Zitto Kabwe: Ninalaani kukamatwa kwa viongozi wa serikali za mitaa wakati wa ziara za viongozi wakuu

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Juzi Meya wa Mwanza ndugu James Bwire alikamatwa na kuwekwa ndani wakati wa ziara ya Rais huko Mwanza.

Ninalaani tabia ambayo imeanza kushika mizizi ya kukamata viongozi wa serikali za mitaa nyakati za ziara za viongozi wakuu.

Meya Bwire ana bahati, mwenzake wa Kibondo Ndugu Simon Kanguye alikamatwa siku moja kabla ya Rais kufika Kigoma tarehe 21 Julai 2017 na hajaonekana mpaka leo.

Viongozi wa ALAT wanapaswa kuchukua hatua na kupaza sauti dhidi ya udhalimu huu dhidi yao. Kukaa kimya ni kuunga mkono utekaji wa viongozi unaofanywa na taasisi tunazozijua lakini tunajifanya ni watu wasiojulikana.
 
Duh aisee! Yule Meya hajaonekana? Jamani kuweni na huruma juu ya hawa viumbe wa Mungu
 
huyu wa mwanza si nimesikia keshaachiwa na kataka kuongea na mkuu faragha amueleze uozo, au ni mwingine
 
Meya Bwire ana bahati, mwenzake wa Kibondo Ndugu Simon Kanguye alikamatwa siku moja kabla ya Rais kufika Kigoma tarehe 21 Julai 2017 na hajaonekana mpaka leo.
Zitto ni muongo sana.Kanguye yupo mtaani,uzushi mwingine hauna maana kabisa
 
Back
Top Bottom