Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe: Oktoba 3 tutatangaza Mgombea wa Urais atakayewakilisha Upinzani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,492
9,265
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema vyama vya Upinzani nchini vimekubaliana kumuunga mkono Mgombea mmoja wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania na pia, kwa upande wa Zanzibar.

Zitto ameongeza kuwa Oktoba 3, 2020 watatangaza ni nani hasa atasimama kama Mgombea Urais katika mkutano wa hadhara utakaohusisa CHADEMA, ACT Wazalendo na vyama vingine vya upinzani.

Amesema ACT-Wazalendo wameshajadiliana na wameshawasilisha mapendekezo yao kwa CHADEMA na baada ya pande zote kukamilisha mazungumzo watatangaza makubaliano yatakayofikiwa.
 
Tayari bundi ametua huko upinzani, vipi kujusu Membe yeye si alichukua fomu ya kugombea uraisi kupitia ACT wazalendo sasa huyu watakae muunga mkono tofauti na membe ni nani, kwaiyo uwekezaji wa membe kwa ACT ni bure kabisa au ndio wameamua kumchinjia baharini
 
Kimenukaaaaa, mwamba ameshapita.. Mwanamayu akachunge ng'ombe sasa.
Wamemchinjia baharini siasa hizi kweli hazina muamana usisahau kumpigia kura yako mh Magufuli maana yeye anatufufaa hawa wengine ni janja janja

2526615_1600781541524.png
 
Wamemchinjia baharini siasa hizi kweli hazina muamana usisahau kumpigia kura yako mh magufuli maana yeye anatufufaa hawa wengine ni janja janja View attachment 1577547
Anawafaaa watu wa Chato tu. Magufuli ni Mbinafsi, mbaguzi wa kidini, kikanda, kichama na kikabila.

Fisadi anayezuia wenzake wasifanye ufisadi ili abaki yeye na mpwa wake kwenye upigaji
 
Tayari bundi ametua huko upinzani, vipi kujusu membe yeye si alichukua fomu ya kugombea uraisi kupitia ACT wazalendo sasa huyu watakae muunga mkono tofauti na membe ni nani, kwaiyo uwekezaji wa membe kwa ACT ni bure kabisa au ndio wameamua kumchinjia baharini
Mbobezi hawezi kukubali kirahisi hivyo.
 
Pole nyingi zimuendee Kachero!!

Urais uliomtoa CCM,hata huko uhamishoni kaishia kuweka jina kwenye fomu za NEC tu.

From the beginning to the end, LOSERS LOSE!
 
Back
Top Bottom