Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Juzi Meya wa Mwanza ndugu James Bwire alikamatwa na kuwekwa ndani wakati wa ziara ya Rais huko Mwanza.
Ninalaani tabia ambayo imeanza kushika mizizi ya kukamata viongozi wa serikali za mitaa nyakati za ziara za viongozi wakuu.
Meya Bwire ana bahati, mwenzake wa Kibondo Ndugu Simon Kanguye alikamatwa siku moja kabla ya Rais kufika Kigoma tarehe 21 Julai 2017 na hajaonekana mpaka leo.
Viongozi wa ALAT wanapaswa kuchukua hatua na kupaza sauti dhidi ya udhalimu huu dhidi yao. Kukaa kimya ni kuunga mkono utekaji wa viongozi unaofanywa na taasisi tunazozijua lakini tunajifanya ni watu wasiojulikana.