Zitto Kabwe: "Hatudanganyiki - Septemba 2015 mishahara Serikalini ilikuwa 523B lakini Julai 2019 ni 566B!"

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Ninaamini hii tweet ya mheshimiwa Zitto Kabwe hapa chini ipo self-explanatory.

Binafsi sina cha kuongeza zaidi ya na mimi pia kushangaa tu kama alivyoshangaa
Zitto !

Mwisho kwa Leo: Sept 2015 gharama ya mishahara ya Wafanyakazi ilikuwa shs 523 bilioni. Mwaka 2016 na 2017 wakaondolewa wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki. Gharama ya mishahara July 2019 ni shs 566 bilioni. Hakuna nyongeza ya mishahara, hakuna ajira mpya kihivyo! HATUDANGANYIKI

Halafu Magufuli anapongezwa kwa KUPAMBANA NA UFISADI. Magufuli anaibana ofisi ya CAG ambayo ndiyo ingemsaidia katika kutanzua hivi vitendawili. CAG anapigwa vita kila kona ili asifanye kazi yake vizuri. anapunguziwa bajeti kila kukicha. anashambuliwa na kutakiwa kujiuzulu. Rais mwenyewe yuko pembeni kumbe wajanja tunajua kwamba ndiye anayemtuma Ndugai na wengine wamshambulie CAG.
 
Ninaamini hii tweet ya mheshimiwa Zitto Kabwe hapa chini ipo self-explanatory.

Binafsi sina cha kuongeza zaidi ya na mimi pia kushangaa tu kama alivyoshangaa Zitto !

Huyu nae akili kashikiwa .Kwani Malimbikizo na madai ya Mshahara haiongezi bajeti?

Awadanganye wakigoma wenzake Serikali imeajiri walimu Tamisemi na pia imeajiro manesi mwaka Jana inakuaje anasema hakuna Ajira Mpya??Tumbafu kabisa!!!
 
Etwege anachosema Zitto ni kwamba, kama safari na semina zimefutwa, wafanyakazi "hewa" wameondolewa na ajira iliyofanywa na serikali ni ajira isiyolingana na walioondolewa kwa wingi wake, ni kwa nini mishahara haiongezeki ama matumizi kupungua kwenye eneo la mishahara?

Kwa hoja yake ya kimahesabu ni kwamba bilioni 566 zilizotumika kwa mishahara Septemba 2019 ukitoa na Bilioni 523 zilizotumika kwa malipo kama hayo mwaka 2015, unaona tofauti inakuwa ni ongezeko la shilingi bilioni 43 tu.

Hoja ya zitto ni hii: Inawezekana ajira iliyofanywa ni ndogo sana ama waliopunguzwa hawajapunguza matumizi ya fedha kwenye eneo la mishahara. Jee waliopunguzwa waliokoa shilingi ngapi na walioajiriwa upya wanatumia shilingi ngapi kwenye malipo ya mishahara yao.
 
Ninaamini hii tweet ya mheshimiwa Zitto Kabwe hapa chini ipo self-explanatory.

Binafsi sina cha kuongeza zaidi ya na mimi pia kushangaa tu kama alivyoshangaa Zitto !

Ivi kweli Zitto ana amini tangu Jully 2015 mbaka Jully 2019 Serikali haija ajalili ata mtu mmoja!! Zitto kweli yupo apa Tanzania au alisafir au kikk!!!
 
1569580223005.png

Watu wa CCM ni kama huyu Mzee. Fasheni nyingine haziwafai wazee!!
 
Ninaamini hii tweet ya mheshimiwa Zitto Kabwe hapa chini ipo self-explanatory.

Binafsi sina cha kuongeza zaidi ya na mimi pia kushangaa tu kama alivyoshangaa Zitto !
Mwisho kwa Leo: Sept 2015 gharama ya mishahara ya Wafanyakazi ilikuwa shs 523 bilioni. Mwaka 2016 na 2017 wakaondolewa wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki. Gharama ya mishahara July 2019 ni shs 566 bilioni. Hakuna nyongeza ya mishahara, hakuna ajira mpya kihivyo! HATUDANGANYIKI

Je, na mna uhakika kuwa hakuna ajira mpya zilizoongezeka tangu mwaka 2015? Je, hakuna nyongeza za kila mwaka kwenye mishahara ya zamani? Nauliza hivi kwa sababu mimi si mmojawapo wa wale ambao hayo mambo mawili niliyouliza, yanawahusu
 
Kwani serikali haijaajiri tangu 2015?
Au ajira mpya mpaka zile zinazoajiri wengi kwa mkupuo?
Ukiweza tembelea website ya utumishi tangu 2015 mpaka sasa waweza ona matangazo luluki ya ajira au nazo ni kick?
Pia mashirika ya serikali mengi kama Tanesco, Tanroads, na mengineyo yamekuwa yakiajiri hivyo ongezeko lazima litokee! Japo haizuii kuifuatilia serikali ije na data sahihi za ongezeko la waajiriwa tangu 2015 vs punguzo la waajiriwa lililopaswa kuleta punguzo la kiwango cha fedha zinazolipwa kama mishahara...
 
Je, na mna uhakika kuwa hakuna ajira mpya zilizoongezeka tangu mwaka 2015? Je, hakuna nyongeza za kila mwaka kwenye mishahara ya zamani? Nauliza hivi kwa sababu mimi si mmojawapo wa wale ambao hayo mambo mawili niliyouliza, yanawahusu
Ajira mpya zipo nyingi tu ila nyongeza nasikia zilisitishwa..
Mimi nae machinga njnaefuatilia mambo ya ajira nchini maana huwezi juwa zali la mentali naweza pata kauteuzi siku moja!
 
Ivi kweli Zitto ana amini tangu Jully 2915 mbaka Jully 2019 Serikali haija ajalili ata mtu mmoja!! Zitto kweli yupo apa Tanzania au alisafir au kikk!!!

Ishu ni kuwa kama walipunguzwa wafanyakazi hewa maelfu, ni dhahili wanaoajiliwa wanajazia sehemu ya watu walio staafu. Pengine, waajiliwa wapya wanaweza kuwa wanazidi idadi ya walio staafu lakini, viwango vya mishahara ni vidogo kwa sababu ndiyo wanaanza ajira. Waajiliwa hawa hawawezi kuwa wameongeza kiwango cha mishahara kwa 43B juu zaidi wakati huo huo kuna watu hewa walioondolewa kwenye ajira.!!
 
Halafu Magufuli anapongezwa kwa KUPAMBANA NA UFISADI. Magufuli anaibana ofisi ya CAG ambayo ndiyo ingemsaidia katika kutanzua hivi vitendawili. CAG anapigwa vita kila kona ili asifanye kazi yake vizuri. anapunguziwa bajeti kila kukicha. anashambuliwa na kutakiwa kujiuzulu. Rais mwenyewe yuko pembeni kumbe wajanja tunajua kwamba ndiye anayemtuma Ndugai na wengine wamshambulie CAG.

Ugomvi wa CAG na jiwe kupitia kibaraka wake Ndugai ni hizi fedha. Tena hili alilisema Zitto unaweza kukuta ni kidogo, ukweli ni deni zaidi ya hili.
 
Hayo mambo anafanya yeye mwenyewe.
Halafu Magufuli anapongezwa kwa KUPAMBANA NA UFISADI. Magufuli anaibana ofisi ya CAG ambayo ndiyo ingemsaidia katika kutanzua hivi vitendawili. CAG anapigwa vita kila kona ili asifanye kazi yake vizuri. anapunguziwa bajeti kila kukicha. anashambuliwa na kutakiwa kujiuzulu. Rais mwenyewe yuko pembeni kumbe wajanja tunajua kwamba ndiye anayemtuma Ndugai na wengine wamshambulie CAG.
 
Ninaamini hii tweet ya mheshimiwa Zitto Kabwe hapa chini ipo self-explanatory.

Binafsi sina cha kuongeza zaidi ya na mimi pia kushangaa tu kama alivyoshangaa Zitto !
Mwisho kwa Leo: Sept 2015 gharama ya mishahara ya Wafanyakazi ilikuwa shs 523 bilioni. Mwaka 2016 na 2017 wakaondolewa wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki. Gharama ya mishahara July 2019 ni shs 566 bilioni. Hakuna nyongeza ya mishahara, hakuna ajira mpya kihivyo! HATUDANGANYIKI

Na eti anaokota kodi 1:3tr, hii ni tozo toka halmashauri na fine za magari na hela za watu anazoiba kutoka mabenki
 
Back
Top Bottom