Zitto Kabwe, Hashim Rungwe na Kafulila Waanzisha Chama Kipya cha Siasa - CHAUMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto Kabwe, Hashim Rungwe na Kafulila Waanzisha Chama Kipya cha Siasa - CHAUMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sophist, Oct 4, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,087
  Likes Received: 1,731
  Trophy Points: 280
  Ndugu,

  Mtakumbuka kuwa hivi karibuni Msajili wa vyama vya Siasa, John Tendwa, amekipa usajili wa muda chama kipya cha siasa kinachojulikana kwa jina la Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA).

  Chama hiki kinasimamiwa na mwanaharakati (utawala bora) maarufu nchini, Ndugu Walace Mayunga ambaye wenye chama wamemkabidhi kazi ya kukisajili hadi kipate usajili wa kudumu.

  Makao Makuu ya CHAUMA ni Kijitonyama Mtaa wa Kameruni. Bandera ya CHAUMA ina rangi nne; nyeusi, nyeupe, nyekundu na njano. Kauli mbiu ya CHAUMA ni Nguvu ya Mabadiliko.

  CHAUMA kinaonekana kuwa na mkakati mkubwa kwa sababu kinatumia waliokuwa makada wa CHADEMA, NCCR-Mageuzi na TLP kutafuta wanachama 200 kutoka angalao mikoa 10 kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa No. 5 ya 1992.

  -Chanzo Mdau wa CHAUMA.

  My take:
  Ni wazi kuwa mwenendo (kujitenga na M4C) na kauli za ZZK ambazo kila mara zinaonekana kuwa na malengo yaliyofichika; kujijenga binafsi (kupata wafuasi wengi) tayari kwa safari ya CHAUMA mara baada ya zoezi la usajili wa kudumu kukamilika.
   
 2. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hamna shida CDM ilianza zamani kwa umakini na ni miaka 20 sasa ndio kina vuma. Wajitahidi.
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ZITTO ameingiaje hapo?
   
 4. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mmmmhhhhhh! Ya kwel hayo? Sasa nani atakuwa mwenyekit,manake wote wa3 wanapenda uboss
   
 5. Az 89

  Az 89 JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 1,613
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Another shit
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Oct 4, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Msije kushangaa jamaa anajijenga kisiasa akiwa chadema, destination = chauma
   
 7. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  RANGI NYEKUNDU - WAMESHA MWANGA DAMU au WATAMWAGA DAMU
  ? Hizi

  Bendera zetu bila
  Umaana zinatisha!!!
   
 8. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Yakufikirika haya!!!
   
 9. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,990
  Likes Received: 3,739
  Trophy Points: 280
  re zitto kuanzisha chama...big deal?

  mbona hata chairman wake mbowe alivyokuwa akihutubia wadau wa US recently alim-quote mwalimu JKN kuwa "chama si baba/mama yangu"?
  hapa mbowe alikuwa aki-imply simply that anaweza kuondoka chadema as/when the situation compels him to!

  hivi vyama vya siasa vikiendekeza kutegemea personalities badala ya established infrastructure, vyafwa!!
   
 10. m

  malaka JF-Expert Member

  #10
  Oct 4, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  ZITTO ni ZITTO akiwa CDM akitoka sidhani kama atakuwa ZITTO. CDM inaweza songa bila hata zito wala slaa. Vifaa vipo vingi usjali.
   
 11. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #11
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Subutu CHADEMA HAPENDWI MTU ILA NI CHAMA! WANANCHI HAWATAJALI NI NANI ATAKAYEGOMBEA URAIS LA HASHA. BALI YOYOTE ILIMRADI CHADEMA IONGOZE KWA SABABU VIONGOZI WAADILIFU NA WANAOFUATA KANUNI NA SHERIA WAKO CDM. KWA HYO HATA ZZK AKIONA WATU WANAHUDHURIA KWENYE MIKUTANO YAKE ASIDHANI NI YEYE WANAMFUATA LA HASHA NI KWA SABABU NI CDM INAFANYA MKUTANO EMBU AJARIBU HATA KWA KUTANIA KWAMBA ATAONDOKA CDM UONE NI AKINA NANI WATAMFUATA ?
   
 12. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  umbea wa hisia na wivu wa kike utakumaliza ndugu, kujadili mambo bila ushahidi ni wehu tu
   
 13. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Zitto Kabwe: Kumbikumbi huruka na kuliwa na kunguru
  Na Nkwazi Mhango - Imechapwa 23 December 2009

  ZITTO Kabwe mbunge wa Kigoma Kaskazini, amekiri kumpa magari matatu ofisa habari za zamani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), David Kafulila.


