Zitto Kabwe: Rais Magufuli alienda Rwanda kujifunza jinsi ya kubana Vyama vya Upinzani

mwobho

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
808
352
Wakuu habarini,

Tayari tupo makao makuu ya chama cha ACT WAZALENDO tunamsubili Kiongozi wa chama hicho Zitto Zuberi kabwe.
Waandishi wamejitokeza wengi kweli kweli.
Viongozi wa chama wanaendelea na maandalizi ya mkutano huo.
Ndani ya dakika chache zijazo mkutano na waandishi unaanza.

Live Updates zitawajia kupitia mimi mwenyewe.

Karibuni

UPDATES
Tayari viongozi wanaelekea eneo la mkutano, waandishi nao wanaweka sawa vinasa sauti vyao na vinasa picha

Nimedokezwa hapa zitto ataongelea masuala kadhaa

- Namna Magufuli anavyominya Demokrasia
- Kuzuiwa kwa Kongamano lao la jana pale Millenium Towers
- Msimamo wao kama chama kuhusu hali inayoendelea
- Way foward

Nitaendelea kuwajuza

UPDATES
.......................
Zitto Amewasili

Anasema hajui ni kwanini Polisi wamezuia Kongamano lao la Kuchambua Bajeti.

Zitto ''juzi usiku siku ya jumaamosi, watu wetu wa usalama wa chama walinijulisha kwamba Jeshi la Polisi wananitafuta, wakaenda nyumbani kwangu na magari manne kunikamata bila kufuata utaratibu''

Zitto ''Jumanne iliyopita Kamishna Wambura alinipigia kuniomba nifike polisi''

Zitto ''Hii ya Jumaamosi walikuwa wanataka Kunivizia''

Zitto ''Watu wetu wa Usalama wa Chama walihakikisha kwamba sitakamatwa ili niweze leo kupata fursa kuzungumza na watanzania kupitia nyie wana habari'

Zitto '' Hatufahamu Watawala wanaogopa nini mpaka kuzuia mikutano ya wanasiasa''

Zitto '' Nasikia Jana Walimkamata Mwenyekiti Mbowe wa Chadema Huko Mwanza kisa eti kawasalimia wananchi, huu ni uvunjwaji na ukiukwaji mkubwa wa utawala wa kidemokrasia''

Zitto ''Tunalaani tabia za KIDIKTETA za Rais Magufuli''

Zitto ''Magufuli ameanza na vyama vya siasa kuonyesha Udikteta wake, nawahakikishia akimalizana na Vyama vya siasa atahamia kwenu Wanahabari, Tumkatalie''

Zitto ''Ndio maana Magufuli Ziara yake ya Kwanza alifanya RWANDA, tumegundua kuwa alikwenda kujifunza namna ya Kudhibiti Demokrasia na Kuongoza Kidikteta''

Zitto '' Hauwezi kupamnana na UFISADI kama haumpi nguvu ya Kiutendaji wa CAG''

Zitto ''Kwa hali Hii anayokwenda MAGUFULI AJIANDAE KUWA RAIS WA TERM MOJA kwa sababu watanzania hawataweza kuvumilia kutawaliwa, kuminywa na kuburuzwa na Rais DIKTETA KAMA YEYE''

Zitto '' CCM wamdhibiti MAGUFULI, na wasipomdhibiti sisi na Watanzania Tutamdhibiti''

Zitto '' Hatutakaa Kimya hata kama atatufunga, akimfunga Zitto watazaliwa wakina Zitto wengine, na kwenye hili hatutakaa Kimya, tutasimama kidete mpaka nchi irudi kwenye misingi''

Zitto ''IGP ameagizwa na MAGUFULI anikamate, lakini hawezi kunikamata bila kufuata utaratibu, hawawezi kunikamata kwa kunivizia, viongozi hatukamatwi kwa kuviwa viziwa, tumewaonyesha kwamba Polisi wanaweza klutukamata kwa kufuata terms zetu na sio zao''

Zitto '' Karibuni kesho saa tisa kwenye Kongamano letu, Hatuwezi kuacha kufanya siasa, lazima tuendelee kufanya siasa, mmeudhuria mikutano yetu hamjaona hata sisimizi amekanyagwa''

