Tunamweshimu Mbowe, ndo maana tunashindwa kusema ukweli...Zitto ni mwizi wa kisasa, nakumbuka enzi za akina Slaa Zitto alisumbua sana CHADEMA, mpaka akina Slaa wakawa wanamkaimisha ofisi Myika, Mpaka akina Kikwete wakamsaidia kumfungulia chama ili kuigawanya chadema. Bahati nzuri Magufuli alivyoingia tu madarakani alikuwa anajua mamluki wote, hivyo mamluki wote aliwasagia kunguni na ndio chanzo cha Zitto kuanza chuki na Magufuli. Zitto ni tapeli wa siasa tu, yeye kuuza mechi ili mkono uende kinywani haoni hasara
Aliyeigawanya CHADEMA ni Mbowe na wala sio Zitto!!!
Zitto hata alipoondoka CHADEMA na kuunda chama chao na akina Mkumbo, wala hapakuwa na impact yoyote ya maana!! CHADEMA ilibaki kuwa ile ile!!
Mgawanyiko CHADEMA ulikuja baada ya kuja Lowassa... tuache unafiki!!
Kuja kwa Lowassa kukamfanya Dr. Slaa achafukwe!
Dr. Slaa alikuwa na wafuasi wengi sana CHADEMA, na alikuwa na ushawishi mkubwa maradufu... ni mjinga tu ndie atapinga hili!!!
Tukiacha unafiki, a moment Lowassa alipotangazwa kugombea urais, CHADEMA ikawa sio moja tena! Wengine waliingia kwenye uchaguzi mkuu 2015 huku wakiwa na vinyongo!!
Vinyongo vilikuwa vya namna mbili... mosi, ilibidi tu wakubaliane na ujaji wa Lowassa hivyo hivyo shingo upande, na pili, wengine walikuwa na kinyongo kwa sababu ya Dr. Slaa!!
Magufuli nae akaja kuendeleza tu kupiga kwenye kidonda kilichokuwa kimeachwa na ujio wa Lowassa ambapo akaanza kununua mpinzani mmoja baada ya mwingine ! Watu wakawa more demoralized hasa baada ya kuona hata huyo Lowassa mwenyewe akakaa mbali na chama mara baaada ya kupita uchaguzi mkuu!!
Huo ndo ukweli mchungu ambao watu mnakwepa kuuongea! Sio kwa sababu hamjui, bali ndo yale yale ya wana-CCM!! Hakuna kuwasema wakubwa!!