Zitto Kabwe: Njia nane(8) za kuwa Dikteta

5 Pitisha sheria kandamizi Sheria zinazohusu uhuru wa vyombo vya habari huwa ni za kwanza kuanza kubadilishwa ili kuziba uhuru wa mawazo na fikra mbadala. Kisha sheria zinazotoa uhuru wa vyama vya siasa na vyama vya kijamii hasa asasi zisizo za kiserikali ( NGO ) huathirika.
4 Chezea Uchaguzi Hapa Dikteta anaamua kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika na yeye kushinda. Atahakikisha kuwa anabana vyama vingine kukua kwa kufunga viongozi wake au kuhakikisha wanakimbilia uhamishoni, wapiga kura watateswa na kulazimishwa kupigia kura Dikteta huyo na hata matokeo kutangazwa kutokana na matakwa ya Dikteta. Hapa Afrika, watawala wengi wamekuwa wakifanya hili bila woga. Uganda, Rwanda, Zambia, Zimbabwe na Angola imeshuhudia chaguzi za namna hii hata kama baadhi ya nchi watawala wake sio Madikteta haswa, ama ni madikteta uchwara au ni madikteta mamboleo.
2 Weka mazingira ya Udharura Udharura unaweza kuwa nafasi kwa Mtawala anayetaka kuwa dikteta kutekeleza nia yake hiyo. Udharura unasaidia kutunga sheria ambazo zinampa nafasi Rais kufanya maamuzi bila kutegemea vyombo vingine. Aghalabu anayehoji maamuzi hayo huitwa si mzalendo, msaliti, mhaini nk. Hitler wa Ujerumani alituma vijana wake kuwasha moto jengo la Bunge ili kuweka udharura. Alilaumu wakomunisti kuwa ndio wamechoma moto jengo hilo na hivyo kuanza kuwashughulikia. Nchini Burundi, Pierre Nkurunzinza aliamua kufanya mapinduzi bandia ili aweze kutekeleza nia yake ya kukaa kwenye madaraka daima. Baadhi ya Watawala huanzisha ajenda za ‘ kizalendo’ ili kuweka udharura. Ajenda hizo ni kama vile tishio la kuvamiwa na nchi nyengine, tishio la kuporwa mali zao asili nk. Mtawala Dikteta hutangaza vita zake binafsi na kuzifanya ni vita za kitaifa na yeyote anayehoji ama umuhimu wa vita hizo au namna zinavyoendeshwa hushughulikiwa na hata kupotezwa.
Sasa hii akili anaipata wapi? nchi jirani au?
 
Haka katoto mi nilikapuuza toka jk alipokaweka kwenye tume ya rais ya nishati na madini..kakatulia kabisa..hako kakikosa fursa huwa kanafukuta sana,.na hivi kalikataaga posho enzi zile kanaenda ikulu kuchukua hela, kazi ipo

Achen uzwazwa bhana, Focus kwenye nondo alizotoa Zitto, Kama tulimpokea Lowasa tuliyemuita fisadi mkuu na kuwa mkombozi wetu 2015, Mambo ya 2008 kwenye kamat za madini hayana mantiki leo tunapopambana na udikteta uchwara nchini.
 
Baba Jesca AKA Dhalimu mtupu!
Nadhani kumejengeka tabia ya kuendekeza tabia za washenzi kutaka nasi watuambukize tabia ya kuona ushenzi kama tabia halali. Tungekuwa na wabunge kama 20 tuu toka pande zote mbili za bunge wenye uthubutu kama wa Lisu na kina Mbowe ujinga huu usingeota mizizi lakini ndio hivyo tena.
Raia wetu ndio hao kama hawa walio JF ambao upumbavu wameweka mbele hata kama wanakandamizwa wao ni ushabiki maandazi tuu. Mtu mdhalimu anaye kanyaga katiba hafai hata kuwapo madarakani.
 
Achen uzwazwa bhana, Focus kwenye nondo alizotoa Zitto, Kama tulimpokea Lowasa tuliyemuita fisadi mkuu na kuwa mkombozi wetu 2015, Mambo ya 2008 kwenye kamat za madini hayana mantiki leo tunapopambana na udikteta uchwara nchini.
Nondo kwa sababu amekosa fursa...kesho akipata fursa anafuta usemi..mambo ya kina mbowe na pesa za lowasa..halafu ifike hatua na nyie madogo muamke..mjifikirishe..sio kila kitu mnamezwa na mihemko
 
( Na Zitto Kabwe, kutoka Vitabu na Majarida kadhaa )

24/9/2017

1 Chaguliwa kuwa Rais Hakikisha kwanza unakuwa na mamlaka ya dola vizuri zaidi kwa kuchaguliwa kwa kura. Adolf Hitler wa Ujerumani alihitaji chama chenye nguvu kumwezesha kuwa Kiongozi wa Ujerumani. Huwezi kuwa Kiongozi wa Imla bila ya kuwa na nguvu za dola. Vladimir Putin amekuwa akichaguliwa kila wakati na hata alipomaliza muhula wake aliweza kuweka mtu wa kumshikia nafasi kwa muda na kurudi tena.

