Zitto Kabwe: Mahakama imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa Assad kama CAG

Magufuli alikuwa ni mvunja katiba mkubwa. Ila hizo mahakama kama angekuwa hai bado zingetoa hukumu ya kumfurahisha. Bila katiba mpya tena kwa njia ya machafuko, tusitegemee hatua zozote kuchukuliwa kwa hawa walevi wa madaraka.
Cc: UHURU JR
Jua kuwa Kila mtu na wakwake
 
Lazima kuna siku, (kama ilivyokuwa kwa dikteta Stallin ambaye alipambwa na kusifiwa sana na wapambe wake, hata kuyafanya mazishi yake kuvunja rekodi ya kuhudhuriwa na watu wengi zaidi Duniani kuliko mtu yeyote, na kusababisha wahudhuruaji wapatao 1,000 kufa), marehemu Magufuli lazima atatangazwa kuwa alikuwa kiongozi mwovu, na yote mabaya aliyoyatenda yatawekwa wazi.

Kwa Stallin, ilichukua miaka 13 tangu kufa kwake, ndipo alitangazwa kuwa alikuwa mtawala dhalimu, aliyegandamiza haki za raia ikiwa ni pamoja na kuwaua.

Watawala tendeni haki.
 
MAMHAKAMA Kuu Tanzania leo tarehe 5 Disemba, 2022 imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomwondoa Prof. Mussa Assad kama Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
FB_IMG_1670258039086.jpg
 
Ndugu kila kitu sio udini, tukiwa hivyo mbona tujiharibia utu wetu. Jee tunaweza sema Marehemu Magufuli alimuondoa Assad kwa sababu ya dini yake?...
Nadhani hawakutofautiana katika maono, walitofautiana katika tabia.

Mmoja alikuwa mwizi lakini akiwahadaa watu kuwa yeye ni mzalendo sana na mfia nchi, mwingine alikuwa muadilifu wa kauli na vitendo.
 
Magufuli alikuwa ni mvunja katiba mkubwa. Ila hizo mahakama kama angekuwa hai bado zingetoa hukumu ya kumfurahisha....
Kwa hizo Akili za kwenda kuambiwa na "I do you"

Au kwa Vision ipi hasa ambayo wapinzani wa nchi hii waliyonayo?

Kwenda kukaa na wazungu halafu wawafundishe jinsi ya kuleta mifarakano kwenye nchi zenu kwa faida zao?

Kazi kubwa ya kituonyesha mfano kwa upinzani wa kitanzania ni kununulika kwa Shekeli tu.

Kuanzia Mr Chairman mpaka kina Zitto!

Kuanzia yule aliyemuuzia chama Lowassa mpaka yule aliyemuuzia Chama Membe!

Hadi hawa Wa- bonge wanaobongewa na kulainika asubuhi.

Kifo cha CCM au Anguko la CCM litatokana na wana CCM wenyewe!
 
Ameandika Zitto katika ukurasa wake wa Twitter

Nimefarijika kuwa leo tarehe 05/12/2022 Mahakama Kuu katika shauri la Zitto Zuberi Kabwe vs. Mwanasheria Mkuu na wenzie na 8/2020 mbele ya jopo la majaji 3 Masoud, Masabo na Kakolaki imetoa uamuzi kuwa Rais John Magufuli alivunja Katiba alipomuondoa Prof. Mussa J. Assad kama CAG.

View attachment 2436886
Huyu mchawi mkimbizi wa kigoma bado yuko na marehemu tu
 
Mahakama Kuu, Masjala Kuu imebainisha kwamba uamuzi wa kuondolewa katika utumishi wa umma kwa aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad ulikiuka Katiba.

Uamuzi huo umetolewa na jopo la majaji watatu, Dk Benhajj Masoud (kiongozi wa jopo), Juliana Masabo na Edwini Kakolaki, kufuatia kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe.

