M-mbabe
JF-Expert Member
- Oct 29, 2009
- 13,203
- 23,020
Muda mfupi uliopita nimewasilisha swali la maandishi Bungeni kuitaka Serikali iueleze umma Kuhusu kesi zote ambazo Jamhuri ya Muungano imefunguliwa kwenye mahakama za kimataifa za usuluhishi ya migogoro ya Biashara, uwekezaji na mikataba. Watanzania wanafichwa Mambo mengi muhimu
Nimechukua uamuzi huu baada ya kupitia nyaraka nyeti za kesi ya Acacia Mining dhidi ya Jamhuri ya Muungano ( LCIA Arbitration No. UN173686 no. 87 ) iliyopo London na kugundua kuwa Serikali yetu inaficha Taarifa Kwa umma wakati Watanzania Ndio watalipa matrilioni ya shilingi....
Kesi iliyoamuliwa juzi dhidi ya @tanescoyetu ilizungumzwa kwenye Taarifa ya CAG ya mwaka huu kwa Hesabu za 2016/17. Lakini pia kesi hii haikuwa yetu kwani Benki ya SCBHK haijawahi kuwa na mkataba na nchi yetu. Uzembe mkubwa umefanyika na hivyo kubambikwa kesi si yetu
Suala la kesi hizi za kibiashara lisipojadiliwa kwa kina wengine tutaachiwa nchi ya kulipa madeni ya kesi tu. Lazima tupewe Taarifa. Mf. Eco Energy Bagamoyo $500m, Symbion $600m, SCBHK $700m, Acacia $2bn! Sasa si kuuza nchi huku pengine kwa kujitakia tu? Bungeni mahala mwafaka.