2 Weka mazingira ya Udharura Udharura unaweza kuwa nafasi kwa Mtawala anayetaka kuwa dikteta kutekeleza nia yake hiyo. Udharura unasaidia kutunga sheria ambazo zinampa nafasi Rais kufanya maamuzi bila kutegemea vyombo vingine. Aghalabu anayehoji maamuzi hayo huitwa si mzalendo, msaliti, mhaini nk. Hitler wa Ujerumani alituma vijana wake kuwasha moto jengo la Bunge ili kuweka udharura. Alilaumu wakomunisti kuwa ndio wamechoma moto jengo hilo na hivyo kuanza kuwashughulikia. Nchini Burundi, Pierre Nkurunzinza aliamua kufanya mapinduzi bandia ili aweze kutekeleza nia yake ya kukaa kwenye madaraka daima. Baadhi ya Watawala huanzisha ajenda za ‘ kizalendo’ ili kuweka udharura. Ajenda hizo ni kama vile tishio la kuvamiwa na nchi nyengine, tishio la kuporwa mali zao asili nk. Mtawala Dikteta hutangaza vita zake binafsi na kuzifanya ni vita za kitaifa na yeyote anayehoji ama umuhimu wa vita hizo au namna zinavyoendeshwa hushughulikiwa na hata kupotezwa.

3 Pitisha sheria ya Hali ya hatari Kukiwa na sheria ya hali ya hatari katiba ya nchi inasimama na nchi inaendeshwa kwa amri za Rais. Hapa Mtawala Dikteta anakuwa amepata fursa ya kutenda yale tu anayotaka yeye. Kwa baadhi ya nchi za Kiafrika hili halihitajiki sana. Rais anaweza tu kusema tupo kwenye vita Fulani na baadhi ya sheria kusimamishwa nan chi kuendeshwa kwa Amri ya Rais, halali ama batili.

4 Chezea Uchaguzi Hapa Dikteta anaamua kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika na yeye kushinda. Atahakikisha kuwa anabana vyama vingine kukua kwa kufunga viongozi wake au kuhakikisha wanakimbilia uhamishoni, wapiga kura watateswa na kulazimishwa kupigia kura Dikteta huyo na hata matokeo kutangazwa kutokana na matakwa ya Dikteta. Hapa Afrika, watawala wengi wamekuwa wakifanya hili bila woga. Uganda, Rwanda, Zambia, Zimbabwe na Angola imeshuhudia chaguzi za namna hii hata kama baadhi ya nchi watawala wake sio Madikteta haswa, ama ni madikteta uchwara au ni madikteta mamboleo.

5 Pitisha sheria kandamizi Sheria zinazohusu uhuru wa vyombo vya habari huwa ni za kwanza kuanza kubadilishwa ili kuziba uhuru wa mawazo na fikra mbadala. Kisha sheria zinazotoa uhuru wa vyama vya siasa na vyama vya kijamii hasa asasi zisizo za kiserikali ( NGO ) huathirika.

6 Pitisha sheria wezeshi Hizi sheria huwezeshwa na sheria nyengine ambazo zaweza kupelekea chama tawala kuwa chama pekee kiuhalisia kwenye nchi husika. Viongozi wa vyama wataishia lupango kwa makosa kama uhaini ili kuhakikisha kuwa vyama vinakosa viongozi na hivyo kutokukua.

7 Futa kabisa Upinzani Hatimaye mtu yeyote wa upinzani huuwawa. Wakati hilo linatekelezwa mihimili mingine ya Dola huminywa ili kubakiza mhimili mmoja tu kutawala. Mhimili wa kutunga sheria huwekwa mfukoni mwa Mtawala na kuwezesha kupitisha sheria wezeshi. Mhimili wa mahakama hufuata maagizo ya mtawala kuhusu kesi mbalimbali zinazofikishwa mbele yake. Lengo ni kuhakikisha kuwa sio Upinzani wa siasa tu unaofutwa bali pia upinzani wa mihimili. Wabunge wasiowatiifu huuwawa, majaji wasiofuata maagizo humalizwa.

8 Jitangaze kuwa wewe ni Mtumishi wa Mungu Mtawala Dikteta hujiita kuwa yeye ni mtu wa Mungu na hutaka kuombewa kila mara. Hujiona ni mtume na yote afanyayo anatumwa na Mungu. Nani atamhoji Mungu?

Njia 8 za kuzuia Udikteta kwenye nchi za Afrika? Inshallah tusome hapa mnamo 24/9/2018.
Hahahaha
Mbona kama ni yaleyale anapopita sizonje
 
Je udikteta huleta maendeleo?
Gadaffi alikuwa dikteta na nasikia walibya walineemeka kwa kiasi fulani.
The best way to development..leo watu wanaogopa kukwapua na kujimilikisha Mali ya umma..wakati kuna mtu alijimilikisha kiwanja cha TBC enzi za jk
 
kweli nimeamini kuwa nyani haoni....

anasahau mfumo wa chama chake ni zaidi ya udiktea ni ufalme...

