Zitto Kabwe: Njia nane(8) za kuwa Dikteta

Hicho ni kilio cha hako katoto kanavyonyooshwa. Fursa za kufanya ufisadi kalizokuwa kamezoea zimekatwa. Mali lukuki kalizochuma kifisadi mara tu baada ya kuhitimu ka BA(Arts) na kubahatika kutinga bungeni, sasa zinafuatiliwa na TRA, TAKUKURU na mamlaka zingine za serikali na zingine zimeanza kuwaka moto zenyewe. Kamebanwa bara bara, hata bungeni kamenyimwa ruhusa ya kuongea cho chote. Kamebaki kutapatapa kwenye mi facebook, twiter, Instagram na mitandao mingine ya kijamii. Soon katakuwa kakipumzika Mirembe. Inatia huruma lakini mafisadi lazima waendelee kunyooshwa. Kelele zao za maumivu wanayoyapata iwe faraja kwetu. Wazee kama akina Lembeli walikaa kwenye nafasi ya ubunge kwa kipindi kirefu kuliko haka katoto lakini hawana mali yo yote ya maana kama haka katoto. Hawana mi Hammer au majumba ya maana. Wamebaki kuwa wazee wa nyeti za kuku tu.
 
Haka katoto mi nilikapuuza toka jk alipokaweka kwenye tume ya rais ya nishati na madini..kakatulia kabisa..hako kakikosa fursa huwa kanafukuta sana,.na hivi kalikataaga posho enzi zile kanaenda ikulu kuchukua hela, kazi ipo

Ndiyo tuvijana tulitobakia humu mwenye siasa ila tunafanya siasa chonganishi.
Sasa serikali ikituweka mikono salama utasikia tunalia machozi ya kujaza ndoo na bahari

Lakini, vijana wengi wamepoteza dira.
 
Hicho ni kilio cha hako katoto kanavyonyooshwa. Fursa za kufanya ufisadi kalizokuwa kamezoea zimekatwa. Mali lukuki kalizochuma kifisadi mara tu baada ya kuhitimu ka BA(Arts) na kubahatika kutinga bungeni, sasa zinafuatiliwa na TRA, TAKUKURU na mamlaka zingine za serikali na zingine zimeanza kuwaka moto zenyewe. Kamebanwa bara bara, hata bungeni kamenyimwa ruhusa ya kuongea cho chote. Kamebaki kutapatapa kwenye mi facebook, twiter, Instagram na mitandao mingine ya kijamii. Soon katakuwa kakipumzika Mirembe. Inatia huruma lakini mafisadi lazima waendelee kunyooshwa. Kelele zao za maumivu wanayoyapata iwe faraja kwetu. Wazee kama akina Lembeli walikaa kwenye nafasi ya ubunge kwa kipindi kirefu kuliko haka katoto lakini hawana mali yo yote ya maana kama haka katoto. Hawana mi Hammer au majumba ya maana. Wamebaki kuwa wazee wa nyeti za kuku tu.

Tuvijana hutu twa leo tumeharibika sana siyo.kama.enzi zetu zile za 1960s na 1970s.
 
anasahau mfumo wa chama chake ni zaidi ya udiktea ni ufalme...
Kwa mfumo wa act hakuna mwenye mamlaka kumzidi yeye.
Hivi Mbunge hawezi kuwa dikteta? Maana naona baadhi ya sifa zinamsadifu Zitto mwenyewe.
Nyie wapumbavu acheni kudandia mambo...dikteta anakuwa na vyombo vya dola. Sasa hao mnaowataja wana polisi, wana jeshi au wana usalama wa taifa? Wana vyombo gani ambavyo viko juu ya sheria? Kumbuka kinachomwezesha Rais kuwa dikteta ni kuwa na vyombo hivyo na yeye akiwa juu ya sheria...hawezi kushtakiwa.
 
Tuvijana hutu twa leo tumeharibika sana siyo.kama.enzi zetu zile za 1960s na 1970s.
Enzi hizo za 1960s na 1970s vijana walikuwa na nidhamu ya hali ya juu. Tuvijana twa siku hizi kama tu Zitto hatujawahi kutokea po pote duniani huko karne za nyuma. Ni vi new species or strains of homosapiens ambavyo vikipewa mamlaka ya kuongoza nchi vitasababisha mwisho wa dunia. Such strains must not be tolerated. Lazima tuvinyooshe. Vikishindikana kunyooka tunavikunja.
 
