Zitto Kabwe kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA endapo....

Zitto mambo yake ni kama vile anaendesha siasa za kibinafsi. Watu wanahangaika na M4C mara yeye yuko Marekani, mara yuko kusini mwa Africa. Bajeti iko busy bngeni yeye yuko Kigoma na Leka Dutigite huku M4C inakimbia mikoani. Bunge lililopita la bajeti, alikuwa active sana na wakna January kuikimbiza bajeti ya Ngeleja. This time kachangia kwa maandishi tu na kwa jinsi tunavyomfaham kwa ile hotuba ya Mnyika ikizingatiwa kuwa Mbowe hajaonekana bungeni, ilikuwa lazima achangie kwa maneno ila kawa kimya tu. Kahamia fb na twitter. Simfagilii Dr Slaa labda chama kikimpitisha ila Zitto ndo simuamini hata kidogo. Anaweza kuwa mzururaji zaidi ya JK akipewa nchi na nchi itauzwa zaidi ya ilivyo sasa
 
mwenye kufikiria mbali akumbuke kwamba Zitto aliwahi kushupalia issue ya buzwagi mpaka sitta akampa adhabu.na ndio issue iliyomletea umaarufu.niliwahi kuongea hapa kuhusu issue ya zitto na january kupokea marupurupu kutoka kwenye kampuni za migodi.zitto pia amewahi kutetea ununuzi wa mitambo chakavu ya dowans ambayo chama chake kilikuwa kikipinga hoja hiyo ya ununuzi wa vitu vilivyotumika.sioni sababu ya kumtetea mtu ambaye anaonekana anafanya mambo against na chama anachokiwakilisha.kwenye maandiko ya biblia yanasema NI HERI KUWA BARIDI AU MOTO KULIKO KUWA VUGUVUGU.Be blessed!
 
akili ndogo huzungumzia majina ya watu, akili za kati huzungumzia matukio, akili pevu huzungumzia maswala mazito.

kwa hiyo bwana "Pasco mtoa mada" chagua katika hayo makundi matatu hapo juu upo kundi gani???
 
Wanabodi,

Nimekuwepo Dodoma kwa haya na yale na miongoni mwa mengi, nimepata fursa kuzungumza na ZZK kuhusu his presidential bid ya 2015!.

Ame confirm bila kuuma maneno kuwa ni kweli yeye ni "Presidential Hopeful" na kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, atatupa karata yake kwenye "presidential bid" kupitia tiketi ya Chadema!.

ZZK amethibitisha kuwa atazingatia sheria, taratibu na kanuni zote za kuomba kuteuliwa kupitia chama chake cha Chadema na kunihakikishia kuwa iwapo hatapitishwa, atamuunga mkono kwa asilimia 100% mgombea yoyote atakayepitishwa na chama chake cha Chadema!.

Kauli hiyo ya ZZK, ni uthibitisho kuwa mwamuzi wa mwisho wa ni nani atasimamishwa kupeperusha bendera ya Chadema kwenye urais wa 2015, utafanywa na Chadema na sio ZZK.

Sifa za kiongozi kwa mujibu wa mmoja wa Ma Great Thikers wakuu na wa ukweli humu JF.



ZZK ana
1.Charisma(haiba)
2. Popularity(umaarufu)
3. intellectual (weledi)
4. 'Political strategy' mkakati wa kisiasa
5. Timing

Na hii ni sehemu tuu ya mchango wa Great Thinker mwingine mheshimiwa sana kuhusu sifa za kiongozi atakayetufaa kwa 2015, nimeedit kwa kupunguza zile sifa mimi nilizoziona sio necessary na kubakisha zile za muhimu tuu ambazo zote ZZK anazo!.


Pia Mkuu sana, ametusisitiza kiongozi ajaye, awe na uwezo.

MY Take.
ZZK anavyo vigezo, anao uwezo na anazo sifa zote za rais tumtakaye kwa mujibu wa sifa zilizoainishwa na wana jf wenzetu, Nguruvi3 na Mzee Mwanakijiji, na muda muafaka ukifika, ZZK atakapo tupa karata yake, miongoni mwa endorsment atakazo pata, ni ya Pasco wa JF!.

