Zitto Kabwe, Halima Mdee na wasanii kibao ndani ya nyimbo ya Sajuki

Mohammed Hamad

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
3,988
1,304
Waheshimiwa wabunge wametoa track inayoenda kwa jina la "nimepoteza mboni yangu" kwa ajili ya kuhamasisha kumchangia pesa za matibabu msanii sajuki tune clouds usikilize sauti ya Halima Mdee.

Unaweza kuchangia kwa kutuma pesa kwenye account number 050000003047 AKIBA BANK jina la mwenye account ni Wastara Juma jina mke wa Sajuki au tuma pesa kupitia MPESA number 0762189592.

Wimbo huu ni maalum kwa ndugu yetu msanii Sajuki ambae anahitaji mchango wako wako wa hali na mali kuokoa maisha yake.Kabla sikupenda kuweka picha yake hapa katika hali aliyonayo sasa ila imebidi ili upate picha kamili.Sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni na mwezi huu anahitajika kusafiri kwenda nchini India kwa matibabu.Wimbo tuliokuwa tunaurekodi unatoka katika filamu aliyowahi kuifanya na mkwewe ya MBONI YANGU.Na wimbo huu upo ndani ya filamu hiyo aliuimba Wastara.Wimbo huu tumeurekodi kuhamasishana kuchangia na utaanza kusikika kesho hapa clouds fm na video ya tukio zima la kurekodi itaonekana clouds tv.Na kesho tutahakikisha tunakusanya angalau Tsh ml 12,000,000 hapa clouds fm.Nakuomba sana mtanzania mwenzangu tushirikiane katika hili.

Baadhi ya wasanii na waheshimiwa walioshiriki katika "nimepoteza mboni yangu" ni pamoja na Wastara mwenyewe na vick kamata, Amini, Barnaba, Peter Msechu, Madee, Rachel, Wema Sepetu, Mzee Yusuph, Pro Jay, Afande Sele , Fid Q, Chid Benz, Linex, Queen Darlin, Shilole, Ali Kiba, William Mtitu, Ester Bulaya, MwanaFA, Halima Mdee, January Makamba ,Zitto Kabwe na Khadija.

Tahadhari.

JIHADHARI NA MATAPELI....unapotuma MPESA ili kutoa mchango wako wa SAJUKI hakikisha jina utakaloliona ni la mke wake ambae ni WASTARA JUMA.

Kuna mtandao fulani aliokuwa anautumia mwanzo watu walihamisha salio kwa kuiswap namba yake siutaji huo mtandao ila nadhani mmeshauelewa.
 
Attachments

  • sajuk[1].jpg
    sajuk[1].jpg
    19.3 KB · Views: 391
  • Sajuki.jpg
    Sajuki.jpg
    44.1 KB · Views: 353
Very gud. Na jana masanja wa komedi alihamasisha uchangiaji wa fedha ili sajuki akatibiwe india. Alifanya kupitia komedi yao ya TBC.
 
Waheshimiwa wabunge wametoa track inayoenda kwa jina la "nimepoteza mboni yangu" kwa ajili ya kuhamasisha kumchangia pesa za matibabu msanii sajuki tune clouds usikilize sauti ya Halima Mdee.

Unaweza kuchangia kwa kutuma pesa kwenye account number 050000003047 AKIBA BANK jina la mwenye account ni Wastara Juma jina mke wa Sajuki au tuma pesa kupitia MPESA number 0762189592.

japo sina mzuka kabisa na muvi za kibongo, lakini angalau nilikuwa natambuwa uwepo wa Stephen Kanumba.

huyu Sajuki ni nani?

maana sasa imekuwa ishu, si FB, si Twitter and now JF.

Sajuki! Sajuki!

Yeye ni nani? na kwa nini anatambulishwa kwa jina moja?
 
Huwezi kumjua kwasababu Sajuki hakuwa na mbwembwe sana. Nadhani hata Mzee Kipara au Fundi Saidi humjui wala huwahi kumjua kwakuwa hakupewa publicity.
 
wana JF watakwambia hawasikilizi hiyo radio! "wivu"

Nyimbo nzuri sana .. BIG UP
 
zinahitajika mil 25 za kibongo, tuchangeni jamani tumuokoe binaadam mwenzetu, mkulu alitoa m 10 na serikali 15 kwa mazishi ya kanumba. huyu mzima anateketea wamekaa kimya
 
Huwezi kumjua kwasababu Sajuki hakuwa na mbwembwe sana. Nadhani hata Mzee Kipara au Fundi Saidi humjui wala huwahi kumjua kwakuwa hakupewa publicity.

ndo nataka nimjuwe sasa ili hata ukiniambia kumchangia matibabu nifanye hivyo bila mawaa.
 
Kama sikosei Serikali ya JK ilitoa Millioni 10 kwa Dead Body Kanumba, ni matumaini yangu kwa huyu ambaye yuko hai Serikali hii ya JK itatoa hata millioni 20.

Nina hakika Rais wetu ni mtu wa watu huenda hajapewa hizi taarifa na wasaidizi wake, nashauri wamuhi kumueleza kabla hajapanda pipa kwenda kwa Obama kwenye G8 Summit.
 
imetumika nguvu kubwa sana kuchangisha hizo fedha. Hii inaleta picha kuwa pamoja na wingi wa wasanii waliopo bado ushirikiano hafifu
 
zinahitajika mil 25 za kibongo, tuchangeni jamani tumuokoe binaadam mwenzetu, mkulu alitoa m 10 na serikali 15 kwa mazishi ya kanumba. huyu mzima anateketea wamekaa kimya

kweli ndugu yangu tatizo tumezowea kuchangia wafu, kuliko walio hai. JAMANI OKENI UHAI WA MTU, HAITAKUWA NA MAANA KUTUMIA MILIONI 60 KWA MAZISHI WAKATI MTU ALIHITAJI ML 25 TU KUTIBIWA.
ASANTE SANA NDUGU
 
Back
Top Bottom