Zitto Kabwe kwenda Uswisi kukutana na watafiti wake Kuhusu Mabilioni ya USWISI

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Novemba 26, 2012 | Mwananchi

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) amesema yupo tayari kuipa Serikali wachunguzi wa kimataifa iwatumie kuchunguza Watanzania walioficha fedha haramu kwenye Benki za Uswisi.

Kauli hiyo ya Zitto imekuja takriban wiki moja tangu alipoieleza Serikali kwamba kama imeshindwa kuwachunguza walioficha fedha Uswisi, iwaachie wenye uwezo wa kufanya suala hilo yenyewe isubiri majibu kwa manufaa ya nchi.

Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, alisema kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika kuwataka Watanzania kupeleka majina ya vigogo walioficha mabilioni kwenye benki hizo ili wachunguzwe, inaingilia uhuru wa Bunge na kwamba alitakiwa kuzungumza jambo hilo bungeni.

Pia, alisema lingekuwa jambo la busara kama Spika wa Bunge, angeweka wazi ripoti ya kamati ndogo iliyoundwa kuchunguza tuhuma za wabunge kujihusisha na vitendo vya rushwa, ili umma uweze kufahamu kwa undani juu ya uchunguzi huo.

Akizungumza na Mwananchi Dar es Salaam jana, Zitto alisema kutaja majina ya Watanzania hao siyo suluhisho, kinachotakiwa ni nchi kuwa na utaratibu mzuri wa kubaini fedha zinazofichwa nje na kusisitiza kuwa siyo lazima iwe Uswisi.

Alisema Desemba 10, mwaka huu anatarajia kwenda Uswisi kukutana na watafiti wake, huku mmoja akiwa anatokea Uingereza na kwamba, atawapatia taarifa ya mahali taifa lilipofikia kuhusiana na fedha hizo.

"Ni muhimu kuacha uchunguzi ukafanyika ili kuwabaini waliohusika kuliko kutaja majina ya watu. Ninaweza kutaja majina watu wakasema natafuta umaarufu," alisema Zitto na kuongeza:

"Nikionana na watafiti hawa nitawaomba kama watakuwa tayari kutoa ushirikiano na timu ya uchunguzi inayofuatilia suala hilo, moja ya jambo ambalo nitawaomba ni kutoa ushirikiano wao kwa taifa kama watakuwa tayari ili watusaidie kubaini majina hayo ambayo siyo yapo Uswisi peke yake bali na nchi nyingine."

Alisema Watanzania waache kupenda mambo rahisi na kwamba, uchunguzi lazima ufanyike kuwabaini walioficha mabilioni hayo ili fedha hizo zirejeshwe nchini.

Alisema Serikali ya Uswisi haiwezi kuisaidia Tanzania kufanya uchunguzi wa fedha hizo.
 
Kauli hii ya Zitto ni nzuri sana lakini kwa nini isishughulikiwe Kichama na yeye akawa kiongozi???
Nakumbuka ushindi uliojitokeza kwenye ile list of Shame kulitokana na Viongozi wa Chadema Kuungana na kutoa msimamo pale Mwembe yanga.

Sasa hili suala la Uswiss Zitto analichanganya na yeye kuingia Ikulu huku akivuruga CDM!!!
Hapa ina onyesha kuwa kuna watu nyuma ya Zitto ili kupotosha umma!!!

Zitto ni mtu wa karibu na Kikwete . Taarifa zinaonyesha Suala la Uswiss limekuja wakati Lowassa kashafanikiwa mpango wa kutenganisha kofia Mbili Dodoma ambapo Kikwete angetoka!!!!

Hivi sasa kuna uadui Mkubwa kati ya Lowassa na Kikwete.
Lowassa anatajwa katika orodha ya walioficha fedha uswiss na hakuna shaka!!!

Hii inatufundisha kuwa Zitto anafanya kazi ya Kikwete kumushambulia Lowassa huku akiwapumbaza Watanzania!!!
Angalia Zitto anavyopewa Nguvu kutumia TBC na vyombo vya serikali wakati TBC hiyo hiyo haitaki kurusha matukio ya mikutano ya viongozi wengine wa CDM
 
Alifanya jambo la maana kuwasilisha hoja ya kutaka kurejeshwa kwa mihela ya Uswis irejeshwe.Hoja yake,pamoja na kupigwa vijembe na wana-CCM wenzangu kule Bungeni.Kama sikosei,Bunge likaridhia kuipa Serikali ili ifanye kazi ya kuandaa ripoti juu ya nini kinafanywa na Serikali kurejesha mihela hiyo ya Mafisadi Nyangumi wa Tanzania iliyofichwa Uswisi.

