Tetesi: Zitto Kabwe Kufungwa jela?

mkalamo

JF-Expert Member
Sep 7, 2013
324
347
Ijumaa hii bunge litahitimisha kikao chake na moja ya jambo litakalofanyika ni kutoa hukumu kwa mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe wa ACT Wazalendo

Ni wazi kwa mazingira yalivyo Zitto atasimamishwa kuhudhuria kikao kijacho cha Januari,lakini pia kuna uwezekano wa kushtakiwa nje ya bunge kwa kule kuweka utetezi wake hadharani

Tayari magazeti kadhaa yaliyoandika utetezi wa Zitto Katika kamati ya Bunge yameshaitwa mjini Dodoma kwa ajili ya kuhojiwa ikiwa ni maandalizi ya kumfungulia mashtaka mengine Zitto ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya awamu ya tano huku akilituhumu bunge kushindwa kusimamia wajibu wake

Tusubiri na kuona kitakchojiri baada ya Ijumaa
 
Back
Top Bottom