Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG

Sheria imetamka wazi vipindi viwili renewable, unless otherwise iwepo sababu za kutokuendelea.
Kwa hiyo hamba option ya kumwo doa CAG kwa kipindi kimoja
kama hawezi kuondolewa baada ya kipindi kimoja walikuwa na maana gani ya kuweks renewable?
 
Sioni impact ya kesi hii kipindi hiki. Kama Mahakama baada ya kesi hii ingemrejesha Ptof. Assad kwenye nafasi yake ningeona umuhimu wa matokeo ya mashauri kama haya maana ni mengi.
Huioni faida Kwa sababu sheria zinakupita kushoto. Hii ni moja Kati ya hukumu zenye faida Sana nchini.
 
Nilikuwa sifahamu kwamba kuna Vita Dhidi ya Marehemu....

Hata hivyo, bado nafahamu Rais pekee ambae hana bahati mbaya ya kusemwa semwa nchi ni Mwinyi peke yake!

Mwalimu Nyerere kafanya mambo mengi sana nchi hii, lakini bado hadi kesho anasemangwa, na wala sijawahi kusikia msamiati wa "Vita Dhidi ya Marehemu"

Jakaya kila siku anasemwangwa lakini sijawahi kusikia msamiati wa "Vita Dhidi ya Mstaafu Jakaya"!

Kwamba, Rais wa sasa anaweza kuvunja katiba na hakuna kitakachofanyika... INAWEZEKANA KABISA!

Inawezekana kwa sababu SSH anatumia staili ya JK na sio ya JPM! Bila shaka unakumbuka CHADEMA ya enzi ya JK ilikuwa STRONG kweli kweli... huku Mbowe, kule Slaa, pale kuna Mnyika, Lema nae yupo kibao... bila kumsahau Mdee, na wengine kadhaa!

Unakuta JK anafanya jambo linalopelekea full mapovu toka kwa akina Mnyika! Watafoka sana! Wataongea kadri wapendavyo, baada ya muda wanaitwa Ikulu "wakajadili" kuhusu suala husika!

CHADEMA na Gwanda zao, haoooo Ikulu... Kwavile mgeni lazima akaribishwe kinywaji, usishangae ukakuta unawekewa juicy kwenye glasi na JK mwenyewe!!!

Hapo watacheka, wanafurahi, na mwisho wa yote JK anawaahidi kufanyia kazi malalamiko yao!

Akina Tundu Lissu na ujanja wao wote ule watatoka hapo huku wakiwa wamekenua magego yote 49 lakini inakuwa ndo imetoka hiyo!! Hakua cha kufanyia kazi wala nini...

So, hakuna cha chuki hapo... it's all about how you handle your opponents!!
Kusemwa kwa kiongozi ni kawaida ila mimi nazungumzia kuchukiwa, jinsi anavyosemwa Magufuli na yanayoendelea huwezi kufananisha na hao viongozi wengine. Huyo Nyerere kumsema tu ni kama dhambi nakumbuka Lissu alivyomsemaga Nyerere jinsi watu walivyomjia juu anamkosea adabu Baba wa taifa, huyo Mkapa na Kikwete walisemwa kawaida tu hawakuchukiwa labda ndio hivyo walikuwa wanauma na kupuliza tofauti na Magufuli.

Leo hii ccm wenyewe wanaweza kumsema Marehemu(Magufuli) ila hawana ujasiri wa kumsema Mstaafu Kikwete, ndio maana nikasema huu uamuzi wa mahakama ni unafki tu ni katika muendelezo wa vita na marehemu.

Mtu kama Zitto hukuti anamkosoa rais Samia sasa ila ana muda wa kukosoa Marehemu hadi kwa hasira anafikia kutamka kuwaambia wenye kumpenda Magufuli wakazikwe naye, hiyo sio hali ya kawaida. Kwahiyo kilichotokea hakina maana yeyote kwa nchi ambayo tunajua isingeweza kutoa uamuzi huo kwa rais aliye madarakani na ndio maana nasema ni vita tu dhidi ya marehemu.
 
Sasa Kwanini Mahakama inatoa Majibu Leo?

Kwanini Haikuingilia kati wakati Ikiwa Inavunjwa kwa Wakati ule na Kuja Kujisemesha Leo?

Tanzania hakuna wakusimama na wananchi bila wanachi wenyewe kuamua 2025.
 
Asad alishindwa kusoma alama za nyakati kwa kubishana na muhimili uliojichimbia.Hakuna Rais Duniani anayetaka maovu ya serikali yake yajulikane.Asad kiprotokali ilipaswa ajiuzulu kulinda heshima yake lakini siyo kutaka Rais awe submissive kwake!
Magufuli was wrong legally but politically correct!
Rais alitakiw akushughulikia waloiba na sio Ashughulikiwe aliyeonesha wizi wakati ndio kazi yake ya kisheria.

Kifupi Jpm alikuwa fisadi
 
Haki iliyocheleweshwa Ni sawa TU na haki tuliyonyimwa.Uamuzi huu hauna msaada wowote kwa taifa kwa Sasa.Yaani mahakama inasubiri mpaka Magufuli afe ndo ijitutumue ! Ni sawa na uwe na ulinzi wa mbwa nyumbani,wezi waingie ndani ya nyumba,mbwa anaufyata mkia muda wote,Wezi wanaiba na kukomba kila Kitu na kuondoka,Halafu baada ya masaa let's say 10,NdoHuyo mbwa anaanza kuwabwekea.Shem on you !
 
Ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter

Nimefarijika kuwa leo tarehe 05/12/2022 Mahakama Kuu katika shauri la Zitto Zuberi Kabwe vs. Mwanasheria Mkuu na wenzie na 8/2020 mbele ya jopo la majaji 3 Masoud, Masabo na Kakolaki imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa J. Assad kama CAG.

View attachment 2436886
Tuna safari ndefu sana kwenye kulinda na kuheshimu Katiba ya Nchi.
 
Hizo ni athari za utawala wa kidhalimu wa Magufuli. Kila rais wa CCM hatakubali mikutano tena, maana wanajua CCM haiko madarakani kwa ridhaa ya umma.
Kwahiyo katiba ifanyiwe marekebisho isomeke Hivyo !!
 
Obama alisema Africa doesn’t need strong people! It needs strong institutions ! Sijui alikuwa ana maana gani !!!
Mahakama Imara
Bunge Huru
Polisi Huru
Tume huru ya Uchaguzi
Wizara zilizoundwa kwa mujibu wa Katiba
Taasisi huru za Ujasusi
Haki
 
Back
Top Bottom