Zitto '' Wanasema Bajeti imeongezeka kwa 32% ukweli ni kwamba Bajeti imeshuka kwa maana Dola imeporomoka''

Zitto ''CCM wamdhibiti mwanachama wao MAGUFULI, wasipomdhibiti sisi Tutamdhibiti''

MASWALI

1. Jambo leo
Naomba unikumbushe sheria inayoruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano na makongamano

Zitto ''Sheria ya Vyama vya siasa namba 5 ya mwaka 1992 inaruhusu vyama vya siasa kufanya siasa, makongamano na mikutano ni sehemu ya siasa, hatuhitaji kuomba kibali

2. SWALI
Je, mkutano utarushwa Live?

Zitto ''Tutaweka Utaratibu ili watanzania wengi zaidi waweze kushiriki kwenya kongamano''

Zitto ''Polisi hawana mamlaka ya kisheria Kuzuia Mikutano ya vyama vya siasa, tunaipongeza Chadema kufungua kesi ya kikatiba mwanza, sisi tunafungua hapa Dar, na tunavitaka vyama vingine vifungue kesi ili ziwe nyingizaidi kudai haki''

Zitto ''Kama serikali haifanyi sawa sawa ni wajibu wetu kuwakosoa, na tutawakosoa tutawakosoa kama tulivyokuwa tukifanya serikali iliyopota...serikali ya sasa haina uvumilivu''

Zitto ''Bunge limenisimamisha Ubunge, tutatumia Forums nyingine kuwatetea wananchi na Demokrasia.Hatuhitaji kibali cha mtu yeyote kufanya kongamano''
 

Attachments

  • Act wazalendo.png
    Act wazalendo.png
    108 KB · Views: 204
Kama ataongelea chochote kuhusu bajeti waandishi wa habari na nyie kakamaeni muulizeni hayo unayoyasema kwa nini usiwakabidhi wabunge wenzio wa upinzani walioko bungeni ili wayatumie kuchangia bungeni ambako yangetumika kufanya maamuzi pia? Kwa nini aamue kuyasema nje ya bunge?

Waandishi ulizeni maswali kakamavu msiishie tu kuchukua picha na kwenda kuandika zitto kasema!! Na nyie je mlisemaje tunataka kuona na nyie upande wenu mliuliza maswali yepi yaliyokakamaa.
 
Kusoma sio kuelimika,kwani zitto anashindwa nini kuyasema hayo bungeni ambako kuna msaada mkubwa,wa kulisaidia taifa kuliko huko vijiweni
 
Asante tunasubiri kwa hamu, na pia kusikia jinsi alivyotekwa ile jana!.

Pasco

Vipi tena mkuu kumbe kulikuwa na mpaka utekaji?
Bora hili asilisemee wataharibu nchi hii wasipokuwa makini! Tusijegeuka kama Kenya na mambo ya ugaidi.
 
Kama ataongelea chochote kuhusu bajeti waandishi wa habari na nyie kakamaeni muulizeni hayo unayoyasema kwa nini usiwakabidhi wabunge wenzio wa upinzani walioko bungeni ili wayatumie kuchangia bungeni ambako yangetumika kufanya maamuzi pia? Kwa nini aamue kuyasema nje ya bunge?

Waandishi ulizeni maswali kakamavu msiishie tu kuchukua picha na kwenda kuandika zitto kasema!! Na nyie je mlisemaje tunataka kuona na nyie upande wenu mliuliza maswali yepi yaliyokakamaa.

Mbona povu babu? Wakakamae kwani wao marehemu? Hebu twende taratibu.

Awakabidhi kwani amekwambia anatoa maoni yake au ya upinzani? Au unadhani kila mtu ana siasa za kuungana mkono? Vipi kama hao wenzake hawayakubali? Kuna sheria namba ngapi ya katiba ya nchi gani inamzuia kuyasema nje ya bunge?

Leo ndio unaona faida ya waandishi eti? Unawatuma wakaulize. Mbona hukuwatuma wakaulize kati ya Barabara ya kwenda kwa Mzee wa Upako na lile daraja la kuvuka kwa kamba Mbeya nini kinapaswa kupewa kipaumbele?
 
Safi sana kiongozi zitto kabwe kwa ufafanuzi mzuri hapa kwa ss waandishi wa habari tunazidi kukuelewa
 
Back
Top Bottom