Profesa Assad aliteuliwa kushika wadhifa huo na aliyekuwa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, Novemba 5, 2014 na alihudumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitano hadi Novemba 4, 2019 baada ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli alipomteua Charles Kichere kushika wadhifa huo.

Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na Serikali mwaka 2019 ilieleza kuwa Profesa Assad kipindi chake kilimalizika Novemba 4, 2019.

Zitto aliamua kufungua kesi ya Kikatiba mahakamani hapo akipinga kuondolewa kwa Profesa Assad katika wadhifa huo na uteuzi wa Kichere kuwa CAG mpya, akidai kuwa Profesa Assad alikuwa hajatimiza muda wake wa utumishi kikatiba yaani umri wa kustaafu.
Zitto aliamua kufungua kesi ya Kikatiba mahakamani hapo akipinga kuondolewa kwa Profesa Assad katika wadhifa huo na uteuzi wa Kichere kuwa CAG mpya, akidai kuwa Profesa Assad alikuwa hajatimiza muwa wake wa utumishi kikatiba yaani umri wa kustaafu.

Katika kesi hiyo ya kikatiba namba 8 ya mwaka 2020, Zitto akiwakilishwa na mawakili Dk Rugemeleza Nshala na Nyaronyo Kichere, alikuwa akipinga kuondolewa kwa Profesa Assad na kuteuliwa kwa Kichere kuwa ni kinyume cha Katiba ya nchi.

Alidai kuwa kifungu cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi wa Umma namba 11 ya mwaka 2008 kinachoweka mihula miwili ya miaka mitano ya utumishi wa CAG, ambacho ndicho kilichotumika kuondolewa kwa Profesa Assad, kinakinzana na masharti ya Katiba.

Zitto alidai kuwa Ibara ya 144(1) ya Katiba ambayo inaeleza kuwa CAG atatumikia wadhifa huo mpaka umri wake wa kustaafu, yaani miaka 60 kikatiba au miaka 65 kisheria, sawa na kifungu 62(a) cha sheria hiyo kinavyoeleza.

Hivyo, alikuwa akiiomba mahakama hiyo itamke kuwa kifungu hicho cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi, ni batili kwa kuwa kinakinzana na Katiba na kwamba kuondolewa kwa Profesa Assad kabla ya kutimiza umri wa kustaafu ni batili na pia uteuzi wa Kichere kuwa CAG mpya ni batili.

Mahakama hiyo katika hukumu yake iliyosomwa jana ilikubaliana na hoja za Zitto kuwa kifungu hicho cha 6(1) cha Sheria ya Ukaguzi kuweka mihula ya miaka mitano mitano ya utumishi wa CAG ni batili kwa kuwa kinakinzana na Katiba Ibara hiyo ya 44 ambacho kinaendana na Katiba.

Mahakama hiyo imesema kuwa wakati kifungu hicho kinaweka mihula ya utumishi wa CAG, Katiba inazungumzia umri wa kustaafu na si mihula.

Hivyo, Mahakama imesema kuondolewa kwa Profesa Assad kabla ya kufikisha umri wa kustaafu kulikuwa ni batili.

Hata hivyo, Mahakama hiyo imekataa maombi ya Zitto kutamka kuwa uteuzi wa Kichere ni batili, badala yake imesema kuwa uteuzi wake ni halali kwa kuwa aliteuliwa kwa mujibu wa Katiba.

Akizungumza na Mwananchi kuhusu hukumu hiyo, Wakili Nshala amesema imeacha utata baada ya kukubali kuwa kuifungu hicho cha sheria kinachoweka mihula badala ya umri ni batili na kwamba Profesa Assad aliondolewa kinyume cha Katiba lakini ikasema kuwa uteuzi wa Kichere ni halali.

Zitto katika taarifa yake kwa umma akizungumzia kipengele hicho amesema kuwa amewaelekeza mawakili wake kukata rufaa Mahakama ya Rufani kwa lengo la kubatilisha uteuzi wa Kichere.

