Zitto Kabwe: Rais umeamua kuchagua upande wa wanaokupa taarifa za uongo na majungu, muda utasema

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Anaandika Zitto Kabwe

Rais umeamua kuchagua upande wa wanaokupa Taarifa za uwongo na majungu. Muda utasema. Wengine tumesema, tumeonya kwa mapenzi mema ya nchi. Wewe ndio mwenye vyanzo vingi na mkono mrefu. Umetamka hakuna njaa. Umefunga mjadala. Lakini uwe tayari kubeba mzigo wa maamuzi yako yanayotokana na habari za majungu, uwongo na kutaka kukufurahisha.

Magufuli-na-Zitto.jpg

=========

SOMA: Rais Magufuli: Magazeti yanayoandika kuna njaa,yamenunuliwa na wanasiasa na wafanyabiashara
 
Rais anasema hatapeleka chakula Simiyu na Bariadi eti kisa ukame.Wananchi walitakiwa kujua kama mvua ni ndogo basi walime mazao yanayostahimili ukame na si kulazimisha kulima mahindi yanayohitaji mvua nyingi.JPM anasema msema ukweli ni mpenzi wa Mungu,na yeye anasema ukweli kuwa hataleta chakula popote kwa sababu ni wanasiasa na wafanyabiashara ndio wananunua magazeti kutangaza njaa.
 
Naona anajihami kabisa kwa kauli hii

Mwishoni Rais amemalizia kwa kusema
"Naweza kuwa sio mwanasiasa mzuri sana,Lakini ipo siku mtakuja kunikumbuka"

Mheshimiwa raisi mpendwa wetu kauli zako zinaudhi sana, uungwana ni kauli nzuri na ndio hekma ya uongozi..
 
"...anayejua kuna njaa nchi hii ni Rais, mimi ndio naejua wapi kuna njaa na wapi hakuna.Tanzania hii haina njaa wala watu hawana njaa". JPM, Simiyu - 11/01/2017.

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG]: Hii ni Nchi ya Kufikirika! Mimi nimekuwa mkoani Mara kwa wiki mbili, watu wanashindia maembe na msimu wa maembe umekwisha sijui kama watashindia mapapai, hakuna chakula. Unapokuwa Rais wa nchi lazima uwe na busara na hekima za juu sana.
[HASHTAG]#JSM[/HASHTAG].
 
"...anayejua kuna njaa nchi hii ni Rais, mimi ndio naejua wapi kuna njaa na wapi hakuna.Tanzania hii haina njaa wala watu hawana njaa". JPM, Simiyu - 11/01/2017.

[HASHTAG]#Note[/HASHTAG]: Hii ni Nchi ya Kufikirika! Mimi nimekuwa mkoani Mara kwa wiki mbili, watu wanashindia maembe na msimu wa maembe umekwisha sijui kama watashindia mapapai, hakuna chakula. Unapokuwa Rais wa nchi lazima uwe na busara na hekima za juu sana.
[HASHTAG]#JSM[/HASHTAG].
Yeye anakula bure chakula bure mpaka kuvaa bure ni kodi zetu ataona shida ya njaa wapi?
 
Naona anajihami kabisa kwa kauli hii

Mwishoni Rais amemalizia kwa kusema
"Naweza kuwa sio mwanasiasa mzuri sana,Lakini ipo siku mtakuja kunikumbuka"

Mheshimiwa raisi mpendwa wetu kauli zako zinaudhi sana uungwana ni kauli nzuri na ndio hekma ya uongozi lazima ijue tofouti ya kiongea na housegirl wako na wapiga kura wako.
Huyu ameshalewa madaraka
 
rais magufuli ifikie kipindi akubaliane na ukweli anaoambiwa ukali hauna nafasi katika shida hizi tulizonazo...nahisi ipo siku atatokewa na mzimu wa hayati baba wa taifa amuelekeze jinsi ya kuiendesha Tanzania

sikatai magufuli ni kiongozi mzuri lakini kuwa kiongozi bila team work ni shida,team work ni sisi na yeye atusikilize basi
 
Na kwa taarifa yenu... Nimeamuru mvua zisinyeshe ili tujue wakulima wa kweli ni wangapi na wapiga dili kwenye hiyo sekta ni wangapi?
Watu mashamba mnayo... Majembe mnayo... Watoto mnafyatua wengi wa kuweza kulima hekari nyingi tu kwa muda mfupi... Lakini bado mmekaa kuimba mapambio njaa njaa njaa...!
Sasa sitatoa chakula cha msaada ng'o.. Mkalalamike kokote.!!!
Msemakweli mpenzi wa mungu!!
Nasema mvua hazitanyesha hadi tujue wakulima hewa ni wangapi...!
Serikali haina shamba wala vyakula vya kugawa hovyo hovyo...!

Lol! Nawaza tu kwa kupaza sauti,
 
Sasa nimejua kuwa Kikwete ni mjaja amemuweka magu kuifanyia kampeni Ukawa ili Lowassa ashinde kwa kishindo 2020 endelea na hayo matamko tu UVCCM kazi wanayo.mzuieni huyo atawakoshesha ushindi ccm 2020



swissme
Wewe endelea kuota mchukue nchi kwa mikakati gan na ip
 
Ni baada ya kuona kuwa Kikwete angemuachia lowassa kijiti 2016 ccm wangeongea sana ila Kikwete akaona bora amuweke NWA
Mtapelewa pelekwa na upepo kama bendera hadi mchanike, (shenzi!)

tulishazoea kutukanwa hadi na mkuu.


"SERIKALI YANGU HAITATOA CHAKULA,NINAPOSEMA SILETI CHAKULA SILETI KWELI,WALA SIMUNG'UNYI MANENO NA SITALETA KWELI,MLIZOEA MANENO MATAMU SASA MIMI SINA MANENO MATAMU"alisisitiza Rais Magufuli.

swissme
 
Back
Top Bottom