Zitto Kabwe: Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa ambayo hamjawahi kuyaona, tusipoteze hii fursa jamani

Hivi ni kwanini hawa wanaoonesha uhitaji na hii bandari hawajikiti kufafanua jinsi gani ulivyo mkataba? Hapa hakuna anayekataa sijui ukubwa wa meli mara ukubwa wa kiwanja cha mpira mara tatu. Hapa tunahitaji hoja za msingi juu ya content ya mkataba wenyewe na si vingine.
 
Zitto huwaga mpiga debe wa mabeberu tu hata sinshangai, hii meli kubwa kiasi gani istue dar? Muongo sana huyo. Na yeye kaiona wapi?
Huko ndio kudanganywa kisomi,with grace and penetration unsurpassed. Tanzania oyee
 
Bado unakuwa mgumu kuelewa, miradi mingi muda wa kurudisha pesa ni miaka 8 au chini ya hapo.
Jingine kwanini tusi chukue mkopo wa hiyo 10bn tukajenga wenyewe. Na tulipe hilo deni sisi wenyewe kwa kuendesha huo mradi.
Au wao nani atakuwa anahakikisha kuwa wamewekwa hizo 10bn, na pia kama hawajapata Mapato ya kuzidi 10bn kwa muda mfupi zaidi
Je umesikia kuhusu port ya Sri Lanka ambayo imeshindwa kurejesha deni kwa wachoma.
Hilo la kuchukua mkopo na kujenga wenyewe lina risk kubwa mno! Huwezi kurudisha investment ya dola bil 10 kwa miaka 8. Hilo linawezekana kwenye mitambo siyo miundo mbinu ya bandari. Tunaweza kuangalia best practice na kunegotiate.

Kuhusu kuendesha wenyewe,sina uhakika kama tunaweza! Bandari ya Dar ilitushinda kuendesha. Kwa sasa,wanaoendesha ni TICTS siyo serikali.
 
Hatutaki Wachina watujengee barabara, madaraja, viwanja na mabomba. Ni aibu kubwa na ujinga kushangalia wachina wakichukua tenda za ujenzi kwenye nchi yako usijue ni hasara kwa kampuni za wazawa.

Kama wachina wangekuwa ni rafiki au ndugu zetu wangetupa hiyo mikopo tujenge kwa kampuni zetu za ndani. Hawa wachina na mabeberu kama mabeberu wengine.

Badala ya kuchukua tenda za ujenzi tu, wawekeze katika viwanda vikubwa ili watoe ajira za kudumu, ujuzi na walipe kodi sio kuchota tu kodi zetu kwenye ujenzi.
Ni mambo ya kushangaza kabisa!

Wachina wamekuwa na sisi kama marafiki kwa muda mrefu tangu tupate uhuru. Wamejenga miradi mingi kwa mikopo,mingine hatujamaliza hata kuwalipa kama Tazara na Urafiki. Lakini pia wao ndio wametujengea uwanja wa kisasa wa Mkapa na ukumbi wa mikutano wa kisasa wa Julius Nyerere.

Hata huu mradi wa bomba la mafuta uliosainiwa juzi, wachina wanamiliki hisa nyingi tu.
 
Hilo la kuchukua mkopo na kujenga wenyewe lina risk kubwa mno! Huwezi kurudisha investment ya dola bil 10 kwa miaka 8. Hilo linawezekana kwenye mitambo siyo miundo mbinu ya bandari. Tunaweza kuangalia best practice na kunegotiate.

Kuhusu kuendesha wenyewe,sina uhakika kama tunaweza! Bandari ya Dar ilitushinda kuendesha. Kwa sasa,wanaoendesha ni TICTS siyo serikali.
Hili la ticts ni watu wamepeana tu ulaji, kwanza mkataba ulikuwa use wa miaka 10 , halafu kuna watu wakaongezea tena hadi miaka 25 , ni sawa na hi miradi ya icd, Richie, ya jengo la umoja wa vijana, uwt na kuendelea.
Hivyo unatakiwa kulielewa hilo
 
Sio kila uwekezaji ni wa kushangilia. Nchi yetu inahitaji uwekezaji wa viwanda vikubwa sio kujengewea tu barabara na flyovers ambapo wanachukua kodi zetu huku kampuni za wazawa wakikosa kufaidi fursa za nchi zao na kuzidi kudumaa.
Huna taarifa za kutosha kuhusu wachina.

China ndio wawekezaji wakubwa sasa hivi duniani kwa sababu ya ukwasi wao. China wana mapesa mengi mno ya kuwekeza!

Hata mradi wa bomba uliosainiwa juzi kule Uganda,wachina wanamiliki hisa nyingi tu kukaribia zile za wafaransa.
 
Hakuna mkataba wowote wataonyesha ndio maana wanazidisha mapambio na miluzi ili kuwachanganya raia.
Hivi ni kwanini hawa wanaoonesha uhitaji na hii bandari hawajikiti kufafanua jinsi gani ulivyo mkataba? Hapa hakuna anayekataa sijui ukubwa wa meli mara ukubwa wa kiwanja cha mpira mara tatu. Hapa tunahitaji hoja za msingi juu ya content ya mkataba wenyewe na si vingine.
 
KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania

Kisha hizi meli tunazoziona zikileta mizigo Dar port ndio zitakuwa zinabeba miizigo kutoka Bagamoyo na kusambaza sehemu mbalimbali duniani amesisitiza Zitto

Tusiiache fursa hii jamani na siyo kweli kwamba kila mradi ulioanzishwa awamu ya Kikwete ulikuwa mbaya kwani hata reli ya SGR mradi uliasisiwa vizuri na serikali ya JK lakini serikali ya awamu ya tano imekuja kuutekeleza kwa namna tofauti, amemalizia Zitto.

Chanzo: Clouds 360
ZITO WATANZANIA SIO WAPUUZI KIASI CHA KUKUBALI UJINGA WENU
 
Mzee wa kurukia hoja.
 
Sijui kwa nini tu huyu jamaa huwa siamini ayasemayo....
Siyo wewe tu. Jamaa ni mtata fulani hivi halafu mjanja janja wa mjini. Ni mtu mwenye underground movements sana. Kuhusu hii bandari: Msione inapigiwa debe namna hii mdhani watu wana uchungu na maendeleo. Kuna watu wameahidiwa mambo makubwa sana huu mradi ukipita. Ngungai alishawekwa sawa ila Magufuli ndiyo alikuwa kikwazo. Sioni wa kuzuia tena sasa hivi kwa sababu wachina wamedhamiria kwani ina faida kubwa kwao.
 
Hatutaki Wachina watujengee barabara, madaraja, viwanja na mabomba. Ni aibu kubwa na ujinga kushangalia wachina wakichukua tenda za ujenzi kwenye nchi yako usijue ni hasara kwa kampuni za wazawa.

Kama wachina wangekuwa ni rafiki au ndugu zetu wangetupa hiyo mikopo tujenge kwa kampuni zetu za ndani. Hawa wachina na mabeberu kama mabeberu wengine.

Badala ya kuchukua tenda za ujenzi tu, wawekeze katika viwanda vikubwa ili watoe ajira za kudumu, ujuzi na walipe kodi sio kuchota tu kodi zetu kwenye ujenzi.
Uko sahihi, wachina watusaidie kwa kuwekeza kwenye viwanda. Bahati nzuri,wamewekeza kwenye viwanda vingi tu hivi karibuni. Naomba nivitaje ninavyo vifahamu:

Kiwanda cha vigae cha GoodOne, Kisarawe.
Kiwanda cha vigae cha twyfold, Chalinze.
Kiwanda cha Dangote. Mtwara
Hivi ni viwanda vikubwa sana ambavyo vinahudumia soko la ndani na la nje. Najua kuna viwanda vingine vingi tu ambavyo wachina wamewekeza. Tusiwabeze. Tuwe objective!
 
Kwanza kasema mradi haukuwa unatekelezwa na china peke yake bali ilikuwa china na oman na ile mizigo haikuwa kwa ajili ya tz pekee bali ilikuwa ni kama kituo ambapo meli kubwa zaidi zinateremsha mizigo halafu hizi meli tulizozea zinaichukua pake na kuisambaza sehemu nyingine za Afrika na dunia.
Amesema ingemaliza ndiyo ingekuwa bandari ya 3 kwa ukubwa duniani. Shida kasema mkataba hata yeye hakuwahi kuona ikulu haikuwahi kuuweka wazi ila angetamani wauweke wazi ujadiliwe zaidi ya kutuambia kama tulivyosikia tu
Sasa hapo ndipo utata unazidi. China na Oman? Hii ni combination ya hatari sana sana.
 
Shida waweke mkataba maana hata wabunge hawakuwahi kuuona hivyo haya yanayosemwa tumesikia tu kutoka kwa mwendazake
Ndungai alisema alikwenda China akaonyeshwa eti presentation akahitimisha ni uwekezaji mzuri. Hivi uwekezeaji mzuri hujulikana kwenye presentation? Uzuri wa uwekezaji uko kwenye mkataba. Huu mradi ni China na Oman wanashirikiana. Hawa ni vinara wa kugawa rushwa duniani. Nina uhakika wengi wanaopigia debe huu mradi wameahidiwa kitu. Jaribu kuangalia aina ya watu wanaopigania huu mradi na tabia zao.
 
KC wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema kitu ambacho wabunge wengi hawakijui ni kwamba Bandari ya Bagamoyo itapokea mameli makubwa makubwa kutoka huko duniani ambazo hatujawahi kuziona hapa Tanzania

Kisha hizi meli tunazoziona zikileta mizigo Dar port ndio zitakuwa zinabeba miizigo kutoka Bagamoyo na kusambaza sehemu mbalimbali duniani amesisitiza Zitto

Tusiiache fursa hii jamani na siyo kweli kwamba kila mradi ulioanzishwa awamu ya Kikwete ulikuwa mbaya kwani hata reli ya SGR mradi uliasisiwa vizuri na serikali ya JK lakini serikali ya awamu ya tano imekuja kuutekeleza kwa namna tofauti, amemalizia Zitto.

Chanzo: Clouds 360
Kwa mkataba hapana labda ubadilishwe na uwe win/win situation

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
 
Tatizo lenu hamtaki kusikiliza!

Mngekuwa mnasikiliza hoja na kizipima badala ya kupinga tu kwa kuwa mtoa hoja humpendi.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo,ulikuwa ujengwe kwa makubaliano ya uwekezaji wa pande tatu,Tanzania,Oman na China. Wawekezaji wangejenga miundo mbinu ya bandari na industrial parks kwa ajili ya viwanda zaidi ya 800 na kuchukua port charges kwa kipindi cha miaka 50. Serikali haikuyakiwa kutoa hata sumuni! Katika kipindi hicho serikali itachukua kodi zingine mbalimbali kama ushauri wa forodha kama kawaida. Baada ya miaka hiyo, bandari inakuwa mali ya serikali 100%

Utaratibu huu ndio unaotumika hata sasa kwenye bandari ya Dar. Wapo TICTS wanaendesha bandari hiyo.

Mradi wa Bandari ya Bagamoyo unamanufaa makubwa katika uchumi wa Tanzania. Pamoja na kuifanya Tanzania kuwa lango juu la bidhaa kwa zaidi ya nchi 8 za Afrika,unaifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda vya kisasa ambavyo vitahudumia soko la ndani na nchi nyingine za Afrika.

Mradi huu utazalisha ajira nyingi mno katika sekta mbalimbali kama mahoteli, usafirishaji nk.
Unanikumbusha Tulivyoandamana udsm enzi izo tukipinga mkataba wa miaka 50 wa mlimani city na ndugu yetu Adong Odwaa alierudishwa kwao Uganda...tulipewa stories km hizi ila uliza udsm inapata how much kwa mwaka, unaweza kutoa chozi...ila siku zote ukweli unatabia ya ku surface ht km utachelewa...sema ndo hua unatoka while madhara yashajitokeza na hakuna namna inabidi tu mvumilie maumivu...
Haya mambo ya mwekezaji ana collect kila kitu then anatoa gawiwo itamfanya mwekezaji kila mwaka ana diclear loss or small profit ili atoe gawiwo kubwa...
SGR ya kenya mpaka leo mwaka wa 4 ina make loss kutokana na uendeshaji wa kichina..
Kifupi chinese are the colonizers...be aware
 
Back
Top Bottom