Zitto Kabwe, Hashim Rungwe na Kafulila Waanzisha Chama Kipya cha Siasa - CHAUMA

Status
Not open for further replies.
Hakuna umaarufu wa ZZK mbali na CHADEMA,akishaondoka basi tena ndo hivo anapotea mazima
 
Chadema hamuwezi kuvuka mstari wa 2015.Kuna siku ililetwa sredi hapa kuwahusisha akina Ben Saanane kuwa nyuma ya hiki chama na akina zitto kabwe na kafulila.
 
Zitto hawezi kuondoka Chadema nyie wote mmemkuta kajiunga Chadema ana umri wa 16 na ndoto zake ni kugombea urais mwaka 2015 kupitia Chadema.
 
Ndugu,

Mtakumbuka kuwa hivi karibuni Msajili wa vyama vya Siasa, John Tendwa, amekipa usajili wa muda chama kipya cha siasa kinachojulikana kwa jina la Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA).

Chama hiki kinasimamiwa na mwanaharakati (utawala bora) maarufu nchini, Ndugu Walace Mayunga ambaye wenye chama wamemkabidhi kazi ya kukisajili hadi kipate usajili wa kudumu.

Makao Makuu ya CHAUMA ni Kijitonyama Mtaa wa Kameruni. Bandera ya CHAUMA ina rangi nne; nyeusi, nyeupe, nyekundu na njano. Kauli mbiu ya CHAUMA ni Nguvu ya Mabadiliko.

CHAUMA kinaonekana kuwa na mkakati mkubwa kwa sababu kinatumia waliokuwa makada wa CHADEMA, NCCR-Mageuzi na TLP kutafuta wanachama 200 kutoka angalao mikoa 10 kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa No. 5 ya 1992.

-Chanzo Mdau wa CHAUMA.

My take:
Ni wazi kuwa mwenendo (kujitenga na M4C) na kauli za ZZK ambazo kila mara zinaonekana kuwa na malengo yaliyofichika; kujijenga binafsi (kupata wafuasi wengi) tayari kwa safari ya CHAUMA mara baada ya zoezi la usajili wa kudumu kukamilika.

............kwa nini asiwe Mbowe, Slaah na Lema ndo wenye hicho chama !? au upuuzi pia unaweza kujificha katika tetesi ?
 
Hakuna mwanachama wala kiongozi yoyote wa CDM aliye juu ya chama,nasubiri kuona anguko la hao makanjanja wa siasa,walafi wa madaraka na watumishi wa mafisadi.

Mungu atawalaani wote wanaoiombea mabaya CDM kwa maana kuwepo kwake ni mpango wa MUNGU.
 
Kwenye Ndoto hizo hizo za ki-CCM AMOEBA (sawa na familia ile ile ya CCM UFISADI tunachokifahamu vema zaidi), kinadharia Urais unabakia CCM Orijino, Umakamu kwenda CCM-ADC aka kijana wa Pemba anayeendelea kuegesha matairi zake pale KAFU hadi hivi sasa na CCM-CHAUMA kutoa Uwaziri Mkuu aliye na nguvu na madaraka kamili kwenye katiba.

Lakini vyote vya huko ma-njozini ni swala la kuyaachilia huko huko kitandani na kuendelea kuchapa kazi ya kufa mtu pale CDM kwa kuimarisha zaidi ile SILAHA YAKE YA MAANGAMIZI YA HALAIKI YA MAFISADI; Movement for Change. Mkuu Dr Slaa na Makamanda wote wa M4C taifa hadi vitongojini nadhani sote tuko pamoja hadi hapo.

Mara baada ya M4C na BAVICHA kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kukibomoa CCM kila kona ya nchi, hivi sasa kombora lielekezwe kutwanga CCM-AMOEBA na wanawe wote wa kisiasa kote nchini.

Kipimo chetu cha mafanikio kiwe ni kuwanasa uongozi wa serikali za mtaa kwa asilimia 90 kote nchini. Na hili liwe ni ombi letu wakati wote tunapokutana na wananchi kwamba CHADEMA kinawataka kukichagulia madiwani waadilifu kwa asilimia zaidi ya 90 ili safari yetu ya 2015 iweze kuwa maridhawa zaidi.
 
Hatushangai alianza Sitta na Nappe kupima upepo ccj badae walikana hata samani zao za ofisi.!
 
Tulishamjua kitambo dhamira zake ndio maana amekua ni mtu wa kuropoka sana
 
Hadi hapa viwango vya undurakuwili ulikofikia,

ni vema ikafahamika wazi kwamba CHADEMA ni chama imara kama simba na kwamba kwetu sie pale CHADEMA hakuna kitu Miungu-Watu wasioweza kusahaulika ki-urahisi tu katika matukio ya kisiasa; I mean NO ONE is indespensable as at CHADEMA party of today and her strongly anchored distinguishing set of principles that has always made us what we are to-date.

Yeyote anayetekenyeka na kutamani saaaana kwenda kukitumikia CCM katika matawi yake mojawapo, wala sipate taabu ya kusubiri kesho badala yake akaondoke leo na wengine huku lazima tutamuandalia sherehe ya kutakiana kheri katika demokrasia.