Baada ya kuahirishwa Bunge, Mkuchika akaropoka juu ya maazimio ya Bunge. Akamtaka Zitto ataje majina ya walioficha mihela Uswisi ili kuisadia Serikali kutekeleza maazimio ya Bunge. Mkuchika alimtega Zitto.Zitto bila kujua akanasa.Anahangaika na mtego huo hadi sasa. Anaweweseka. Anaharibu hoja yake. Kwanini asiiache Serikali iendelee kupiga sarakasi zake zinazoimarisha hoja yake? Kwani ana haraka gani wakati Bunge linarejea Februari. Nadhani anaharibu hoja yake
 
Sina uhakika kama Zito yupo mwenyewe ktk hili kwani hili ni hoja nzito sana tena kuliko sana Zito anapaswa jambo hili liwe ktk mikono ya Chama ili hata kama Bad guy get him bado inaweza kuendelezwa na chama ktk kuifuatilia mwisho wake, Nadhani ni risk sana kama anaifuatilia yeye mwenyewe, Ni wakati wa KUIFUNJA TAKUKURU KWANI WAO WALIPASWA KUJUA HAYA MAPEMA KABLA HATA YA ZITO, NN MAJUKUMU YA TAKUKURU SASA?
 
KING COBRA CHADEMA mtasubiri sana zitto kurejea katika kiwango cha zamani na kukubaliana na chama chake.Juzi kasema yeye na JK ni marafiki binafsi, so Lowassa anatafutwa na JK kwa maana nyingine zitto yuko buzzy na tender nono aliyopatiwa na JK dhidi ya Lowassa kwa kushirikiana na Membe.CDM be sure zitto is no longer with you is at different planet right now.mtasubiri sana
 
Last edited by a moderator:
"Zito yupo mwenyewe ktk hili kwani hili..."

Economic Hit Men ktk kutekeleza mipango yao mbalimbali yenye lengo la kunyonya rasilimali za mataifa machanga ikiwemo Tanzania huwa wanamipango endelevu ya kuwaweka madarakani watu wao (Makuwadi) kuanzia ngazi ya Urais, Mawaziri, na hata kwenye vyombo muhimu vya kimaamuzi...in return hawa EHM huwa wana-guarantee maisha mazuri kwa hawa makuwadi na familia zao kwa kuwapa makazi na fedha nyingi kwenye MABENK yao kama ya USWIS...

Swali lamsingi hapa la kujiuliza ni nani mwenye ubavu wa kupambana na CIA? nani mwenye uwezo wa kuzuia mipango ya nchi tajiri tena zenye ushirikiano wa kila namna? Jibu ni hakuna kwa sasa...

Kilichobaki ni sisi kupiga kelele mikataba yote iwekwe hadharani, sijui ni nani wa kuiweka hadharani kwani karibu wote walioko madarakani ni "MAKUWADI"...SAD!!!
 
Mzito kabwela kitakacho kuangusha ni sifa na ubinafsi we hoja kama hiyo ni hoja ya cdm usijifanye una uchungu na hii nchi alafu we ni danganya toto mafisadi wote ni rafiki zako usitutanie walahi ukisimamishwa 2015 kura yangu we mi sikupi
 
Eti kutaja majina sio suluhu = hypocrisy + Puppet

Cha msingi kuhusu ZZK ni kukumbuka ahadi anazozitoa

Alisema angewataja kwenye bunge lililopita. Na hii ya safari utakuja kusikia amebadili stori.
 
Kauli hii ya Zitto ni nzuri sana lakini kwa nini isishughulikiwe Kichama na yeye akawa kiongozi???
Nakumbuka ushindi uliojitokeza kwenye ile list of Shame kulitokana na Viongozi wa Chadema Kuungana na kutoa msimamo pale Mwembe yanga.

Sasa hili suala la Uswiss Zitto analichanganya na yeye kuingia Ikulu huku akivuruga CDM!!!
Hapa ina onyesha kuwa kuna watu nyuma ya Zitto ili kupotosha umma!!!

Zitto ni mtu wa karibu na Kikwete . Taarifa zinaonyesha Suala la Uswiss limekuja wakati Lowassa kashafanikiwa mpango wa kutenganisha kofia Mbili Dodoma ambapo Kikwete angetoka!!!!

Hivi sasa kuna uadui Mkubwa kati ya Lowassa na Kikwete.
Lowassa anatajwa katika orodha ya walioficha fedha uswiss na hakuna shaka!!!

