wa fedha 2011/12, Kampuni ya Airtel ilikuwa na trafiki ya dakika 4,847,642,069 zinazoweza kutozwa Vat na ushuru wa bidhaa, lakini kampuni ilionyesha dakika 4,233,637,174 tu ambayo ni tofauti na dakika 614,004,885.

Alisema TRA imekiri kutoshirikiana katika kutafuta taarifa zilizosahihi kwa ajili ya ukokotoaji wa kodi lakini TCRA waliiarifu Kamati kuwa wamenunua mtambo utakaotumiwa na TCRA na TRA katika kutambua aina, kiasi halisi na thamani ya miamala inayofanywa na kampuni za simu.

Kwa hisani ya Mwananchi na Nipashe.
 
lyinga

JF-Expert Member
Nov 18, 2013
2,498
0
Tushachoka na hizi ngonjera kila siku song mpya kutaja hawataji kibaya zaidi wanaongea km wamemeza betri hatujaona mtu hata mmoja kakamatwa au yupo segerea tumebaki kuliwazana tu kama yatima akili ishachoka kusikiliza riwaya za wabunge
 
notradamme

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
2,012
1,195
the real man at work.
wakati wenzake wanapiga siasa yeye anapiga kazi. wakati wenzake wakiendeleza majungu, yeye anapigania taifa na mustakabali wake.
wakati wengine wakikimbia vitabu na tafiti na kukimbilia kutumia fedha za michango ya wanachama, yeye anasoma na kuchanganua mambo makubwa ya kidunia.
wakti wenzake wakizidi kununua vijana (kama akina ben saa8) yeye anatengeneza wafuasi kutokana na matendo yake yaliyotukuka.
huyu sio KANJANJA, TOO LOCAL wala mhafidhina. huyu ndio haswaaa anaonyesha tofauti kati ya uongozi maslahi na uongozi wito
 
Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,761
2,000
Mojawapo ya Kamati za Bunge zinazofanya kazi yake kwa kiwango kikubwa nchini ni hii ya Public Accounts Committee (PAC).

Pamoja na kwamba hawana meno ya kutosha kisheria kwa sasa, lakini wanatumia sauti yao kama activist social mobilization kwenye vyombo vya habari na pia kwenye majukwaa bungeni kuihabarisha jamii ili itambue nini kinachoendelea na katika kutambua huko, wananchi watapata msukumo na kuwa active and accountable citizen ili hatimaye to exert pressure to the government and ruling party to act accordingly. Somehow, it's working ukilinganisha na rigid bureaucratic control iliyopo serikalini kupitia ruling party.

It's stupid kwa Serikali kuwa mstali wa mbele katika ku-attract the largest portion of the world's investment wakati huo huo ikawa ni goigoi katika ukusanyaji wa mapato yatokanayo na hizo investment.

The government must design fully structured and sustainable tax collection methods ili wananchi wanufaike na 'God given' natural resources zao.

It's not the full shilling kusikia Waziri Muhongo anawafahamu watu au makampuni ambayo hayajalipa kodi lakini wizara inayohusika na ukusanyaji wa kodi iko kimya kisheria. This is intolerable katika jamii inayojitambua.

Mwaka 1995, Mwl. Nyerere aliwahi kusema kuwa Kutokusanya kodi ni sifa moja ya viserikali corrupt popote pale.

Siyo ajabu survey ya Transparency International imeiweka Tanzania kuwa nchi ya 111 kati ya nchi 177 kwa rushwa katika public sector kwenye corruption perception index ya 2013.
 
