Zitto Kabwe na nchi ya kufikirika

BAKOI

JF-Expert Member
Jan 31, 2016
1,211
2,328
Jamhuri moja ya KUFIKIRIKA ina wanajeshi wake nchi jirani, magharibi. Huko nchi jirani kuna nchi jirani nyengine inasaidia waasi ambao Jamhuri ya KUFIKIRIKA imeenda kupambana nao kwa ombi la Umoja wa Mataifa. Amiri Jeshi Mkuu mpya wa KUFIKIRIKA ana mahusiano ya karibu sana na Amiri Jeshi Mkuu wa Nchi ambayo inasaidia waasi wanaopigana na Askari wa KUFIKIRIKA.

Ari ya Wapiganaji itakuwa chini sana na kitakachofuata ni urafiki wa wakubwa kutamalaki na maslahi ya nchi kuwekwa pembeni. Madhara yake hayaelezeki...
 
Maneno mazito hayo! Sasa hapa mhe Zitto atusaidie, wale askari walioenda huko nchi ya kufikirika wakipoteza maisha yao utakuwa ni ushujaa au uzembe? Maana mtapiganaje vita wakati mabosi wenu ni marafiki? Tena sio urafiki kama wa facebook, bali ule wa kufa na kuzikana?
 
Watumie nafasi hiyo ya urafiki wao kuumaliza mgogoro huo vinginevyo itakuwa kioja
 
Hii style ya uhandishi wa Zito nimeipenda. Ujumbe umeeleweka vizuri sana.
 
Back
Top Bottom