Zitto Kabwe kugombea urais 2020, aanza kampeni kabla ya wakati

Mr worldwide

JF-Expert Member
Dec 30, 2017
348
737
Zitto Kabwe ameamua kupitia chama chake cha ACT Wazalendo kuamua kuweka wazi nia yake ya kugombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania

Ni wazi sasa kampeni za Zitto zimeanza mapema kabla hata ya wakati, ndio Zitto Kabwe anapiga kampeni za urais kabla ya wakati.

Zitto anawataka wananchi hapo 2020 wachague na walinganishe wenyewe kati ya "hapa kazi tu" na hii ya kwake "kazi na bata".

Zitto anajitanabaisha kitofauti na Magufuli kwa kuirejea kilimo kuwa kipaumbele kwake kama ilivyokua katika awamu ya nne.

Je Zitto Kabwe anatosha kuongoza nchi?
Rais Magufuli yuko tayari kuruhusu ushindani katika nafasi yake na akubali kupingwa vijembe kipindi cha kampeni na mpinzani wake?

Usalama wa mpinzani wa kiti cha rais upo kwa kiwango gani? Zitto umejipangaje kiusalama? Hali ya nchi yetu kiusalama si ya kuridhisha.

NEC mnatambua kuwa Zitto ameanza kampeni kabla ya wakati? Sheria zinasemaje hapa?
 
Mgombea mwenza ni Maalim Seif ama nani? 2020 hakuna UKAWA? Lissu hagombei? Mbona ilisemwa kuwa Membe ndiye mgombea kupitia ACT au Zitto anatingisha kiberiti tu aone friction ilivyo?

Tatizo kubwa la Zitto ni kuwa haaminiki.
 
Kachukue na "LOUD SPEAKER" kabisa, ili usikike vizuri. Sijui lini mtaacha upuuzi wana lumumba, CCM campaign mlizofanya mwezi uliopita nchi nzima mlikaa kimya, hamkuongea, tena mlitembea na gari zenye speaker na konvoy la mawaziri wote, na meku alikua anatembea na maburungutu ya hela anagawa.

Nenda kalale, mdudu wewe.
 
Ninesoma tu aya ya kwanza nikaona umeandika "Katia nia" nikaachia hapo hapo. Kumbe kutia nia nako ni kampeni? Mbona mm pia nimeshatia nia ya kugombea hiyo nafasi?
Mbona Magufuli kila mteule pamoja na TBC wanafanya kampeni live kabisa na wanasema 2020 ni yeye?
Au Dhambi iko kwa Zitto na Maalim Seif tu?
Lala umalizie ndoto zako.
 
Huyo Zito na wapinzani wengine watakuwa wajinga kuendelea kukaa kimya huku Magufuli anafanya kampeni waziwazi, halafu wanaccm wanapotosha umma eti wapinzani wako kimya kisa hawana cha kuwaambia wananchi. Wakati ni sasa, tena wamechelewa.
 
Je Zitto Kabwe anatosha kuongoza nchi?

P
 
Hapa tayari kura za upinzani zitagawanyika zitaenda ACT na zingine UKAWA za CCM zitabaki palepale.
Tunashinda kwa kishindo CCM oyeee
 
Ndugu, usimshangae na campaign ina gharama nyingi sana, kama yeye anazo pesa za kufanya hivyo bila kuharibu amani, shauri kwake na pesa yake.

Kwani hiki chama chetu cha ccm, na hizi ziara zetu kila mikoa na ziara za Raisi na Mawaziri si pia ni mtayarisho wa campaign ya uchaguzi ujao. Mr worldwide,
 
Aaminike Mbowe asiaminike Zitto, acheni uzembe na usharati
Mgombea mwenza ni Maalim Seif ama nani? 2020 hakuna UKAWA? Lissu hagombei? Mbona ilisemwa kuwa Membe ndiye mgombea kupitia ACT au Zitto anatingisha kiberiti tu aone friction ilivyo?

Tatizo kubwa la Zitto ni kuwa haaminiki.
 
Mikakati inayoendelea sasa ni kumshawishi Mzee Sumaye agombee kupitia ACT

Vita iliyopo sasa sio ya Urais 2020, vita iliyopo ni ya kugombea U Kiongozi wa Upinzani Bungeni kati ya Zitto na Mbowe

Mbowe anamshawishi Lissu agombee urais sio kwa kuwa anadhan atashinda la hashaa, anataka asaidie wapate kura nyingi ku maintain Ruzuku ambayo inategemea kura za Urais , Mzee Lowassa amesaidia Chadema kukunja 200M kila mwezi kuanzia Nov, 2015

Zitto nae kaanza mikakati ya kumshawishi Sumaye kuwania Urais ili tu asaidie wapatepate kura za kutunisha Mfuko wa Ruzuku
 
Hapa tayari kura za upinzani zitagawanyika zitaenda ACT na zingine UKAWA za CCM zitabaki palepale.
Tunashinda kwa kishindo CCM oyeee
CCM wanalijua hilo ndio maana walifuta sheria inayomtaka rais kupata zaidi ya 50% ya kura la sivyo kuna hatari ya kuaibika
 
Pohamba, Kuna ukweli kwa asilimia fulani katika hili, coz chama cha siasa bila ruzuku mambo hayaendi, so, bora kutumia njia zozote zinazowezekana kuhakikisha wanapata idadi ya kura zitakazowawezesha kupata ruzuku, but also, Maalim Seif ni mtaji kwa Zitto upande wa Zanzibar, but only if ataruhusiwa kugombea.
 
Back
Top Bottom