Zitto Kabwe kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA endapo.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto Kabwe kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA endapo....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Jul 27, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Nimekuwepo Dodoma kwa haya na yale na miongoni mwa mengi, nimepata fursa kuzungumza na ZZK kuhusu his presidential bid ya 2015!.

  Ame confirm bila kuuma maneno kuwa ni kweli yeye ni "Presidential Hopeful" na kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, atatupa karata yake kwenye "presidential bid" kupitia tiketi ya Chadema!.

  ZZK amethibitisha kuwa atazingatia sheria, taratibu na kanuni zote za kuomba kuteuliwa kupitia chama chake cha Chadema na kunihakikishia kuwa iwapo hatapitishwa, atamuunga mkono kwa asilimia 100% mgombea yoyote atakayepitishwa na chama chake cha Chadema!.

  Kauli hiyo ya ZZK, ni uthibitisho kuwa mwamuzi wa mwisho wa ni nani atasimamishwa kupeperusha bendera ya Chadema kwenye urais wa 2015, utafanywa na Chadema na sio ZZK.

  Sifa za kiongozi kwa mujibu wa mmoja wa Ma Great Thikers wakuu na wa ukweli humu JF.

  ZZK ana
  1.Charisma(haiba)
  2. Popularity(umaarufu)
  3. intellectual (weledi)
  4. 'Political strategy' mkakati wa kisiasa
  5. Timing

  Na hii ni sehemu tuu ya mchango wa Great Thinker mwingine mheshimiwa sana kuhusu sifa za kiongozi atakayetufaa kwa 2015, nimeedit kwa kupunguza zile sifa mimi nilizoziona sio necessary na kubakisha zile za muhimu tuu ambazo zote ZZK anazo!.

  Pia Mkuu sana, ametusisitiza kiongozi ajaye, awe na uwezo.
  MY Take.
  ZZK anavyo vigezo, anao uwezo na anazo sifa zote za rais tumtakaye kwa mujibu wa sifa zilizoainishwa na wana jf wenzetu, Nguruvi3 na Mzee Mwanakijiji, na muda muafaka ukifika, ZZK atakapo tupa karata yake, miongoni mwa endorsment atakazo pata, ni ya Pasco wa JF!.

  Kwa vile mimi sina chama, sio mwanachama, mshabiki, wala mkereketwa wa chama chochote, kwa Chadema nitaiunga mkono bid ya ZZK!. Kwa CCM bado namshabikia sana EL asimamishwe, na kama ni kweli afya yake ni mgogoro kuhimili mikiki mikiki ya 2015, then namshabikia Membe!. Kwa CUF na NCCR Mageuzi, nawashauri, wasi waste time and money kwenye presidential bid ili kuzipunguza kura za ushindi, kwa 2015, it won't work!.

  Wale mnaendelea kumbeza ZZK, endeleeni, ili kwa sisi tuliofuatilia safari ya Barak Obama, toka alipoanzia, alipo pitia na hatimaye hapo alipofikia, mtakubaliana na mimi kuwa hii bid ya ZZK, siyo ya kubezwa hata kidogo!.
  "Where there is a will, there is a way!".

  NB, nawaombeni sana tutumie jina hili la ZZK, kwa vile jina lake kamili limetwajwa mmno mpaka linakinaisha au kuchusa!.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo umemstosa EL?
   
 3. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Kama anakufaa mwambie Kama mgombea binafsi anaruhusiwa ajiwakilishe
   
 4. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Sasa mbona simsikii kwenye M4C?
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,219
  Trophy Points: 280
  divide n rule.....

  ccm wanacheza karata zao vizuri sana hapa....
   
 6. M

  Makwarukwaru Member

  #6
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 66
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ngoja tuone changamoto ya vijana sasa.
   
 7. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 259
  Trophy Points: 180
  Ulimuuliza kuhusu kashifa inayomnyemelea ya kula rushwa ya kumtetea mhando na wife yake?
   
 8. R

  Rwechu Member

  #8
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Niwakati wa kujenga chama sio kutafuta mgombea wa Urais
   
 9. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  2015 hana sifa ya kugombea nayo ni umri wake utakuwa chini ya miaka 42
   
 10. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ni upepo tu utapita
   
 11. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  nathubutu kusema ni bora tutawaliwe na fisadi kichwa cheupe kuliko huyo ndumilakuwili kuwa rais...
   
 12. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  This Sounds. japo alikuwa kwenye kazi za chama Overseas but he must engage in M4C campaigns.
   
 13. GreenCity

  GreenCity JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 4,651
  Likes Received: 2,094
  Trophy Points: 280
  ungezingatia hayo kwenye RED (NYEKUNDU) nadhani na wewe ungetulia kimya. lakin kwa kuwa hujazingatia hayo , basi na wewe umetumwa na huyo ZITTO.
   
 14. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Labda awe rais wa familia yako !
   
 15. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  2015,bado sana!zzk anatakiwa atumie busara na kutengeneza njia kwanza,na siyo kuropoka na kutafuta u'popular'!cdm inavichwa vingi vya maana vinavyofaa kabisa for presidecy,but vimetulia!why zzk?there must be something under the carpet!tuweni makini na huyu jamaa,na busara za kumkaripia zisipotumika huyu jamaa ataharibu chama na kudhoofisha nguvu na njia ya ushindi kwa chadema 2015.
   
 16. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Pasco,
  wewe unasema siyo mwanachama wkt unamsapoti Lowassa, halafu unatuletea uzushi hapa ili utugawe wanachadema? nenda zako na ccm yako. CHADEMA hawahitaji wewe uwaambie nani anafaa kuwa mgombea wao bali wana taratibu zao. Kama taratibu zikifuatwa hakuna shida. Wewe kwanza ni mchumia tumbo sijui(waandishi makanjanja) wanaoingia kwenye mikutano bila mwaliko. Labda Lowassa au Zitto amekuhaidi Post tutajuaje? Si unakumbuka kipindi cha uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki ulivyokosa msimamo, mara useme Sioi mara Nassary. Usituletee mambo ya Sheick Yaya ndani ya CHADEMA, hayo unaweza peleka CCM, kwani CHADEMA kuna utaratibu na tuna umoja. Na kamwe CCM kwa propaganda zao hamtaweza kukigawa CHADEMA.
   
 17. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  @Pasco 3 years to come ni muda mrefu na mengi yanaweza kutokea. Politics can change and take a complete turn kiasi kwamba hata endorsement yako ikabadilika.

  I prefer the fact kuwa: We cross the bridge when we are there. Time will tell. Time. Timex.
   
 18. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  zito anafaa ila Dr slaa anafaa zaidi
   
 19. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  mbona wewe Pasco na huyu zito wako mnawashwa sana na uraisi? hivi Mungu amewagonga mihuri kuwa mtakuwa hai hiyo 2015? hivi hamna kazi nyingine za maana za kufanya na kuona hili ni dili sana?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,736
  Likes Received: 1,447
  Trophy Points: 280
  Habari ya ovyo, tena ya kiimla na yenye nia zile zile za kuchumia tumbo kwa gharama ya ukombozi wa TZ.
   
Loading...