Kwa vile mimi sina chama, sio mwanachama, mshabiki, wala mkereketwa wa chama chochote, kwa Chadema nitaiunga mkono bid ya ZZK!. Kwa CCM bado namshabikia sana EL asimamishwe, na kama ni kweli afya yake ni mgogoro kuhimili mikiki mikiki ya 2015, then namshabikia Membe!. Kwa CUF na NCCR Mageuzi, nawashauri, wasi waste time and money kwenye presidential bid ili kuzipunguza kura za ushindi, kwa 2015, it won't work!.

Wale mnaendelea kumbeza ZZK, endeleeni, ili kwa sisi tuliofuatilia safari ya Barak Obama, toka alipoanzia, alipo pitia na hatimaye hapo alipofikia, mtakubaliana na mimi kuwa hii bid ya ZZK, siyo ya kubezwa hata kidogo!.
"Where there is a will, there is a way!".

NB, nawaombeni sana tutumie jina hili la ZZK, kwa vile jina lake kamili limetwajwa mmno mpaka linakinaisha au kuchusa!.
Mkuu kama ni kweli ulifuatilia rekodi na kampeni za obama mpaka ushindi wake basi tambua kuwa Zitto hana sifa yoyote ya kujilinganisha na Obama.kwanza Obama hakuanza kujitangaza kugombea uraisi miaka mitatu kabla ya uchaguzi.Matter of fact Obama hakuwahi kuplan kuja kugombea uraisi 2008.kama umefuatilia historia yake utaona kwamba alifuatwa na viongozi wanaoheshimika ndani ya chama chake cha democratic( majina yao pia yalitajwa) na kumshauri kugombea nafasi ya uraisi ambayo hata hivyo Obama alipinga wazo hilo.baada ya kumshauri sana na yeye(Obama) kupata ridhaa ya FAMILIA YAKE(mainly mke wake) ndipo alipo kubaliana nao.Pia rekodi ya Obama kabla hajawa senetor na baada ya kuwa senetor haina walakini hata kidogo.nikiimanisha kwamba Obama hajawahi kuhusishwa au kutuhumiwa kwenye issue yoyote ndani ya chama chake au serekali.hajawahi kutoa matamshi yanayopingana na maamuzi ya chama chake wala hajawahi kulumbana na viongozi wenzake ndani ya chama chake kwaajili ya maslahi binafsi.Mgombea yoyote mwenye rekodi ya kulumbana na viongozi wenzake ndani ya chama chake sio kiongozi mzuri.mgombea ambaye sio msikivu na anayejiona anajua zaidi kuliko wenzake sio kiongozi mzuri.amgombea ambaye anagombea uraisi ili tu apate madaraka au anayetaka madaraka kwa kisingizio cha DEMOKRASIA sio kiongozi mzuri.Demokrasia haitumiki pale ambapo kiongozi anataka kugombea nafasi fulani kwenye chama chake au nchi.demokrasia ni neno la kigeni ambalo watanzania bado hatuwezi kulitumia.pale wananchi wote watakapotambua umuhimu wa kila mwananchi mwenye umri zaidi ya miaka 18 ni wajibu wake kupiga kura,kwamba kiongozi mzuri atapatikana kwa kura za wananchi.kwamba ni haki na wajibu wa wananchi kumchukulia hatua kiongozi yeyote ambaye atakuwa hawasaidii.kwamba ni wajibu wa kila mwananchi mwenye shahada ya kupiga kura kwenda kupiga kura na kulinda kura yake.tanzania hatujafika huko.kwahiyo kuongelea suala la demokrasia kwa watanzania pasipo kujaribu kuwafundisha maana ya demokrasia ni uhuni mtupu.Be blessed!
Nadhani sifa nyingine muhimu ya Raisi ajaye ni TEAMWORK.wananchi waangalie historia ya wagombea na kujaribu kuona ni mgombea gani ambaye amekuwa na sifa ya kufanya kazi kwa style ya teamwork.namna gani wagombea waliweza kufanya kazi kwa ushirikiano na wenzao ili kufanikisha malengo yao.wahenga wanasema KIDOLE KIMOJA HAKIVUNJI MFUPA.Raisi hata awe na sifa nyingine zote hatakuwa mzuri kama atakuwa mbinafsi na akashindwa kuorganize viongozi wenzake kwenye masuala ya utendaji.
 