Siasa jamani.. Leo marafiki, kesho maadui, keshokutwa no one knows.. Juzi tu like a month ago, Mh Zitto alimsifia sana Mh. Rais wetu JPM wakiwa Kigoma.. Sisi wana CCM tukapata furaha na kupiga makofi kuona hilo.. Narudia juzi kati kule Kigoma, tena Zitto alisema anamuunga mkono Mh. Rais wetu na serikali yake, akaenda mbali zaidi na kusema mawaziri wamempa ushirikiano sana ktk serikali hii ya JPM.. Na slogan ilikuwa MAENDELEO KWANZA.. VYAMA BAADAE..

Sasa ghafla tena yamekuwa haya..

Siasa haina rafiki wa kudumu, ukijua haya wala hupati shida, wanasiasa wanacheki maslahi yao tu...

Dunia hii, Extra mind is needed kuwajua hawa viumbe "POLITICIANS", i know them well, wengine muwajue pia.
Zitto anatafuta Ulaji,bado uteuzi wa waziri wa madini.
Huyo kijana anahaha kikweli kweli,lakini naona Magu hana mpango nae,ametumika sasa ametupwa kwenye dampo.
 
kweli nimeamini kuwa nyani haoni....

anasahau mfumo wa chama chake ni zaidi ya udiktea ni ufalme...

Kwa mfumo wa act hakuna mwenye mamlaka kumzidi yeye. hata mwenyekiti yupo chini yake.

zito ni mfalme wa act; kwa title ya kiongozi mkuu wa chama.

huyu ndio yupo busy kuita wenzake majina ya hovyo amesahau kujijumuisha humo.

ngoja tumkumbushe mfalme wa act.
Yakupasa usome katiba ya hicho chama, kuna mengi ya kujifunza
 
( Na Zitto Kabwe, kutoka Vitabu na Majarida kadhaa )

24/9/2017

1 Chaguliwa kuwa Rais Hakikisha kwanza unakuwa na mamlaka ya dola vizuri zaidi kwa kuchaguliwa kwa kura. Adolf Hitler wa Ujerumani alihitaji chama chenye nguvu kumwezesha kuwa Kiongozi wa Ujerumani. Huwezi kuwa Kiongozi wa Imla bila ya kuwa na nguvu za dola. Vladimir Putin amekuwa akichaguliwa kila wakati na hata alipomaliza muhula wake aliweza kuweka mtu wa kumshikia nafasi kwa muda na kurudi tena.

2 Weka mazingira ya Udharura Udharura unaweza kuwa nafasi kwa Mtawala anayetaka kuwa dikteta kutekeleza nia yake hiyo. Udharura unasaidia kutunga sheria ambazo zinampa nafasi Rais kufanya maamuzi bila kutegemea vyombo vingine. Aghalabu anayehoji maamuzi hayo huitwa si mzalendo, msaliti, mhaini nk. Hitler wa Ujerumani alituma vijana wake kuwasha moto jengo la Bunge ili kuweka udharura. Alilaumu wakomunisti kuwa ndio wamechoma moto jengo hilo na hivyo kuanza kuwashughulikia. Nchini Burundi, Pierre Nkurunzinza aliamua kufanya mapinduzi bandia ili aweze kutekeleza nia yake ya kukaa kwenye madaraka daima. Baadhi ya Watawala huanzisha ajenda za ‘ kizalendo’ ili kuweka udharura. Ajenda hizo ni kama vile tishio la kuvamiwa na nchi nyengine, tishio la kuporwa mali zao asili nk. Mtawala Dikteta hutangaza vita zake binafsi na kuzifanya ni vita za kitaifa na yeyote anayehoji ama umuhimu wa vita hizo au namna zinavyoendeshwa hushughulikiwa na hata kupotezwa.

3 Pitisha sheria ya Hali ya hatari Kukiwa na sheria ya hali ya hatari katiba ya nchi inasimama na nchi inaendeshwa kwa amri za Rais. Hapa Mtawala Dikteta anakuwa amepata fursa ya kutenda yale tu anayotaka yeye. Kwa baadhi ya nchi za Kiafrika hili halihitajiki sana. Rais anaweza tu kusema tupo kwenye vita Fulani na baadhi ya sheria kusimamishwa nan chi kuendeshwa kwa Amri ya Rais, halali ama batili.