Hii inatufundisha kuwa Zitto anafanya kazi ya Kikwete kumushambulia Lowassa huku akiwapumbaza Watanzania!!!
Angalia Zitto anavyopewa Nguvu kutumia TBC na vyombo vya serikali wakati TBC hiyo hiyo haitaki kurusha matukio ya mikutano ya viongozi wengine wa CDM

The true picture of ZZK is in RED! He has joined the Anti EL group for the benefit of his hero JK!! If he has joined CCM B is he really fit in the opposition. Who is funding the process and travels? By ZZK being used by JK is it healthy for the opposition? He learnt the hard way, the way the list of shame he shared with his party leaders was used in also hammering his dark boss JK? What a coward and weak prezidah! He can only work from the backs!! It is good work but the masters he is serving spoils the whole broth! ZZK bring the evidence and we will see its use!!
 
Cha msingi kuhusu ZZK ni kukumbuka ahadi anazozitoa

Alisema angewataja kwenye bunge lililopita. Na hii ya safari utakuja kusikia amebadili stori.
kwa kweli mi naona kuna kamchezo kanafanyika.....nilikuwa naona anakwenda vizuri lakini sasa Zito anatuyeyusha....ni danadana na porojo...mwanzo alisema atataja majina,mara uchunguzi kwanza,sasa analeta stori kwamba kuwataja haisaidii hivyo anakwenda Uswisi kupiga stori na 'watafiti' ,kHA! akirudi stori itabadilika kabisa..ndio maana nashindwa kuwafuatiliaga hawa wanaSIHASA...ni headache na unaweza ukadata kabisa!!!
 
Namuombea mungu amsaidie katika kuwapignia watanzania,zawadi yake pekee ni kumpa urais 2015 ili awe na mamlaka zaidi badla ya kuhangaika hivi mara kwa mara.wabhejasana zitto.
 
"katika hili zitto ni mnafiki" usiniulize kwanini changanya bongo yako
 
Hivi Zitto pamoja na ubunge wake wa zaidi ya miaka saba sasa haoni kama anajichosha tu na suala hili? Hivi kwa mfano, akishajua ni Lowasa ana mihela hiyo huko Uswisi atafanya nini? Hakujifunza lolote kutokana na vile "vijisenti" vya Chenge kule Jersey?

Zitto arudi Bungeni waiangalie upya ile sheria iliyoanzisha TAKUKURU ya sasa waipe nguvu ya kukabiliana na uhamishaji/utoroshaji wa fedha zetu kwa njia hizi haramu. Vinginevyo yeye aende tu kutalii Ulaya
 
Anasema eti serikali ya Uswiss haiwezi kuisadia Tanzania kupata hizo pesa! This is a big lie!

Kama tutaonesha nia basi Uswiss automatically will be bound by INTERNATIONAL MUTUAL LEGAL ASSISTANCE LAW

Ila kama CCM ingekuwa na nia ya kujisafisha basi ingeanzia kwenye hili la pesa za Uswiss. Umoja wa Mataifa(UN) kwa kupitia World Bank wana kitengo cha kufuatilia pesa zilizoibwa, kinaitwa STOLEN ASSET RECOVERY (StAR). Hao huwa wanalipa hata gharama za mpelelezi, judge etc
 
Zitto arudi Bungeni waiangalie upya ile sheria iliyoanzisha TAKUKURU ya sasa waipe nguvu ya kukabiliana na uhamishaji/utoroshaji wa fedha zetu kwa njia hizi haramu.
Bado una imani na TAKUKURU? Pimia mwenye kauli ya Dr. Hoseah kwa ubalozi wa Marekani,
"Unapodhuria mikutano ya vigogo wanataka utambue kwamba wao ndo wamekupa hicho kitengo. Na kama wakiona unatofautiana na matakwa yao, basi upo hatarini"
 
Anasema eti serikali ya Uswiss haiwezi kuisadia Tanzania kupata hizo pesa! This is a big lie!

Kama tutaonesha nia basi Uswiss automatically will be bound by INTERNATIONAL MUTUAL LEGAL ASSISTANCE LAW

Ila kama CCM ingekuwa na nia ya kujisafisha basi ingeanzia kwenye hili la pesa za Uswiss. Umoja wa Mataifa(UN) kwa kupitia World Bank wana kitengo cha kufuatilia pesa zilizoibwa, kinaitwa STOLEN ASSET RECOVERY (StAR). Hao huwa wanalipa hata gharama za mpelelezi, judge etc
Azipa,
Ushahidi kwamba walio na fedha Uswisi wameziiba mtautoa wapi? Alichokifanya AG mstaafu Chenge na Mkapa ni kuichakachua sheria ile ya PCB ibaki kama ilivyo sasa. Ushahidi unatafutwa na dola na sio kumsimamisha mtuhumiwa aeleze alikozitoa pesa hizo.
 
Back
Top Bottom