Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,802
- 11,961
Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa ndoto yake siku moja ni kuiongoza Tanzania akiwa katika nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
"Mimi urais nautaka, sababu naamini nina uwezo, nina maarifa, nina uzoefu wa kutosha katika siasa kuweza kuiongoza nchi yetu kupiga hatua mbele, lakini siwezi kusema moja kwa moja kuwa nitagombea Urais waka 2025
“Uamuzi wa kugombea unatokana na kudra za Mwenyezi Mungu chama lazima dhamana na baadaye wananchi watoe dhamana.
“Pia kuna kilio cha ushirikiano wa vyama vya upinzani ili kupambana dhidi ya Chama Cha Mapinduzi, kama tutashirikiana inawezekana mgombea nikawa mimi au nisiwe akawa mwingine,” Zitto
Video: Mwananchi