4 Chezea Uchaguzi Hapa Dikteta anaamua kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika na yeye kushinda. Atahakikisha kuwa anabana vyama vingine kukua kwa kufunga viongozi wake au kuhakikisha wanakimbilia uhamishoni, wapiga kura watateswa na kulazimishwa kupigia kura Dikteta huyo na hata matokeo kutangazwa kutokana na matakwa ya Dikteta. Hapa Afrika, watawala wengi wamekuwa wakifanya hili bila woga. Uganda, Rwanda, Zambia, Zimbabwe na Angola imeshuhudia chaguzi za namna hii hata kama baadhi ya nchi watawala wake sio Madikteta haswa, ama ni madikteta uchwara au ni madikteta mamboleo.

5 Pitisha sheria kandamizi Sheria zinazohusu uhuru wa vyombo vya habari huwa ni za kwanza kuanza kubadilishwa ili kuziba uhuru wa mawazo na fikra mbadala. Kisha sheria zinazotoa uhuru wa vyama vya siasa na vyama vya kijamii hasa asasi zisizo za kiserikali ( NGO ) huathirika.

6 Pitisha sheria wezeshi Hizi sheria huwezeshwa na sheria nyengine ambazo zaweza kupelekea chama tawala kuwa chama pekee kiuhalisia kwenye nchi husika. Viongozi wa vyama wataishia lupango kwa makosa kama uhaini ili kuhakikisha kuwa vyama vinakosa viongozi na hivyo kutokukua.

7 Futa kabisa Upinzani Hatimaye mtu yeyote wa upinzani huuwawa. Wakati hilo linatekelezwa mihimili mingine ya Dola huminywa ili kubakiza mhimili mmoja tu kutawala. Mhimili wa kutunga sheria huwekwa mfukoni mwa Mtawala na kuwezesha kupitisha sheria wezeshi. Mhimili wa mahakama hufuata maagizo ya mtawala kuhusu kesi mbalimbali zinazofikishwa mbele yake. Lengo ni kuhakikisha kuwa sio Upinzani wa siasa tu unaofutwa bali pia upinzani wa mihimili. Wabunge wasiowatiifu huuwawa, majaji wasiofuata maagizo humalizwa.

8 Jitangaze kuwa wewe ni Mtumishi wa Mungu Mtawala Dikteta hujiita kuwa yeye ni mtu wa Mungu na hutaka kuombewa kila mara. Hujiona ni mtume na yote afanyayo anatumwa na Mungu. Nani atamhoji Mungu?

Njia 8 za kuzuia Udikteta kwenye nchi za Afrika? Inshallah tusome hapa mnamo 24/9/2018.
Bora uongee kwa staili hiyo wasikushike kwa uchochezi.. naona mama fulani na alopewa usimamizi wa nyumba wakiiguswa nidirect
 
kweli nimeamini kuwa nyani haoni....

anasahau mfumo wa chama chake ni zaidi ya udiktea ni ufalme...

Kwa mfumo wa act hakuna mwenye mamlaka kumzidi yeye. hata mwenyekiti yupo chini yake.

zito ni mfalme wa act; kwa title ya kiongozi mkuu wa chama.

huyu ndio yupo busy kuita wenzake majina ya hovyo amesahau kujijumuisha humo.

ngoja tumkumbushe mfalme wa act.
Sasa ukiongelea chama out of country ntazidi kukuona wewe ni stroke tu
 
Achen uzwazwa bhana, Focus kwenye nondo alizotoa Zitto, Kama tulimpokea Lowasa tuliyemuita fisadi mkuu na kuwa mkombozi wetu 2015, Mambo ya 2008 kwenye kamat za madini hayana mantiki leo tunapopambana na udikteta uchwara nchini.
Ufisadi hampambani nao tena sa hivi,hahah
 
kweli nimeamini kuwa nyani haoni....

anasahau mfumo wa chama chake ni zaidi ya udiktea ni ufalme...

Kwa mfumo wa act hakuna mwenye mamlaka kumzidi yeye. hata mwenyekiti yupo chini yake.

zito ni mfalme wa act; kwa title ya kiongozi mkuu wa chama.

huyu ndio yupo busy kuita wenzake majina ya hovyo amesahau kujijumuisha humo.

ngoja tumkumbushe mfalme wa act.
Unaijua katiba ya chama chake?
 
Back
Top Bottom