  Magari hayo anayatoa kama msaada kwa Kafulila ili aweze kushinda kampeni za ubunge katika jimbo la Kigoma Kusini. Hizi ni habari zinazozua maswali mengi, ikiwamo utajiri na uwezo wa Zitto kiuchumi.


  Je, inakuwaje Zitto aweze kumiliki magari matatu wakati kipato chake kinajulikana? Lakini la pili, Kafulila na Zitto wanawezaje kuanza kampeni za ubunge wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi haijatangaza?


  Tayari Zitto amekaririwa akisema, “Ni jambo la msingi kupunguza idadi ya wabunge wa CCM…ndiyo maana nimeamua kumsaidia Kafulila katika chama alichopo (NCCR-Mageuzi). Nipo tayari kujitolea kwa kijana mwingine anayegombea, hata kwa chama kingine, isipokuwa CCM.”


  Kwa maneno ya Zitto ni kwamba anamuunga mkono Kafulila, ingawa bado anadai yuko CHADEMA. Ni ajabu kidogo. Je, kama CHADEMA wataamua kusimamisha mgombea Kigoma Kusini wakati Zitto ana mtu wake, atamuunga mkono nani kati ya mgombea wa chama anachodai kimemlea na kumkuza na kumfikisha hapo alipo na rafiki yake kipenzi?


  Si vizuri kumsemea Zitto wala Kafulila. Kuna haja ya CHADEMA kuuliza swali hili kabla mambo hayajafika huko. Kwa sasa, Zitto ama kwa kujua au vinginevo, anaanza kujiona maarufu kuliko chama, kama Jakaya Kikwete-kwa mujibu wa maneno ya katibu mkuu wa CCM, Yusufu Makamba.


  Ifahamike. Kumbikumbi akaribiapo mauti huotesha mbawa na kuruka na kuishia kuliwa na kunguru.

  Inapofikia mtu akafikia kujiona bora kuliko chama, huyu bila shaka hakifai chama wala chama hakimfai. Na lazima kuna tatizo, tena kubwa tu. Hivyo, uwezekano wa kukitosa chama wakati mbaya, hasa ule wa uchaguzi, ni mkubwa. CHADEMA wasingoje kufika huko.


  Siasa za Tanzania zina bahati mbaya. Chama kinamlea mtu hadi kufikia umaarufu kama alivyo Zitto Kabwe sasa. Halafu mtu huyu aliyefinyangwa na kulelewa na chama, analewa sifa kiasi cha kujiona bora kuliko chama. Mwisho wake huwa mbaya kwa mhusika na chama. Daniel arap Moi wa Kenya alifikia hatua ya kulewa sifa hizi pale alipoitwa profesa wa siasa. Alifanya ubabe hadi akakikosesha dola chama chake cha KANU.


  Kuna haya ya wanasiasa kuchagua kati ya chama na urafiki. Tumekuwa tukimshutumu Kikwete na CCM kwa kuendekeza urafiki na kujuana. Hata wapinzani wanamlaumu kwa hili, hasa kwa kusema anaendesha nchi “kishikaji.” Hili sina mjadala nao wala sitaki kuingia undani wake. Lakini CHADEMA waangalie wasitoe kibanzi kwenye jicho la mwenzao wakaacha boriti kwao. Zitto kwa watu wa nje ya chama chake anaonekana kuwa mguu mmoja ndani na mwingine nje. Ushahidi ni shaka juu ya msimamo wake. Kwenye mkutano wa Opesheni Sangara kule Tanga watu wanataka kujua kama Zitto bado yumo chamani au la.


  Ni rahisi mtu kukanusha, lakini ushahidi wa mazingira unaweza kupaaza sauti kuliko mwenye kukanusha. Ingawa Zitto anasisitiza kuwa yuko CHADEMA, matendo husema zaidi ya maneno matupu. Inakuwaje Kafulila awe mali kuliko chama? Zitto anapaswa kubanwa ajibu swali hili kwa usahihi na majibu yanayoingia akilini siyo kupiga siasa. Je, kwa kumuunga mkono Kafulila, hata dhidi ya uamuzi wa CHADEMA, Zitto hadhihirishi asivyokubaliana na hukumu aliyopewa Kafulila?

