Zitto Kabwe, Halima Mdee na wasanii kibao ndani ya nyimbo ya Sajuki

Tunaomba na mzee wa kaya ajititimue hapo kusaidia, kwani itakuwa vizuri zaidi kutoa za matibabu, kuliko ubani kwenye msiba.
 
:clap2: Ishakuwa deal!!!! Tutasikia mengi mwaka huu..... Na sisi tusio na fun wacha tuanze kunyenyua vyuma ili tujazie mwali tuwe ma-bouncer labda watatukumbuka......:painkiller:
 
japo sina mzuka kabisa na muvi za kibongo, lakini angalau nilikuwa natambuwa uwepo wa Stephen Kanumba.

huyu Sajuki ni nani?

maana sasa imekuwa ishu, si FB, si Twitter and now JF.

Sajuki! Sajuki!

Yeye ni nani? na kwa nini anatambulishwa kwa jina moja?

Nenda kaazime mikanda yake uangalie, ni kijana muigizaji mzuri kuliko wale wote unaowajua, Yuko smart sana kuvaa, kuigiza, hata kutoa matamshi, anafikiri kabla ya kusema, Tatizo lililompata anaumwa! sasa hajiwezi, hivyo wanamuwezesha. Mungu ampe nafuu ya haraka.
 
Sajuki Sajuki....hao walioshirikishwa kutoa iyo singo wao wamechangia kiasi gani hayo matibabu...nilitegemea hii ishu ingekua imeshamalizwa siku nyingi twa huto tu milioni 25..au ni kujitaftia umaarufu wa ziada??

soon utaskia na raisi nae anatembeza bakuli..hivi kila mtu akimtembezea bakuli nani atamchangia mwenzie?...

sipingi huyu jamaa kuchangiwa..ila napinga hawa ambao ilibidi wawe wameshazichanga izi hela kuendelea kupiga debe huku wakijisahau?..kw amfano.Dina Marios wa Clouds yeye ametoa bei gani?..au hao waliotunga wiomb wamechanga jumla y abei gani?...tafakari.tuwe responsible sio kuzunguka zunguka
 
Mohammed Shossi na watu wa upande wa pili uwe unawathamini hivi!!

Sawasawa?
 
Watuhakikishie kwanza kwamba hizo hela hazitaliwa kama za Kanumba. Afu mbona huyo tu ndo ameanzishiwa harambee wakati kila siku kuna watu wanaomba misaada ya matibabu kwenye tv?
 
waheshimiwa wabunge wametoa track inayoenda kwa jina la "nimepoteza mboni yangu" kwa ajili ya kuhamasisha kumchangia pesa za matibabu msanii sajuki tune clouds usikilize sauti ya halima mdee.

Unaweza kuchangia kwa kutuma pesa kwenye account number 050000003047 akiba bank jina la mwenye account ni wastara juma jina mke wa sajuki au tuma pesa kupitia mpesa number 0762189592.

wimbo huu ni maalum kwa ndugu yetu msanii sajuki ambae anahitaji mchango wako wako wa hali na mali kuokoa maisha yake.kabla sikupenda kuweka picha yake hapa katika hali aliyonayo sasa ila imebidi ili upate picha kamili.sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni na mwezi huu anahitajika kusafiri kwenda nchini india kwa matibabu.wimbo tuliokuwa tunaurekodi unatoka katika filamu aliyowahi kuifanya na mkwewe ya mboni yangu.na wimbo huu upo ndani ya filamu hiyo aliuimba wastara.wimbo huu tumeurekodi kuhamasishana kuchangia na utaanza kusikika kesho hapa clouds fm na video ya tukio zima la kurekodi itaonekana clouds tv.na kesho tutahakikisha tunakusanya angalau tsh ml 12,000,000 hapa clouds fm.nakuomba sana mtanzania mwenzangu tushirikiane katika hili.

baadhi ya wasanii na waheshimiwa walioshiriki katika "nimepoteza mboni yangu" ni pamoja na wastara mwenyewe na vick kamata, amini, barnaba, peter msechu, madee, rachel, wema sepetu, mzee yusuph, pro jay, afande sele , fid q, chid benz, linex, queen darlin, shilole, ali kiba, william mtitu, ester bulaya, mwanafa, halima mdee, january makamba ,zitto kabwe na khadija.



Tahadhari.

Jihadhari na matapeli....unapotuma mpesa ili kutoa mchango wako wa sajuki hakikisha jina utakaloliona ni la mke wake ambae ni wastara juma.

Kuna mtandao fulani aliokuwa anautumia mwanzo watu walihamisha salio kwa kuiswap namba yake siutaji huo mtandao ila nadhani mmeshauelewa.

waislam bana hayaa
mohamed sajuki
mohamde shoshi
zuberi kwabwe
halima mdee
wastara jumaaaaaa
sasa kina frank,john nao inabidi wamchangie kanumba steven au yule wa zekomed
 
Mkuu ampe lift kwenye ndege yake, amdrop india then aende kwenye G8 summit.
 
Back
Top Bottom