Wakili Nshala alisema kuwa wako tayari kwa maelekezo ya mteja wao, Zitto kukata rufaa Mahakama ya Rufani katika kipengele hicho ili kupata ufafanuzi zaidi.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dk Boniface Luhende alipotafutwa kwa njia ya simu kuzungumzia uamuzi huo, hakuweza kupatikana kwa kuwa simu yake haikuwa hewani.
 
Zitto aliumia sana kimapato baada ya Assad kutumbuliwa na kisha yeye kuukosa ubunge na Pia ujumbe wa kamati za "PAC" na "LAC".

Huko ndio alikuwa akipatia deal za wakurugenzi wenye madudu kwenye mashirika yao.

Kwa kupewa "Data" zote na Mussa Assad "CAG" wa wakati huo.

Na Zitto alikiwa akizitumia kuwatishia na kuwaomba milungula kwa mgongo wa hizo kamati za Bunge za Mahesabu ya Serikali.

Jambo lililompatia ukwasi wa ghafla enzi hizo,hadi akaweza kununua gari la kifahari aina ya Hammer.....

Akiwa mbunge wa kwanza miaka hiyo 2012.
Screenshot_20221205-195201_Twitter.jpg
 
Nionyeshe kiongozi wa nchi hii asiyekaa mezani na wazungu. Na ukitaka kufurahi zaidi weka mikataba tuone waliyoingia wapinzani tufananishe na mikataba waliyoingia viongozi wa CCM tupime ipi ni hatari kwa nchi hii.

Usiseme anguko la CCM litatokana na wañaccm, sema siku vyombo vya dola vitaacha kuibeba CCM, siku hiyo hiyo CCM itaingia kaburini.
 
Jamaa alikuwa na pupa sana katika maamuzi yake mengi, na tena yasiyozingatia matakwa ya katiba, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali. Hii inathibitisha ukweli ya kwamba alikuwa muimla.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umeelewa lakini? Kilichopo ni mgongano kati ya Sheria na Katiba!

Katiba inatamka kuwa mkaguzi mkuu atatumikia mpaka afikishe miaka 60 ndipo astaafu lakini sheria ya ukaguzi inatoa mwanya kuwa mkaguzi mkuu atakuwa na vipindi viwili vya utumishi katika kiti chake, yaani miaka 5 ya kwanza then ikimpendeza Rais atamteua tena, kwaiyo Magufuli aliutumia mwanya wa sheria ambayo inafafanunua Katiba, wakati uo Zitto alienda Mahamani kupinga kifungu hicho cha Sheria na kwa mujibu wa Sheria zetu, sheria yoyote inayokinzana na Katiba basi kifungu hicho ni batili.

Sheria za namna hii tunazonyingi sana katika Taifa letu! Ata lile la Ndugai kulazimishwa kujiuzulu ni sawa tu na ili la Assad sapo wanaoamua wanaangalia upepo kuwa sasahivi Magufuli hayupo basi hakuna cha kuhofia, ila now Samia yupo ndiye alitefanya Ndugai atoke basi ili haliwezi kukubaliwa kule!

Unaweza sema bora Magufuli alitumia mwanya wa kisheria kukinzana na Katiba ila Samia hakutumia lolote kwa Ndugai zaidi ya power aliyonayo.
 
Hiyo ni moja je uteuzi wa Bashiru Ally Kuwa CS ulikuwa halali?

Pia It's high time vyeo hivi vikawa vya kupatikana kwa merit watu wafanyiwe scrutiny kwenye open platform ili isionekane ni vya kupewa tu ndio maana mtu akiamua anateua au kutengua bila kuulizwa na mtu.

Kwa jinsi hii ni kichaa tu ndio hatoona umuhimu wa kuwepo na kitabu kipya hiki cha sasa hakina meno kwa viongozi ambao wanatakiwa watumikie wananchi ila wao ndio hugeuza wananchi watumwa wao.
 
Back
Top Bottom