Zitto Kabwe: Jina la Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar tulilompelekea Rais Mwinyi limetokana na wosia wa Maalim Seif

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,833
2,000
Kiongozi mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema jina walilompelekea Rais Hussein Mwinyi kwa ajili ya uteuzi wa makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar limetokana na wosia aliouacha Maalim Seif mwenyewe.

Zitto Kabwe amesema mtu huyo anaenda kumsaidia sana Rais Mwinyi na pia atawaunganisha wana ACT Wazalendo baada ya kuondokewa na nguzo yetu muhimu.

Zitto Kabwe yuko kwenye mjadala katika kipindi cha Clouds 360.

Chanzo: Clouds tv

Maendeleo hayana vyama!
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
7,687
2,000
Kwa vile selikari ya CCM ilimpamba sana Maalim Seif akiwa mfu kana kwamba walimkubali kihivyo basi na waridhie sasa wosia wake maana ndiyo huo tena.

Vinginevyo yale maneno yote mazuri juu yake baada ya kifo yatakuwa kuvikana vikana vilemba vya ukoka tu. Kuwa uhalisia ni ule tuliouona kwenye misukosuko waliyokuwa wakimpitisha Maalim katika maisha yake yote.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 

sem2708

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,471
2,000
How can we trust him? Ni ujanja ujanja tu huo. Ni dalili ya kuwa chaguo la wengi halijateuliwa
 

Bishop Hiluka

Verified Member
Aug 12, 2011
6,478
2,000
Sasa kama rais ndo anateua kwanini wampangie
Kwani ACT wamempangia au wamependekeza jina kama Sheria inavyosema? Wao wameshamaliza jukumu lao kuteua jina na sasa ni jukumu la Rais Mwinyi kuteua na kutangaza...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom