Zitto Kabwe kuwa kiongozi wa Upinzani Bungeni?

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Kuna habari kuwa Zitto Kabwe anagombea nafasi ya kuwa kiongozi wa Upinzani Bungeni.

Taarifa zaidi, watch this space!
 
Zitto ana harufu ya CCM, i don't trust him anymore esp baada ya hoja zake kuhusu mitambo ya Dowans! Pia ni mfagiliaji mzuri wa CCM siku hizi!
 
Sijui ni kwa nini sijaipenda hiyo, Zitto angekaa pembeni tu
 
Kama Mwenyekiti wake yuko Bungeni, je isingekuwa busara na hekima amuachie Mbowe awe kiongozi wa upinzani? Unless kama Mbowe hagombei nafasi hii, nahisi inaweza tena ikawagawa katika makundi.

Kuna vijana wawili walioondoka Chadema wameshinda Kigoma. Wangekuwa CHADEMA ushindi ungeongezeka.
 
Anaweza kufaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA lakini si Kiongozi wa Upinzani. Hana uwezo huo, itakuwa aibu kwake na kwa CHADEMA.
 
japokuwa Kuna wabunge wengi wa upinzani, lakini CCM wanaanza kutumia strategy za chinichini za kuzima nguvu ya Bunge, just imagine Bunge litakuwaje, maana kuna RA, EL spika awe Chenge na naibu spika say Kinana (Kama akigombea) na msemaji wa upinzani awe Zitto
 
Niliwai chart na mr zitto facebook kuhusu kugombea nafsi ya kiongozi wa kambi ya upinzani bunge alisema bado hajaamua na atatoa mwelekeo siyo sasa. Je katoa tamko hilo mkuuu ?
 
Siungi mkono busara ni kumwachia Mwenyekiti wa chama kuwa kiongozi wa upinzani angalia bunge la UK inapendeza kiongozi wa upinzani bungeni anakuwa kiongozi mkuu wa chama chake.
 
Sio kila mfumo unaweza kufaa kila mahali. Kiukweli hana hata sifa za kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA. Angalau ndani ya CHADEMA anaweza kuvumilika ila si nje ya CHADEMA.
 
Niliwai chart na mr zitto facebook kuhusu kugombea nafsi ya kiongozi wa kambi ya upinzani bunge alisema bado hajaamua na atatoa mwelekeo siyo sasa. Je katoa tamko hilo mkuuu ?
Mkuu,

Sijakurupuka! Watch this space nakupa 24hrs utaona kama hajatoa tamko hilo
 
Kama Mwenyekiti wake yuko Bungeni, je isingekuwa busara na hekima amuachie Mbowe awe kiongozi wa upinzani? Unless kama Mbowe hagombei nafasi hii, nahisi inaweza tena ikawagawa katika makundi.

Kuna vijana wawili walioondoka Chadema wameshinda Kigoma. Wangekuwa CHADEMA ushindi ungeongezeka.

Safari hii demokrasia ichukue mkondo, atakayeshindwa amuunge mkono mwenzake.

Binafsi ninaamini Zitto ana uwezo wa kuwaunganisha wabunge wa vyama vyote vya upinzani vilivyoko bungeni kuliko Mbowe, na ni muhimu sana kwa wabunge wote wa upinzani kuwa na sauti moja.
 
Sina tatizo Zito kuwa kiongozi wa upinzani bungeni, ila nadhani kuwa watu kama Lisu, kwa kuwa ni mwanasheria na mwenye uwezo na upeo mkubwa katika maswala ya jamii angefaa zaidi. Mwingine kwa sababu za ukomavu (maturity) wa kisiasa ni Mbowe.
 
Siungi mkono busara ni kumwachia Mwenyekiti wa chama kuwa kiongozi wa upinzani angalia bunge la UK inapendeza kiongozi wa upinzani bungeni anakuwa kiongozi mkuu wa chama chake.

Chadema ni lazima wawe careful kwani nimekwisha ona mbinu za ccm zikianza kutaka kuwagawa hawa wabunge katika makundi kupitia kuutafuta uongozi wa upinzani!! Zitto ana baggage nyingi za ccm toka enzi za Dowans haaminiki; kama sio Mbowe basi hata Halima Mdee ana uzoefu anaweza kuwa kiongozi wa upinzani na akamudu zaidi ya Zitto!!
 
Kama Mwenyekiti wake yuko Bungeni, je isingekuwa busara na hekima amuachie Mbowe awe kiongozi wa upinzani? Unless kama Mbowe hagombei nafasi hii, nahisi inaweza tena ikawagawa katika makundi.

Kuna vijana wawili walioondoka Chadema wameshinda Kigoma. Wangekuwa CHADEMA ushindi ungeongezeka.
Lakini ni vijana wasio na displine. Ni afadhali wakakaa mbali nasi kuliko kuwa nao kama mzigo ndani ya chama. Mi nadhani tutashirikiana nao vizuri wakiwa nje ya chama kuliko walivyokuwa ndani ya chama. Mnamkumbuka Kafulila na battle ya zitto na wenyekiti? Wacha akae na Mbatia huyo watawezana maana ni wale wale tu, undisciplined.
 
Chadema ni lazima wawe careful kwani nimekwisha ona mbinu za ccm zikianza kutaka kuwagawa hawa wabunge katika makundi kupitia kuutafuta uongozi wa upinzani!! Zitto ana baggage nyingi za ccm toka enzi za Dowans haaminiki; kama sio Mbowe basi hata Halima Mdee ana uzoefu anaweza kuwa kiongozi wa upinzani na akamudu zaidi ya Zitto!!
Hapa tunachanganya vitu. Si kwamba Zitto haaminiki, la hasha, Zitto anasema ukweli muda woote hata kama ukweli huo unawaudhi wenzake ndani ya CHAMA. Kwa ujumla Zitto anasimamia maslahi ya Watanzania zaidi kuliko maslahi ya kisiasa ndio maana kwake hata kugombea ubunge haikuwa kazi ngumu. Ipo mifano mingi tu juu ya utendaji wake na muono wake ila mfano mkubwa atakuwa ni Kafulila aliyeshinda ubunge huko Kigoma.
 
hawa chadema waangalie wasije wakaharibu mambo

Je, Chenge kugombea nafasi ya Spika ni sahihi? Maana ninaanza kupata mashaka kwamba nawe mgombea ubunge kupitia CCM mawazo yako yamekaa kiitikadi zaidi. Angalieni na ninyi, mkienda kwa mwendo huu hata huko vijijini moto wa mabadiliko unakuja, hamtaendelea kuwadanganya wananchi kwa sera za kiungo uongo kwa kutumia ujinga na umasikini wao kama mtaji.
 
Back
Top Bottom