Zitto Kabwe na 'Saini za Wabunge 70' za kumg'oa Pinda - Tafsiri yangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto Kabwe na 'Saini za Wabunge 70' za kumg'oa Pinda - Tafsiri yangu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Apr 20, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Apr 20, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Leo asubuhi wakati nikifanya ' jogging' kwenye mitaa ya Dar es Salaam niliwasikia watu wa kawaida kabisa wakijiuliza na kujadili; " inakuwaje Serikali iwalipe marehemu mishahara huku sisi tulio hai hatuna hata uhakika wa milo miwili ya siku?" Wanauliza watu wa mitaani.

  Naam, nchi yetu imekumbwa na mafuriko ya habari. Kule bungeni Dodoma kuna moto unawaka. Zimeitishwa sanini 70 ili Jumatatu ipigwe kura ya kukosa imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. Ndio, kuna wanaotaka Pinda ang'oke, na labda kutolewa kafara, maana, siamini kama tatizo la msingi ni Pinda, bali ni la kimfumo zaidi. Na jana kuna mbunge wa CCM kayasema makali yafuatayo;

  "Mheshimiwa Naibu Spika, inashangaza na kusikitisha kuwa nchi inatafunwa. Wanaofanya haya ni mawaziri wetu. Nchi inakufa na tuelewe kuwa Tanzania sio mali ya CCM, ni ya Watanzania wote.
  "Mawaziri wetu wamekuwa mchwa, wanaangamiza nchi na leo nitamtaja waziri anayeongoza kwa kutafuta fedha za Watanzania. Ni Waziri wetu wa Fedha, Mustafa Mkulo. Ameuza viwanja, amelidanganya Bunge baada ya kuivunja CHC,"- Deo Filikunjombe ( CCM) Bungeni jana.

  Lakini ya jana yalitanguliwa na ya juzi; Mbunge mwanadamizi wa CCM Godfrey Zambi aliyasema makali haya;

  " CCM inaweza kung'olewa madarakani katika uchaguzi wa mwaka 2015 endapo kasi ya ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma itaendelea kama ilivyo sasa"- Godfrey Zambi ( CCM, Mbozi Mashariki).

  Kauli za wabunge hao wawili wa CCM zinatoa tafsiri ya kilio cha wabunge wa CCM kuomba msaada kwa anayeweza kuwasaidia. Inatoa tafsiri pia kuwa hicho ni kilio cha wabunge wengi wa CCM. Kwamba hayo ndiyo wanayaongea hata chini chini.

  Ndio, wananung'unika na wameanza kuiona adhabu wanayokwenda kuipata kutoka kwa wananchi ifikapo 2015. Wanaona pia, kuwa ' kisungura' hiki kidogo kinachopatikana kila mwaka kinavyoliwa na wajanja na wengine kuachiwa mifupa.

  Wabunge wa CCM na wengine wanaona jinsi baadhi ya mawaziri wa kutoka chama chao wanavyojiangalia wenyewe kwa kujikatia zaidi kasungura hako kadogo na hata minofu mingine kuikimbizia kwenye majimbo yao badala ya kuangalia majimbo mengine pia. Hakika, Wabunge wa CCM sasa wanatoa kilio cha kuomba msaada na kilichochanganyika na hasira na hofu ya kupoteza mamlaka ya kuongoza dola ifikapo mwaka 2015. Ndio, kuna wanaokiona chama chao kikielekea kwenye kuzama 2015. Kelele wanazopiga bungeni zimegeuka kama kelele za nyikani, hazisikiki. Wameanza sasa kuwa na ujasiri wa kuzomeana wazi wazi kwenye vikao vyao badala ya kusubiri kuzomewa na wananchi hadharani. Naam, CCM ya sasa inapata tabu hata kwenye kujua namna ya kuitumia misamiati mipya ya kisiasa, maana, kuna wanaojivua gamba, wanaovuliwa magamba na sasa kuna ' wanaojinyambua' magamba wakiwa ndani ya chama- 'Political evolution' ya namna fulani.

  Na Mtego wa Zitto Kabwe kwa CCM?

  Jana Mbunge Zitto Kabwe ameitega CCM. Ni mtego wa hatari. Saini zile 70 zina maana hii;
  - Kama wabunge wa CCM hawatachangamkia kutia sahihi zao zikavuka hata mia na hamsini, basi, kuna ujumbe unaopelekwa kwa umma. Kuwa wabunge wa CCM ni maneno tu, hawana dhamira ya kweli ya kupambana na ufisadi. Wabunge wengi wa CCM hawataiepuka adhabu ya umma inaweza kuwa inawasubiri 2015.
  - Kwa wabunge wa CCM kutia sahihi zao na hata Pinda kupigiwa kura ya wabunge kukosa imani nae ina maana pia kuwa wabunge hawana imani na bwana mkubwa aliyemteua Pinda. Busara haiwataki wabunge wa CCM kufikia hapo. Hilo halina maslahi kwa taifa.

  Nini kitakachotokea?


  Kuna matatu;
  Mosi, Mawaziri wale watano wanaotuhumiwa kwa ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma wanaweza kuepusha aibu kwa Serikali kwa wao wenyewe kutangaza kujiuzulu. Ingawa hili ni gumu kufanyika katika nchi hii, lakini, wakati mwingine kuna lazima ya kufanyika- maana, hapo watakuwa wamemnusuru Waziri Mkuu na aliyemteua.

  Pili- Likishindikana la kwanza, basi, kabla ya Jumatatu, Waziri Mkuu Pinda awe ameshajiandaa kufanya maamuzi magumu. Kujiuzulu na kulinda heshima yake na ya aliyemteua. Au kutolewe ' Tamko la Serikali' litakalobadili upepo unaovuma sasa bungeni.

  Tatu: La kwanza na la pili yaweza yasifanyike, na badala yake. Rais anaweza kuyaona yanayotokea sasa bungeni kama fursa ya kufanya mabadiliko makubwa Serikalini mara akitua Dar kutoka ziara ya Brazil.

  Naam, yumkini pale Diamond Jubilee, kabla ya Jumatatu, kuna watakaopewa kazi ya kusafisha ukumbi na kupanga viti tayari kwa Mkuu wa Nchi kusema jambo kubwa kwa taifa kupitia kwa ' Wazee wa Darisalama'.

  Na tusubiri tuone.

  Maggid Mjengwa,
  0788 111 765
   
 2. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana nawe kabisa
   
 3. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2012
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Hii isijekuwa ile 1987 iliyomleta jakaya ktk medani kuu za siasa.....
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Umechambua vizuri sana ngoja tuone hilo tego kwa wabunge wa sisiemu.
   
 5. mkomatembo

  mkomatembo JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2012
  Joined: Dec 17, 2011
  Messages: 1,466
  Likes Received: 503
  Trophy Points: 280
  tEH TEHTEH hayo yote matatu hayatafanika !na watu watakaa kimya, angalau hata wazanzibari wanathubutu !
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Mi nadhani CCM wafanye hivi, wakatae kutoa sahihi 70, Zitto apate hizo sahihi kutoka kwa wabunge wa CUF na NCCR- Mageuzi na CDM; halafu hoja iletwe bungeni kura ishindwe kumtoa Pinda.

  Sisi, tutarudi kuwashitaki kwa wananchi na ushahidi utakuwa umeongezeka kwayo haya yatendekayo; ndipo wabunge wa CCM wasubiri hasira kuu ya wadanganyika!!! Tuwachape toka 2014 hadi 2015!! Nhci irudishwe kwa wananchi!

  Asante maggid, japo 2010 ulikula hela zao kuwauza kwa umma!
   
 7. D

  Davie Member

  #7
  Apr 20, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Uchambuzi mzuri Majjid....
   
 8. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #8
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Analysis nzuri,bahati mbaya ccm hawajui kuchagua lililo jema.
  Watawapa CHADEMA sababu nyingine ya kuzunguka,Dr.Slaa ana wasubiri
  kwa hamu wakosee,Lema yupo fit vitani,....na wabunge wa chadema
  wana tamani mpango wa zitto ushindwe,kwani itakua ni turufu kubwa
  kwa kuwaaibisha wabunge wote wa ccm.

  Wananchi nao hawako mbali,wanataka kuangalia kelele za wabunge
  wa ccm ni zile zile zilizokuwa za kina kilango,6,mwakyembe
  au kuna jipya?

  Tusubiri,yetu macho na maskio.
   
 9. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #9
  Apr 20, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa CUF na CDM wote wanasaini hivi sasa ifikapo saa tano tutakuwa na sahihi zote zinazotakiwa. CCM wamesaini 10

  Zittokabwe 2 hours ago.

  Hii nimepata on twitter, hope its genuine.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Apr 20, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kwa ninavyoielewa Tz hilo la wazee wa Daislam ndo litafanyika
   
 11. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #11
  Apr 20, 2012
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ndugu Maggid,

  Uchambuzi mzuri, ila hapo kwenye red naomba ufafanue zaidi,

  Yepi kwa mtazamo wako ndio na sio maslahi kwa Taifa ?

  Respect !
   
 12. J

  John W. Mlacha Verified User

  #12
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  kulitokea nini?
   
 13. Mapi

  Mapi JF-Expert Member

  #13
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 6,871
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  kaka umefanya kaz nzur. Tusubir tuone ccm watachagua fungu gani.
   
 14. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #14
  Apr 20, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kazi kubwa ya Lukuvi akishirikiana na Wassira ni kuwatisha wenzie........!
   
 15. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #15
  Apr 20, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  naam kazi ipo wacha tuone mi nasuburi tu hizo sahihi 70..
   
 16. M

  Mbuyi Member

  #16
  Apr 20, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 13
  Mzee wa kiminyio atanyuti nywii! 70 zitapatikana, motion italetwa,magamba(washapigwa mkwala) watanyuti, PM(ambaye siye lengo) atapeta, baadaye mtapigwa changa kwa reshuffle ya Mkulo,Mkuchika,Mponda na Celina, mtashangilia ushindi wakati wenyewe wanaendelea kujipanga na kuadhibu waliowaunga mkono! Imekaaje hii?
   
 17. k

  kibunda JF-Expert Member

  #17
  Apr 20, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 403
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kenge hasikii mpaka atoke damu puani!
   
 18. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #18
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
 19. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Udp kagoma ku-sign dah....
   
 20. Hercule Poirot

  Hercule Poirot JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 1,195
  Likes Received: 463
  Trophy Points: 180
  Hivi hizi ripoti za CAG ndio mara ya kwanza kusomwa bungeni? Vipi kuhusu miaka mingine iliyopita 2005-2011 au ni mwaka huu tu ndio ubadhirifu umevuka mpaka? Wabunge wanakosa imani dhidi ya serikali yao kwa haya tu?


  Aliloanzisha Zitto Kabwe ndio aina ya siasa tunazozitaka kuonyesha uchungu/maslahi ya wananchi kwa vitendo.....kimtazamo PM Pinda amekuwa mwanadiplomasia zaidi ktk nafasi yake kuluiko kuwa mtendaji/mkali ktk masuala ya kiserekali, kauli zake nyingi zimekuwa za kubembeleza zaidi kwa kweli hata mimi sina imani naye....pamoja na heshima kubwa juu yake
   
Loading...