Zitto Kabwe kuwa waziri baada ya uchaguzi mkuu 2010

Status
Not open for further replies.

Nyauba

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
1,098
105
Kuna tetesi kuwa huenda Mh Zito Kabwe akapewa nafasi ya uwaziri katika baraza lijalo la mawaziri kutokana na kumvutia sana Muungwana (JK) katika utendaji na upeo makini wa masuala ya kitaifa na kimataifa..

Mwenye nyeti zaidi ya hili atujuzee hapa jamvini...JF kila taarifa natumai inapatikana.
 
kama inatokea akenda CCM , kisha kwa bahati akashinda Ubunge na Rais akaonelea ampe Uwaziri anaweza kumpa.

Ingawa mimi si shabiki wa Zitto, ila naamini ana uwezo kuongoza kama Waziri kuliko Masha, Ngeleja, Malima, Simba, Pinda na hata Kikwete mwenyewe ambae ni mkuu wa cabinet.
 
-Nadhani Zitto ana uwezo wa kuongoza wizara.Hata hivyo sijui kwa nini Muungwana asingempa uwaziri ,tufike mahala tuaache conservatism,Zitto kuwa opposition haimnyimi nafasi ya Uwaziri.JK amteua tu hata kama yuko ndani ya Chadema...

Nasema sio Zitto tu,Dr.Slaa angefaa sana nafasi ya uwaziri mkuu au TAMISEMI.

Pia Mnyika ana uwezo mkubwa kuliko mawaziri wetu wa sasa bila kumsahau Hamad Rashid wa CUF
 
Kuna tetesi kuwa huenda Mh Zito Kabwe akapewa nafasi ya uwaziri katika baraza lijalo la mawaziri kutokana na kumvutia sana Muungwana (JK) katika utendaji na upeo makini wa masuala ya kitaifa na kimataifa..

Mwenye nyeti zaidi ya hili atujuzee hapa jamvini...JF kila taarifa natumai inapatikana.

Navyojua mimi kazi ya waziri ni kumsaidia Rais na serikali iliyoko madarakani kwa ujumla kutekeleza ilani ya uchaguzi ya chama kilichoko madarakani- sasa Zito atakapoteuliwa kuwa Waziri je atakuwa anakeleleza ilani ya chama kipi ? CHADEMA au CCM ?
 
Navyojua mimi kazi ya waziri ni kumsaidia Rais na serikali iliyoko madarakani kwa ujumla kutimiza ilani ya uchaguzi ya chama husika- sasa zito atakuwa anakeleleza ilani ipi ? ya CHADEMA au CCM ?
Atakuwa anamsaidia Raisi zaidi kwani Ilani yao walishagundua haitekelezeki na ni kiini macho kurubuni kura tuu.
 
Hii itakuwa serikali ya mseto, umoja wa kitaifa, maridhiano au nini?

Katiba ya wamarekani kwenye hili ipo vipi? Maana siasa ya hivyo ndo tunaweza kuiga. That is a good move but can we handle it?
 
Kama kweli wakimpa huo uwaziri itakuwa ni kwa lengo la kumfunga mdomo.,kitu ambacho si kizuri sana kwani Zito ametokea kuwa mpambanaji na mkosoaji wakubwa wa serikali.
 
Tetesi tu kama tetesi nyingine....

JF tuache haya mambo watu wanatoka na mada za ubishani kijiweni halafu anaamua kuileta humu bila hata kuwa na source ya maana. Hiyo tetesi inatoka wapi?

Tusitumie mwanya wa tetesi kuweka mijadala ambayo ni ya kufikirika tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom