Zitto Kabwe ni muumini wa Azimio la Arusha anayeushangaa uongozi wa Wajamaa Dr Magufuli na Dr Bashiru Ally!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,769
141,632
Kwa nyakati tofauti mbunge wa Ujiji ambaye pia ni kiongozi mkuu wa ACT amekuwa akijitambulisha kama muumini mzuri wa azimio la Arusha lililoasisiwa na mwalimu Nyerere.

Wengi tulitegemea Zitto kwa imani yeke hiyo ya kijamaa basis angekuwa mstari wa mbele kumuunga mkono mjamaa wa ukweli Rais Magufuli ambaye amevalia njuga kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufuaisha watanzania wote.

Cha ajabu Zitto amekuwa kinara wa kubeza jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli akisaidiwa na mjamaa mwingine Dr Bashiru katika kuirudisha nchi kwenye mstari.

Najiuliza tu Zitto analijua vizuri azimio la Arusha au alivamia tu akidhani ndio azimio la Zanzibar?

Dr Magufuli endelea kuchapa kazi wanaoshangaa shangaa acha washangae.
Maendeleo hayana vyama!
 
Sera ya ujamaa na kujitegemea ilipitiwa upya na vikao rasmi vya chama cha mapinduzi vya mwaka 1992. Baada ya hapo tukaingia kwenye sera ya soko huria ambayo ndiyo inayoendelea mpaka sasa. Mpaka sasa haijatungwa Sera tofauti na ya soko huria ya 1992.
 
Back
Top Bottom