Zitto Kabwe, Halima Mdee na wasanii kibao ndani ya nyimbo ya Sajuki

Kama sikosei Serikali ya JK ilitoa Millioni 10 kwa Dead Body Kanumba, ni matumaini yangu kwa huyu ambaye yuko hai Serikali hii ya JK itatoa hata millioni 20.

Nina hakika Rais wetu ni mtu wa watu huenda hajapewa hizi taarifa na wasaidizi wake, nashauri wamuhi kumueleza kabla hajapanda pipa kwenda kwa Obama kwenye G8 Summit.

Ndio tatizo la sisi Watanzania, mtu akiumwa ukienda kuomba msaada kila mmoja hana pesa, anasubiri afe utasikia ametoa ubani wa tsh 10m ZA NINI? zinamsaidia nini maiti zaidi ya kufurahisha waombolezaji? alikuwa akihitaji msaada wakati anaumwa hukutoa , amekufa kama muislamu anahitahi sanda ya tsh 40,000 , ubao na vya kusafisha maiti ambavyo havizidi hata tsh 100,000 za kitanzania, labda na pesa ya mchimba kaburi kazi yake imeisha.

Ikitokea arusi hapo utaona watu wanatoa michango ya ajabu ..jamni tubadilike sisi wana adamu, watu wanahitaji michango wakati wanaumwa , kwenda shule sio arusi na mtu anapokufa ! ...
 
zinahitajika mil 25 za kibongo, tuchangeni jamani tumuokoe binaadam mwenzetu, mkulu alitoa m 10 na serikali 15 kwa mazishi ya kanumba. huyu mzima anateketea wamekaa kimya

Ndo ajabu ya waswahili wazima hawachangii wanasubiri ufe ndo waanze kujionyesha kwenye rambi rambi si unajua ukimchangia mgonjwa haitangazwi lakini akifa inatangazwa jamaa flani katoa kiasi flani ya sanduku au ubani n.k
 
hilo jina kama na lijua, lakini redio aliyotumia ndiyo siijui, au ndo ile KIBONDE FM niliyoiacha, any way nafikri pesa zitatosha akichangia mkuu.
 
Rais wetu anapenda sana watu (waliokufa)
haishi kwenye misiba!

Watu walio hai anapenda kupiga nao picha tu basi!

Kama sikosei Serikali ya JK ilitoa Millioni 10 kwa Dead Body Kanumba, ni matumaini yangu kwa huyu ambaye yuko hai Serikali hii ya JK itatoa hata millioni 20.

Nina hakika Rais wetu ni mtu wa watu huenda hajapewa hizi taarifa na wasaidizi wake, nashauri wamuhi kumueleza kabla hajapanda pipa kwenda kwa Obama kwenye G8 Summit.
 
Ndo ajabu ya waswahili wazima hawachangii wanasubiri ufe ndo waanze kujionyesha kwenye rambi rambi si unajua ukimchangia mgonjwa haitangazwi lakini akifa inatangazwa jamaa flani katoa kiasi flani ya sanduku au ubani n.k
Mkuu, hii ya kutangaza ubani nimeiona kwa serikali and to be specific nimeiona kwa JK.
Rambirambi haina pledge/au kutamka kwa nguvu kwamba natoa bei hii kama kwenye michango mingine!!
 
nadhan kuna haja sasa ya hizi habari kutangaza ktk media zingne coz hii clouds watu wanaidis nowdays.so ila watu wengi wapate habar basi kuwe na mchanganyo wa media
 
zinahitajika mil 25 za kibongo, tuchangeni jamani tumuokoe binaadam mwenzetu, mkulu alitoa m 10 na serikali 15 kwa mazishi ya kanumba. huyu mzima anateketea wamekaa kimya

Sajuki sio mtu wa mbwembwe na hapendi publicity kama ****** anavyotaka,kwa hiyo hawezi kuguswa kwa namna hiyo,ila nimefarijika sana Watanzania wengi kwa umoja wao wameguswa sana kwa ili,na leo wamechanga vya kutosha,mpaka jumatatu kwa uwezo wa Mungu hela itakua imetimia
 
Hizi siasa jamani!
Hapa Zito na Halima wanatafuta umaarufu kupitia ugonjwa wa mwenzao...dhambi sana.
 
Hizi siasa jamani!
Hapa Zito na Halima wanatafuta umaarufu kupitia ugonjwa wa mwenzao...dhambi sana.

Mkuu u re wrong kwa ilo,hawa watu tayari ni maarufu mno!walichofanya ni kwa kutumia umaarufu wao kutuma ujumbe na kuhamasisha jamihi iweze kuchangia ili kuokoa maisha ya huyu Mtanzania mwenzetu!
 
Back
Top Bottom