Zitto Kabwe: Nusu ya walimu wanalipwa mishahara ya bure, hawafundishi

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Baada ya Hussein Bashe kusema ni watu waliofeli, Zitto Kabwe nae amesema nusu ya walimu hawafanyi kazi na ndio 'watumishi hewa haswa'
Ameongezea pia utafiti uliofanyika na Benki ya Dunia na REPOA ukitembelea ghafla kwenye shule za umma utakuta walimu hawapo shuleni

 
Ni kweli, hasahasa kwenye hizi shule za kata hali ni mbaya sana, walimu hawafundishi na wapo shuleni na headmaster wapo. Hali hii ni mbaya zaidi hasa mikoa ya kanda ya ziwa.
 
CCM washazoea kusikia na kudharau michango ya wapinzani hata kama inamashiko.ndio maana wameamua Bunge.liwe offline ili tusisikie michango mizuri kama hii wanayoambiwa na kupuuza.
 
Hili hata halina ubishi, walimu tubadilike. Hasira zetu juu ya serikali tusizihamishie kwa wanafunzi wasio na uwezo wa kujitetea. Tunawadhurumu watoto haki zao na baadae tunazalisha vijana wasiojielewa, wavuta bangi, wazurulaji n.k
 
....ndio nimeona kwenye taarifa ya habari ITV saa mbili usiku,wanafunzi wa UDOM wanalalamika wana mwezi mmoja hawajawaona walimu madarasani!
 
kiukweli wabunge wameamua kuwashupalia walimu. mbona hawazungumzii changamoto kubwa zilizopo shule za umma ? hususani ukosefu wa walimu wa sayansi na hisabati? je kina zitto hawalioni hili? any way kwa hiyo wabunge wanalipwa mishahara ya halali?
 
Kanikumbusha enzi za shuleni..... mwalimu anakuambia " NIFUNDISHE AMA NISIFUNDISHE, MSHAHARA WANGU UPO CONSTANT KAMA Pi, NA NINAWAFUNDISHA KWA HURUMA YANGU TU... "

alafu kesho unawakuta wanalalamikia kupata ongezeko la pesa huku hata waipatayo hawaistahili..

WAALIMU WA SHULE ZA SERIKALI YAWAPASA MBADILIKE
 
kabla yakumtupia lawama mwalimu hebu rudini nyuma kidogo angalieni hali ya huyu mwalimu; mshahara kiduchu.mazingira ya kazi bado ni shida.darasani unapewa watoto nyomi.acheni jamani.

kuna baadhi ya waalimu wachache wa shule za serikali wanafanya kazi vyema katika mazingira hayohayo magumu na kufaulisha wanafunzi kuliko hata wa private schools.... ni ubunifu tu wa kukabiliana na mazingira isipokuwa kwa waalimu wa vijijini ambao hukutana na mazingira yasiyowezekana kabisaaa

TUACHE SABABU ZA KUUHALALISHA UDHEMBE
 
Haya mambo ya walimu ni ya muda mrefu sana......anachosema Zitto ni ukweli....yani ni kwamba lazima pande mbili zipatanishwe
Mwalim apewe motisha ya kufundisha vile vile awajibishwe kwa hilo..
Conspiracy ni kwamba ukiongeza mshahara wa walimu. Mishahara ngazi zote zitapanda anzia serikalini hadi sekta binafsi na hivyo kufanya maisha kuwa magum kias kwa mwananchi wa kawaida..( jicho la tatu linahitajika kwa hili)
Maana kwa waajiri watongeza cost of production na importer wataongeza WACP,
So ni kama unarud square one...
Otherwise vitu kama nyumba, mazingira bora ya kaz ni vitu muhim sana..walim wa zaman walifundisha kwa weled sana, japo maslaj yao yalikuwa duni zaid
 
kiukweli wabunge wameamua kuwashupalia walimu. mbona hawazungumzii changamoto kubwa zilizopo shule za umma ? hususani ukosefu wa walimu wa sayansi na hisabati? je kina zitto hawalioni hili? any way kwa hiyo wabunge wanalipwa mishahara ya halali?
Mkuu hujawahi kusikia kuwa wabunge wa ccm na upinzani kwenye maslahi wote ni familia moja tu, hawazungumzii mishahara yao.... Ila wanalaum waalim, japo zitto kaomba pia walim walipwe vizuri
 
Back
Top Bottom