  Kama chama kilimuona Kafulila ana makosa na kikafuata taratibu zote za kumtimua, naye akaamua kujitoa na kutoa kashfa nyingi, maana yake ni kwamba kuna mgongano hata kama wahusika hawataki kulikubali hili. Litakuwa jambo la ajabu kwa mtu wa cheo na elimu ya Zitto kutoliona hili. Wenzake wamekaa chini wakamtimua Kafulila na kutaja makosa yake-kuvujisha siri za CHADEMA.


  Yeye bado anamtetea. Je, huku si kutetea madhambi yake au kuonyesha kuwa kipenzi chake kimeonewa? Kwanini asimtetee kwa namna inayoeleweka badala ya kuendelea kukidhoofisha chama?Ifahamike. Tunaelekea kwenye uchaguzi mwakani. Kwa uzoefu wangu, wanasiasa nyemelezi watavitelekeza vyama vyao, hasa baada ya kuahidiwa vinono na CCM. Nani mara hii amesahau akina Masumbuko Lamwai, Tambwe Hiza, Walid Aman Kabourou, Shaib Akwilombe, Salum Msabaha na wengine wengi? Kwanini uone ubaya wa chama baada ya kutimuliwa? Ingawa kuhama vyama ni haki ya wahusika, wengi wa wanasiasa, hasa waliojirejesha CCM baada ya kukosa ukuu kwenye vyama vyao, wameonyesha kuwa nyemelezi na “changudoa.”


  Ukiwaondoa watu kama Wifred Rwakatare na wengine wachache, wengi wamedhihirisha wanavyosaka madaraka badala ya kutumikia umma. Wamejivua nguo hata kama baadhi yao wanapewa madaraka ya kufinyangwa kama ilivyo sasa ofisi ya propaganda ya CCM, ambayo imegeuka dampo la wanasiasa nyemelezi. Hivyo basi, CHADEMA wangembana Zitto wajue msimamo wake kwamba ni nani hasa atamuunga mkono kati ya mgombea wa chama chake na rafiki yake Kafulila.

  Ni heri CHADEMA wakamkosa Zitto mapema kuliko kuwachenga saa za mwisho. Huu si wakati wa kucheza pata potea.

  Bado Zitto ni mdogo kisiasa na kiumri. Ubunge wa kipindi kimoja hauwezi kumfanya awe yote katika yote hadi kuwa maarufu kuliko chama. Na chama kinapozidiwa umaarufu na mtu mmoja, kama CCM, kijue kinaelekea kuzimu. Nisingetaka CHADEMA wafike huko ingawa dalili zinaonyesha ukomavu wa hali ya juu katika kuyakata mawimbi haya na majaribu makubwa.


  Zitto kaamua kumuunga mkono Kafulila wazi wazi, hata kabla ya chama chake kuamua kumsimamisha mgombea Kigoma Kusini. Anajiona si mchezaji bali mwamuzi. Je, alitaka kujenga mtandao ndani ya chama ili baadaye apate madaraka?

  Na ikumbukwe. Hii si mara ya kwanza kwa Kabwe kupimana misuli na chama. Nani amesahau mvutano uliotokea hivi karibuni kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa chama? Je, Kabwe anatingisha kiberiti kwa ajili ya kuchukua uamuzi katika chaguzi

  Archieved: Zitto Kabwe: Kumbikumbi huruka na kuliwa na kunguru | Gazeti la MwanaHalisi
   
 14. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Abrakadabra tupu!
   
 15. k

  kilaki Member

  #15
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 27, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We av so many jembes there,chama c cha zitto wala slaa.tuko fiti kinoma noma.:a s 465:
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Oct 4, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,744
  Likes Received: 12,820
  Trophy Points: 280
  Mmmmmmmh
  Zitto ni cdm, cdm si Zitto-Zitto
   
 17. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #17
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  e
  Yale Yale huku nguvu ya umma huku nguvu ya mabadiliko kazi kweli kweli
   
 18. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #18
  Oct 4, 2012
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  NDOTO ZA MKAKATI WA KI-UTAWALA KWA MTINDO WA KI-CCM-AMOEBA NA MPANGO MZIMA WA DHANA JIPYA LA 'SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA' KURUDISHA WATU CCM WAPENDE WASIPENDE

  Tehe tehe tehe; mbona tuliyafahamu siku nyingi sana tu hat kabla ya chama hicho kuhamia Kijitonyama!!!!!!!!!!

  Na katika hilo namuunga mkono rafiki yangu mkubwa Zitto Zuberi Kabwe kutamani kwake kujijengea ka-mji mpya kujitawalia kwa uhuru zaidi apendavyo HIVYO TUNAMTAKIA KHERI WAKATI WOWOTE atakapochagua kujiunga rasmi huko!

  Mtihani sasa ni kwa Zitto kuthibitishia umma ukweli wa ile kauli yake ya hivi majuzi kwamba HATARAJII JINA LAKE KUINGIA KATIKA HISTORIA KAMA MTU ALIYEKWAMISHA MBADILIKO kutokea nchini kwa kuendeleza juhudi zozote zile za ki-rivesi vile.

  Karibu katika uwanja wa mapambano ya kisiasa kama kiongozi wa CCM-D = CHAUMA ili watu tukaendeleze demokrasia zaidi kwa kuwa hata kwepo mwana-CHAUMA pia ni haki yako mtakakokutania na baadhi ya wna-CCM watakaokoseshwa amani huko mara baada ya CCM kupasuka hapo baadaye kidogo.

  Cha zaidi tunachojua ni kwamba kuna mpango wa kuazima ile DUPLICATE ya CUF na CCM kule Zanzibar nako kuja kutengeneza mdudu unaoitwa SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA TANZANIA BARA nako kwa mara ya kwanza katika historia na hivyo kusaidia KUSHINDA JUHUDI ZA MABADILIKO YA KWELI wanayotaka wananchi hivi sasa.

  Kwa wale waliowahi kuingia huko madarasa ya sayansi, katika mpango huo hapo juu CCM kitajigawa katika familia mbalimbali kama yule MDUDU AMOEBA (ukipenda waweza kukiita sura ya Vyama-CCM vijavyo kama vile CCM-AMOEBA; hapo utakua unamaanisha:

  1.
  CCM-Orijino kile kisichopendwa (mama Asha-Rose Migiro - mgombea wa kuleta suluhu),

  2.
  CCM-KAFU

  (Prof Lipumba mwenye jukumu la kusaka kura za Waislamu, VYOVYOTE WATAVYOJALIWA kote Bara na Visiwani, na kuleta kura hizo kwenye kapuni lile lile,

  3.
  CCM-CHAUMA

  (kiongozi wake '?' mwenye jukumu la kusomba kura za vijana Tanzania Bara na kuzirudisha kura hizo hizo kule kule wasikokupenda kwenye CCM Orijino,

  4.
  CCM-ADC

  (kiongozi wake bado kegesha zake pale KAFU na jukumu lake ni kuleta kura za Pemba kwenye kapu lile lile la CCM-AMOEBA na dhana mpya ya serikali ya umoja wa kitaifa.

  5.
  CCM-UDP

  (kiongozi wake wa maisha, Mhe John Mimose Cheyo mwenye jukumu la kuleta kihalalishio chochote cha kura za kanda ya ziwa kwenye kapu la CCM-AMOEBA pale serikalini.

  Hadi hapa enyi wenzetu wapenda mabadiliko ya kweli yatokanayo kweli na Umma wa Tanzania kuondokana na madhila ya UFISADI ndani ya CCM na Vyama-Matawi yake yote, chaguo lako pekee na la uhakika kukusemea upendavyo ni CHADEMA - period!

  Nimeupenda sana huu mkakati mpya wa CCM uliotengenezwa na baadhi ya Makada wake wanaosomea Sayansi ya Siasa pale Mlimani.

  Huu mpango ambao ni maridhawa kinadharia zaidi, utekelezaji wake hadi hivi sasa ni kila kitu kwa CCM chenye udhaifu uliotukuka ili kujiendelezea ndoto za kuweza kupata uhai mwingine kisiasa nchini muonekano wake wa hivi sasa.

  Lakini mpango huu utaweza kuangukia pua kabisa na kuaibisha wabunifu wake katika hali halisia ya Tanzania ya sasa inayotaka mabadiliko ya kweli bila utani endapo pale tu ambapo CHADEMA kitaweza kuwaelewesha vizuri wananchi juu ya ghiliba hii inayowasubiri hapo baadaye kidogo, basi NADHARIA ITAENDELEA KUBAKIA NADHARIA kule maabara ya wasomi wa mezani na kwa upande mwingine ukweli kujitokeza na kuwaumbua wote hao.

  Pamoja na yote, hiyo
  RANGI NYEKUNDU kwenye bendera ya CCM-CHAUMA tafsiri yake ni nini maana ni rangi isiofahamika kabisa katika medani ya siasa nchini?????
   
 19. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #19
  Oct 4, 2012
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Imetosha sasa mwacheni Zitto ampumzike na kujipanga na harakati zake za kuingia ikulu 2015 kwa tiketi ya CDM!
   
 20. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #20
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  and he is very right!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...