Na huo ndio ukomavu wa CHADEMA kwa miaka yote iliosababisha CCM kubakia chama dhaifu ajabu inayokimbilia MKAKATI DHAIFU NA VURUMAI ZAIDI iitwayo serikali ya mseto wa MAFISADI wanaojipanga upya kuja kulimaliza kabisa taifa letu.

Wengine humu tunajiuliza kwamba enyi wenye safari zenu za kisiasa mnaondoka lini au hadi KUJA KUPATA NAULI kiaina?????????
 
Kwenye Ndoto hizo hizo za ki-CCM AMOEBA (sawa na familia ile ile ya CCM UFISADI tunachokifahamu vema zaidi), kinadharia Urais unabakia CCM Orijino, Umakamu kwenda CCM-ADC aka kijana wa Pemba anayeendelea kuegesha matairi zake pale KAFU hadi hivi sasa na CCM-CHAUMA kutoa Uwaziri Mkuu aliye na nguvu na madaraka kamili kwenye katiba.

Lakini vyote vya huko ma-njozini ni swala la kuyaachilia huko huko kitandani na kuendelea kuchapa kazi ya kufa mtu pale CDM kwa kuimarisha zaidi ile SILAHA YAKE YA MAANGAMIZI YA HALAIKI YA MAFISADI; Movement for Change. Mkuu Dr Slaa na Makamanda wote wa M4C taifa hadi vitongojini nadhani sote tuko pamoja hadi hapo.

Mara baada ya M4C na BAVICHA kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kukibomoa CCM kila kona ya nchi, hivi sasa kombora lielekezwe kutwanga CCM-AMOEBA na wanawe wote wa kisiasa kote nchini.

Kipimo chetu cha mafanikio kiwe ni kuwanasa uongozi wa serikali za mtaa kwa asilimia 90 kote nchini. Na hili liwe ni ombi letu wakati wote tunapokutana na wananchi kwamba CHADEMA kinawataka kukichagulia madiwani waadilifu kwa asilimia zaidi ya 90 ili safari yetu ya 2015 iweze kuwa maridhawa zaidi.

aksante baba. ujumbe wako maridhawa na tnaukubali. cdm twanga kotekote
 
Haya ni baadhi ya makundi ya Chadema katika kuelekea uchaguzi mkuu.
 
Sasa ZITTO KABWE; HASHIM RUNGWE na KAFULILA na Pia kuna KIONGOZI aliyeki-register hicho CHAMA
Sasa Ukiangalia na kuwapa EXAM ya nani awe MWENYEKITI ni nani atabaki CHINI bila kukimbilia JUU ?? SISI tunajua
Wasiofaaa... lakini Mmmm...

Our Political System.png
 
Mkuu umakini ulioutumia katika kufikisha ujumbe wako hapo chini hakika kofia nalivua mwenyewe; heshima kwa sana!!!!!!!

Sasa ZITTO KABWE; HASHIM RUNGWE na KAFULILA na Pia kuna KIONGOZI aliyeki-register hicho CHAMA
Sasa Ukiangalia na kuwapa EXAM ya nani awe MWENYEKITI ni nani atabaki CHINI bila kukimbilia JUU ?? SISI tunajua
Wasiofaaa... lakini Mmmm...

View attachment 67131
 
and he is very right!
Nadhani hatumtendei haki zitto na chadema pia, mpaka sasa yeye ni kiongozi mkubwa kwenye chama na bado anafanya kazi za chama kupambana nae kusema kweli ni kupambana na chadema kwa sababu kadhaa..kwanza, ni kutengeneza makundi ndani ya chama maana lazima wapo watu ndani ya chama ambao wanamkubali zitto na wanampenda kama icon wao
pili, chadema kama chama kina mbinu mbalimbali za kuwachenga maadui zao kwa zitto kusema atagombea uraisi yaweza kuwa mbinu mojawapo kudivert mind za maadui wao maana mpaka sasa uongozi haujatoa taarifa yoyote kulaani kauli za zitto
mwisho, mie sidhani kama watu wote siku moja tutafanana fikra zetu mbowe hawezi kuwa slaa, zitto hawezi kuwa tundu lissu nk. Tofauti zao kifikra maadam haziathiri chama ni vema zikavumiliwa unleśs tumetumwa na ccm kwa kuvaa kombati za chadema!
Masuala ya uongozi waachiwe viongozi..nawasilisha
 
Zitto hawezi kuondoka Chadema nyie wote mmemkuta kajiunga Chadema ana umri wa 16 na ndoto zake ni kugombea urais mwaka 2015 kupitia Chadema.

poor analysis,think before write anything broda.,may b'w not you but someone was use ur ID.NYIE NDO MNADUMISHA FIKRA ZA MWENYEKITI.
 
Hivi ni kwa nini wafuasi wengi wa CHADEMA wana wasiwasi sana na mwenendo wa Zitto kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya Chadema?
 
Hivi ni kwa nini wafuasi wengi wa CHADEMA wana wasiwasi sana na mwenendo wa Zitto kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya Chadema?
Labda kwa matendo yake kutwa yuko misafari na mwenyekiti wa CCM,halfu matangazo ya kutaka uraisi anayatoa kukiwa na agenda muhimu ya chama kuvuruga ile agenda na kubadilisha attention labda ndio maana wanamuona kirusi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom