Zitto Kabwe Mnamkamata mtu kwa kosa lenye dhamana. Mahakama Kuu inaruhusu dhamana

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Anaandika Zitto Kabwe
Mnamkamata mtu kwa kosa lenye dhamana. Mahakama Kuu inaruhusu dhamana. Serikali inakataa rufaa kuzuia dhamana. Mtu anakaa jela miezi 4, tena mwakilishi wa watu. Siku ya hukumu kuhusu dhamana Serikali inaondoa shauri mbele ya jopo la majaji 3.

Lengo? Kumkomoa mtu. Siasa za ukomoaji zinajenga chuki kwenye jamii na chuki inazaa visasi.

Haitoshi majaji kukemea Ofisi ya DPP. Mfumo wetu lazima uweke uwezo wa waendesha mashtaka wa aina ya kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini kuwajibishwa. Wanasheria tazameni namna ya kuwajibisha ofisi ya DPP kwa uonevu wa makusudi dhidi ya wananchi
 
Mama Tanzania, tumekosea wapi watanzania ili tufanye marekebisho, maana kwa hali ilivyo hivi sipati picha hadi ifike 2020 tutakua ktk hali gani.
 
Binafsi chuki dhidi ya WanaCCM Imeshazaliwa na imekomaa sana.

Ndio mana kila atwaliwapo mwanaccm kwangu huwa ni sherehe.kama zilivyo sherehe nyingine.
 
Back
Top Bottom