Zitto kabwe: Mradi wa NSSF wa kiwanda cha kuzalisha sukari Mkulanzi kilichogharimu Tsh bilioni 130 hakijazalisha hata tani moja mpaka sasa

Sana bila wa kusahau na ule mradi wa jimboni kwake wa kununua viwania kwa heka milioni 200.
Inabidi upelekwe mswada wa kulinda hela za wastaafu kwani watu wanajichotea tu.


Kwani wakati ule ilisemekana kuwa ekari 1 ilinunuliwa kwa shilingi 800 Mil ?

Kwani sababu ya kuzuiwa kuendelea na ule ujenzi itakuwa ni zipi kwa yale Mapagale ya maghorofa ya Kigamboni?!

Kazi ipo!
 
..kuna ghala kubwa limejengwa dakawa inaonekana wenyewe(wamiliki wa ghala) wana jambo walilishalifahamu kuhusu bidhaa tarajiwa toka kiwanda cha sukari ... "waka-invest storage facility" hapo karibu na barabara kuu kabisa.
Na kuna wakati Miwa ilikuwa inapelekwa turiani na malori sasa labda wanatest au imekuwaje
 
Mazingira ya uchumi yalikuwa yanaruhusu ila yalivurugwa na marehemu ndio maana miradi imejifia
Hapana! Marehemu anasingiziwa sana! Hii mifuko ilikuwa inajitafuna yenyewe chini ya yule aliyekuwa msimamizi wao. Kila mfuko ulijiingiza kwenye ujenzi ili kupiga hela. kumbuka sekta ya ujenzi ilivyojaa rushwa. Angalia majengo yote yaliyoko mijini kwa majina ya NSSF, PSPF, PPF towers, yooote hayana wapangaji tangu yalipojengwa. Hawa wapuuzi walitegemea pesa hiyo irudi kwa njia gani? Alipoingia Magufuli ndo akawapiga stop.
Ni majengo yaliyojengwa kwa Bilioni 10, unakuta 3 katika hizo ni kugawana tu!
 
Kwani wakati ule ilisemekana kuwa ekari 1 ilinunuliwa kwa shilingi 800 Mil ?

Kwani sababu ya kuzuiwa kuendelea na ule ujenzi itakuwa ni zipi kwa yale Mapagale ya maghorofa ya Kigamboni?!

Kazi ipo!
Ziko zilizonunuliwa kwenye jimbo la Zitto ila kwa sababu alikuwa mnufaika alikuwa anakaa kimya, kwa kifupi wakati wastaafu wanahangaika juu ya mafao yao kumbe wanasiasa wanajichotea
 
Tanzania hakuna teknolojia kuzalisha sukari tani 250,000 kwa kulima hekari 800 ambazo ni sawa na ekari 2,000, haiwezekani hilo unatakiwa uelewe hivyo
Lengo halikuwa kulima hekta 800. Lengo ilikuwa kulima zaidi ila kwa ufisadi wamelima hekta 800 tu. Nbona mgumu kuelewa?
 
Mradi wa ujenzi wa kiwanda hiki unakadiriwa kutumia sh bilioni 130 mpaka sasa na mtaji wake sh bilioni 250.

Uwezo wake wa kuzalisha sukari ni tani 250,000/= lakini hakijazalisha hata tani 1.

Shamba la miwa lina miwa ya hekta 800 imechomwa moto, mradi umekufa.
Serikali kwanini isiache kufanya hizi biashara maana hawaziwezi? Kama hela zikipotea au kutumiwa vibaya, nani atabeba hizo lawama? Illovo au Bakheresa wanaweza kufanya hizi biashara.
Serikali ingejikita kwenye kazi zake za msingi. Muda ni mwalimu mzuri. Huko nyuma viwanda vyote vilikufa. Tunaanza tena yale yale halafu tunategemea matokeo tofauti!!!
 
Back
Top Bottom