Kwa mfumo wa act hakuna mwenye mamlaka kumzidi yeye. hata mwenyekiti yupo chini yake.

zito ni mfalme wa act; kwa title ya kiongozi mkuu wa chama.

huyu ndio yupo busy kuita wenzake majina ya hovyo amesahau kujijumuisha humo.

ngoja tumkumbushe mfalme wa act.
Nyie si ndio huwa mnamsifia Leo kawaponda kichwa mnalaum nini na si mmewapa vyeo hao
 
Nondo kwa sababu amekosa fursa...kesho akipata fursa anafuta usemi..mambo ya kina mbowe na pesa za lowasa..halafu ifike hatua na nyie madogo muamke..mjifikirishe..sio kila kitu mnamezwa na mihemko
Kila jambo na wakati wake, anayesema ukweli leo na ukaujua ni ukweli huna sababu ya kufikiria jana alisema nini. Zitto amezinduka na anasema anayoona kwa sasa hivyo hakuna sababu kujiuliza juzi alisema nini. Mbona Magu awali alisema mambo ambayo wapinzani waliyakubali hadi kufikia kusema anatekeleza ilani yao, lakini sasa amejipambanua kuwa sio mkweli na wanamuambia sio mkweli na anachukia na kutumia vibaya mamlaka ya katiba aliyopewa kuwaumiza wampingao?
 
The best way to development..leo watu wanaogopa kukwapua na kujimilikisha Mali ya umma..wakati kuna mtu alijimilikisha kiwanja cha TBC enzi za jk

Anyway hayo yote yamedhibitiwa mbona hata watafutaji halali mambo yao yanazidi kuwa mabaya?
 
kweli nimeamini kuwa nyani haoni....

anasahau mfumo wa chama chake ni zaidi ya udiktea ni ufalme...

Kwa mfumo wa act hakuna mwenye mamlaka kumzidi yeye. hata mwenyekiti yupo chini yake.

zito ni mfalme wa act; kwa title ya kiongozi mkuu wa chama.

huyu ndio yupo busy kuita wenzake majina ya hovyo amesahau kujijumuisha humo.

ngoja tumkumbushe mfalme wa act.
Chama kuwa na Mwenyekiti na kiongozi wa chama!Sijui waliichukua wapi hii!Akiwa na mamlka huyu ni zaidi ya Kim!
 
huyu naye naona kuna kitu anakitafuta na nadhani soon atakipata tuu ,kama jinsi pyong yong ilivyosema kuwa marekani ijiandae kupokea vifurushi vya kutosha kutoka korea
 
kweli nimeamini kuwa nyani haoni....

anasahau mfumo wa chama chake ni zaidi ya udiktea ni ufalme...

Kwa mfumo wa act hakuna mwenye mamlaka kumzidi yeye. hata mwenyekiti yupo chini yake.

zito ni mfalme wa act; kwa title ya kiongozi mkuu wa chama.

huyu ndio yupo busy kuita wenzake majina ya hovyo amesahau kujijumuisha humo.

ngoja tumkumbushe mfalme wa act.
Unapoongea kuhusu ishu kama hii jaribu kuishirikisha akili yako japo kidogo. Kwa hiyo kwa point yako hiyo unataka kutuaminisha kwamba Sizonje baada ya kuyaona ya ACT akaamua na yeye kulipiza!!
 
The best way to development..leo watu wanaogopa kukwapua na kujimilikisha Mali ya umma..wakati kuna mtu alijimilikisha kiwanja cha TBC enzi za jk
Safi sana.Basi na sisi tujaribu.Maana nasikia Kagame, Museveni, Kabila na Mugabe wametumia utawala huo na wamefaniwa kuleta development.
 
Safi sana.Basi na sisi tujaribu.Maana nasikia Kagame, Museveni, Kabila na Mugabe wametumia utawala huo na wamefaniwa kuleta development.
Mugabe vikwazo, museveni yupo kimadaraka zaidi
 
Siasa jamani.. Leo marafiki, kesho maadui, keshokutwa no one knows.. Juzi tu like a month ago, Mh Zitto alimsifia sana Mh. Rais wetu JPM wakiwa Kigoma.. Sisi wana CCM tukapata furaha na kupiga makofi kuona hilo.. Narudia juzi kati kule Kigoma, tena Zitto alisema anamuunga mkono Mh. Rais wetu na serikali yake, akaenda mbali zaidi na kusema mawaziri wamempa ushirikiano sana ktk serikali hii ya JPM.. Na slogan ilikuwa MAENDELEO KWANZA.. VYAMA BAADAE..

Sasa ghafla tena yamekuwa haya..

Siasa haina rafiki wa kudumu, ukijua haya wala hupati shida, wanasiasa wanacheki maslahi yao tu...

Dunia hii, Extra mind is needed kuwajua hawa viumbe "POLITICIANS", i know them well, wengine muwajue pia.
 
Back
Top Bottom