What makes him think that he can replace Dr Slaa? Let him deal with serious allegations against him of being an hypocrite and corrupt. He can be a friend to Kikwete but never a presidential material.
 
wejemani huyu kinda anaota urais hata siku moja zitto usidhani ni kazi rais kumjuwa kikwete umeshaona wewe kaa kuishia kuwaletea watanzania abari za kujisomea kwenye google maana haujuwi kitu zitto wewe ukishaingia kusoma google unawadanganya watanzania na riport zako za kijinga una mada yoyote wewe unachokalia ni kutafuta ccm wamekosea nini unalipuka watanzania tuamke tusikubali hu ujinga wa zitto huyu zitto aondoke haraka sana kwa anaitaji msahada mkubwa mimi nilipomuona alivyokuja kutudanganya karibu nimuamini khee nikajitahidi kumsoma jamaa ni mjinga kweli atawadanganya wajinga wa tanzania sio huku uzunguni bado sana upinzani bado tunaitaji watu makini mbowe slaa zitto mmmh no way ushauri tuu slaa akifunguwa chama chake pekeee achaguwe watu wake makini labla na asimuache yule mbunge wa singida labda mnakazi ya ziada
 
Napata hasira sana kuona mnamzungumzia zitto hana maana mnampa jina tuu kweli siasa za tanzania bado sana ccm kuna watu wa maana sio chadema watu wa maana inabidi mjitokeze kupitia ccm muweze kupambana na ujinga wa chadema maana mtu wa maana ni tundulisu tuu hapo lakini wengine ni zero nchi haichuliwi na matusi ,maandamano, ya kijinga kila siku ccm mnaweza tujipange pale tulipokosea basi turekebishe ni bora kuwapa nchi ccm kuliko kuwapa chadema ni zero kabisa
 
Zitto anahitajika kurudisha imani na matumaini ya wana Chadema juu yake kama kweli anakusudia kuwa raisi wa nchi hii kupitia Chadema.

Kwa hali halisi ilivyo sasahivi wanachama wengi wamekuwa wakimuona kama msaliti na kupunguza imani na uaminifu kwake. Kwakuwa hajachelewa na muda bado unamtosha kujirudi, basi asiipoteze nafasi hii ya kujirudi, aitumie vizuri kwa manufaa yake na mustakabali wake.

Mimi naamini Zitto anakuwa juu kisiasa akiwa Chadema, nje ya hapo hawezi kuwa juu kisiasa kama alivyo sasa. Ni muhimu sana acheze vizuri karata yake ndani ya Chadema bila kumsababishia chuki, hisia za usaliti, hisia za unafiki, hisia za ubinafsi ama hisia za undumilakuwili.

yuko ACT ila anawika kuliko chadema yote

ha ha ha
 
Wanabodi,

Wale mnaendelea kumbeza ZZK, endeleeni, ili kwa sisi tuliofuatilia safari ya Barak Obama, toka alipoanzia, alipo pitia na hatimaye hapo alipofikia, mtakubaliana na mimi kuwa hii bid ya ZZK, siyo ya kubezwa hata kidogo!.
"Where there is a will, there is a way!".

NB, nawaombeni sana tutumie jina hili la ZZK, kwa vile jina lake kamili limetwajwa mmno mpaka linakinaisha au kuchusa!.
Pasco
Nime note Zitto anatajwa tajwa sana humu jukwaani, nikaona na mimi nijikumbushe niliwahi kuandika nini kumhusu mtu huyu.
All and all, huyu Zitto sio mtu wa mchezo mchezo, he is a man to watch very closely!, sio mtu wa kawaida!.
P
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom