Zitto Kabwe: Bila UKAWA CCM haing'oki

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,502
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), amesema kuwa mwanasiasa yeyote makini kutoka vyama vya upinzani mwenye dhamira ya kuiondosha madarakani Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hawezi kukwepa kufanya kazi na muungano wa vyama vinavyounda kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Zitto anasema kuwa hata vyama vichanga vinavyokua kama ACT-Tanzania na vingine, vina nafasi ya kuingia katika umoja huo ili kuzidisha nguvu ya upinzani kuing'oa CCM kwa maslahi ya nchi na wananchi.

Mwanasiasa huyo, alitoa kauli hiyo katika mahojiano maalum na gazeti hili, yaliyofanyika juzi nyumbani kwake jijini Dar es Salaam juu ya masuala mbali mbali ya kijamii na kisiasa, huku akieleza namna UKAWA wanavyoweza kufanikisha ushindi wa kuing'oa CCM.

Zitto alisema kuwa, uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Disemba 14 mwaka huu, uchukuliwe kama sehemu ya kujifunza makosa yatakayofanyiwa kazi kuelekea katika ushindi wa mwaka 2015.

"Nimefurahi kukutana na wenzangu wa CHADEMA wakati wa mashauriano juu ya maazimio ya kamati ya PAC, nimekulia CHADEMA…nimefanya kazi CHADEMA, wapo niliowalea kisiasa, wapo niliowapokea kina Silinde, Lyimo na wengine, hivyo kukutana nao kwa pamoja baada ya mtafuruku ulioanza Disemba 22 mwaka jana, kumenipa faraja sana na sioni shida kufanya kazi na UKAWA kwa maslahi ya nchi,"alisema Zitto.

Alisema tofauti yake na chama chake haiwezi kumzuia kufanya kazi na UKAWA na kwamba hata kukutana kwao katika kujadili maazimio ya kamati ya Bunge kwa ajili ya kuwachukulia hatua watuhumiwa wa kashfa ya Escrow, ulikuwa mpango wa Mungu.

Kwa mujibu wa Zitto, ili UKAWA waweze kushinda katika uchaguzi ujao ni vema viongozi pasipo kujali maslahi binafsi, wakajiwekea malengo ya idadi ya viti vya ubunge watakavyopigania kwa nguvu zote wakiwa katika mgawanyo watakaokubaliana.

"Katika hili la ushindi kwa upinzani ndani ya muunagano ni dhahiri hauna mjadala, cha muhimu ni kukubaliana kwa mfano kuwa wanataka wabunge wangapi watakaowapigania kwa pamoja na hapa wasipungue 150 kwa mgawanyo utakaokubalika; mfano Zanzibar, CUF wasimamishe wagombea katika majimbo yote na bara wapate katika baadhi ya maeneo wanayokubalika," alisema na kuongeza;

"CHADEMA NCCR-Mageuzi na ACT-Tanzania waweke wagombea kwa upande wa bara katika maeneo wanayokubalika na kila mgombea apiganiwe kwa nguvu zote katika eneo analokubalika dhidi ya mgombea wa CCM,"alisema Zitto.

Alisema vyama hivyo kwa umoja wao vikiwa na uhakika wa kupata wabunge 150, wasiokuwa na ushindani kutoka CCM, wanaweza kugombania majimbo mengine kwa ajili ya kuongeza idadi ya wabunge kwa lengo la kupata serikali yenye nguvu zaidi.

Kuhusu kutafuta maridhiano ndani ya CHADEMA, Zitto alisema maridhiano ya aina yoyote yatakayofanywa yanapaswa kuwashirikisha watu wote walioumizwa na shutuma alizopewa.

"Nimesamehe kila aina ya matusi niliyofanyiwa lakini mambo mawili sitoweza kuyaacha, moja ni kutaka shutuma kuwa ninatumiwa na CCM kwa ajili ya usaliti ithibitishwe na kama haupo waliotunga uongo huo wawajibishwe kwa kuwa hii pasipo kuthibitishwa kwa tuhuma hizo za usaliti, kutamuathiri hata mwanangu na kizazi change,"alisema Zitto.

Alisema yupo tayari kuwajibika kwa yale atakayoyafanya kuliko kuvumilia baadhi ya mambo yasiyokuwa na maslahi kwa Umma.


CHANZO: Tanzania Daima
 
Niliahawahi kusema, Uzuri wa siasa za Tanzania, hawa wote wanaojenga hoja na vioja mpaka wengine wakiumiza vidole kwa sababu ya typing kwenye keyboard/keypad huku wakiandika na kusema hawataki Mhe. Zitto arudi CHADEMA, lakini ndiyo hawa hawa ambao kesho kama Mhe. Mbowe au Dkt. Slaa wakisema tunamrudisha Mhe. Zitto kwenye kundi la CHADEMA, utawasikia tena wakisema, siasa hazina marafiki au maadui wa kudumu.

Siasa za Tanzania ni vichekesho vitupu!.

Ndiyo maana kuna hoja zinasema, siasa za Tanzania zimejaa misukule!

Ni huyu huyu Mhe. Zitto baada ya vyama kuamua kushirikiana alibeza na kusema wasanga tonge kwa sababu wanaungana kwa lengo la kugawana madaraka badala ya kuungana katika mlengo wa kiitikadi, kifalsafa na kisera.

Leo hii huyu huyu anaongelea jinsi ya kugawana majimbo kwa ajili ya kupata ushindi.

Kwa jinsi wanasiasa walivyo kama vinyonga, hata ukimwendea na kumuuliza kuhusu kauli zake za nyuma, hawezi kukosa jibu!

Baadhi ya watanzania wataendelea kuyumbishwa sana na wanasiasa hasa ukichukulia kuwa, siasa za Tanzania ziko based on personality badala ya Institutional.

Mwanasiasa akihamisha magoli, wafuasi wake wanabaki kuweweseka kwa sababu hawafahamu sehemu atakayoweka magoli.

Kuna baadhi ya watu katika upande wa CHADEMA na wale wa upande wa Mhe. Zitto kwa sasa wanaweweseka kutokana na statements za Mhe. Zitto ambazo zimeanza kubadilika kila siku. Hawafahamu msingi wa hoja zake na matokeo ya hoja zake.

Ama kweli siasa za Tanzania siyo za wapita njia!

Wahenga walisema, mavi ya zamani hayanuki!

attachment.php
 
Huwa unanishangaza sana napoona mtu ambaye anajua kabisa udhaifu wa kiongozi au kundi fulani na anajua kabisa uzuri wa kiongozi mwingine then anaamua kabisa kujitoa fahamu na kutetea udhaifu.

Kuna kazi kubwa kuwatoa au kuwapunguza walaji bila kufanya kazi huko madarakani.
Mungu atusimamie
 
Aliyoongea ni kweli tupu. Ila nina wasiwasi na huo umoja wao UKAWA kama utadumu.
 
Mungu akurinde zitto na mama yako mungu amuweke mahali njema peponi.wakilisha mkuu.welcome to home ukawa like mother like sun. Don't worry and don't give up.


Swissme.
 
Bila kuweka ushabiki,ZZK kaongea ukweli mtupu,hakuna aliye mkamilifu hapa duniani jamani.Nina miss sana harakati za Chadema ikiwa na Zitto.Kutofautiana kupo tu katika Maisha yetu kwa sababu sisi ni binadamu.
Cha msingi ni kusahau yaliyopita na kuganga yajao,visasi chuki na husuda kamwe si misingi ya ungwana.
 
Kwa nini zitto anakazia Act iungane na ukawa? Kwa nini asitaje Udp? Hapo kuna jambo! Zitto wakati mwingine hapimi maneno yake na athari zake! Nilipenda sana zitto arudi rasmi chadema lakini mmmh!
 
Kwa muda mfupi nimejifunza somo moja kuhusu ukawa nayo ni kwamba CHADEMA ndiyo ukawa wengine ndani ya ukawa LAZIMA WAFUATE CHADEMA vunginevyo unakuwa msaliti wa ukawa.
 
Asante sana Zitto , Wewe usijali karibu tena nyumbani na hapa hakuna mwenye chuki. Kwani mpaka gazeti la TANZANIA DAIMA limechukua hatua ya kukufata kwako na kukuhoji basi tuna imani lipo jambo jema mbele linakuja.

Peoples..........
 
Last edited by a moderator:
Kwa nini zitto anakazia Act iungane na ukawa? Kwa nini asitaje Udp? Hapo kuna jambo! Zitto wakati mwingine hapimi maneno yake na athari zake! Nilipenda sana zitto arudi rasmi chadema lakini mmmh!

Hakya Mungu kuna watu mapaka kweli hapa duniani, yani wewe katika hoja zote hujaona hata jema moja we unatafuta pungufu ni lipi, ngoja nikuulize hivi kama CHADEMA imeungana na CUF itashindwa vipi kuungana na ACT? Japokuwa siwapendi hawa jamaa wa ACT lakini sijaona ubaya wa hoja ya Zitto.
 
Hata waungane na wanyama wakali kama simba, ccm lazima iwachezeshe kwata
 
Kwa nini zitto anakazia Act iungane na ukawa? Kwa nini asitaje Udp? Hapo kuna jambo! Zitto wakati mwingine hapimi maneno yake na athari zake! Nilipenda sana zitto arudi rasmi chadema lakini mmmh!
Baada ya machadema kumfanyia majungu ulitaka afanyeje? Wewe ni zuzu. Chadema sio mama wa watu wala sio last resort
 
Back
Top Bottom