NullPointer

JF-Expert Member
Feb 7, 2011
3,467
2,000
Huyu Zitto bna hadi leo anabaki kusema ntawataja ntawataja, si ataje sasa?
Ndiyo yale ya Mbowe, ohh nina evidence kamili kule Arusha hadi leo kimya ina maana kaamua kuachia liende...
Hawa jamaa uaminifu nshapoteza kabisa, mimi ukisema unamajina na ukayataja na ikawa ni kweli, wewe kura yangu nakupa fasta bila kufikiria mara mbili, ila kuzungushana miezi yote kwa nini ulianzisha mada in the first place? usingeleta hilo wazo hadi umepata evidence kamili, tatizo bongo vichwa mbovu wengi wale wafata mkumbo, akisikia flani kasema kitu flani ashameza kama kilivyo, hana muda na evidence wala habari nyingine, ndio maana wamejipatia umaarufu hadi hapa na si vingine... Wa marekani wanasema flani halipi ushuru wanatoa data kamili, wabongo hadi hili wameshindwa kufatilia... Kwa kibali cha serikali unashindwa kupewa data za wenye hela, means hata serikali haina nguvu ktk hili, ngoja wengine tuanze kwenda kuzificha huko kumbe ndio kwa kukwepa kodi
 
Ngisibara

JF-Expert Member
Jan 2, 2009
2,906
2,000
the real man at work.
wakati wenzake wanapiga siasa yeye anapiga kazi. wakati wenzake wakiendeleza majungu, yeye anapigania taifa na mustakabali wake.
wakati wengine wakikimbia vitabu na tafiti na kukimbilia kutumia fedha za michango ya wanachama, yeye anasoma na kuchanganua mambo makubwa ya kidunia.
wakti wenzake wakizidi kununua vijana (kama akina ben saa8) yeye anatengeneza wafuasi kutokana na matendo yake yaliyotukuka.
huyu sio KANJANJA, TOO LOCAL wala mhafidhina. huyu ndio haswaaa anaonyesha tofauti kati ya uongozi maslahi na uongozi wito

Hizi ni single mpya mpya za CCM kupitia mbunge wao wa CCM ndani ya upinzani lakini tunashukuru mungu katujalia mapema kujinasua toka kwenye mtego huo hivyo basi siku hizi wala hutasikia wabunge wa CDM wakikomenti chochote kuhusu single za huyu bwana msaliti labda hao wabunge wenzie wa CCM,

Mangapi Zitto alishayasema lakini hayana msaada wowote ndani ya chama chake wala kwa hao mashoga zake??? nafikiri Zitto anaamini watanzania bado ni wadanganyika...

Nyamgluu

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
3,141
2,000
halafu jamaa ndio wakwanza kupeleka bakuli ya kuomba nje!
Inashangaza sana!
 
MASELE

JF-Expert Member
Aug 30, 2011
792
500
Majina si anayo awataje tu ili nasi tuamini kuwa anafanya kazi kweli
 
Uchaguzi

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
915
170
Hongera sana Kamati ya Zitto kwa kazi nzuri, natumaini wanaokuchukia watakupenda wenyewe!
 
CHAMVIGA

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
7,689
2,000
Dah hii hatari sana. Hiyo pesa ni ndefu na taifa linaingia hasara kubwa sana. Swali langu ni kuwa kwanini serikali imekuwa goigoi katika kushughulikia jambo hili la utoroshaji wa pesa kinyemela nje ya nchi?
 
Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,110
2,000
Huyu Zitto ni Msanii Mkubwa sana, anapotosha UMA kwa manufaa yake, Maswala ya kutorosha fedha ili kuepuka kodi sio uvunjifu wa sheria, nyingi zinafanyika kwa mfumo unaitwa transfer pricing. na hizi fedha haziendi kufichwa wala sio swala linalofanywa kwa siri.

Tunachokitegemea kutoka kwake ni kututajia watu walioficha fedha zilizopatikana kwa njia za rushwa na ufisadi wa rasilimalin zetu.
.
Asitake kufanya watu wajinga, shit.

Na alisema atawataja katika mkutano huu Bunge. I am seating here waiting him to name them or else He will have bear with my big mouth.
 
KirilOriginal

JF-Expert Member
Feb 13, 2012
2,148
2,000
So what! Unalia lia ama unakuja na suluhisho? Biashara ya kutuimbisha ubeti ule ule ili tukuone bab kubwa ungekuwa wamaana ungekipatia chama chako hii ishu ikifanyie kazi ya kuibana serikali angalau hata idadi ya wabunge wa upinzani wangeongezeka, haya pambana tuone utafika wapi.
By the way endelea manake ndo style maccm waliyoiona watapenyezea fedha kukulipa kiaina ili kuimarisha vurugu kwa upinzani.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom