Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,279
- 25,852
Mara tu baada ya mgogoro wa kufutwa kwa uchaguzi wa Zanzibar kuibuka, Zitto Kabwe kama Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo alisema hivi:
Kimsingi, Zitto alimtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli kutangaza hali ya hatari Visiwani Zanzibar kama muafaka juu ya kurudiwa kwa uchaguzi au kutangazwa kwa mshindi kupatikana. Pia, Zitto alizitaka mamlaka zinazohusika na suala hilo kumtangaza mshindi wa Urais Zanzibar na mshindi huyo kuunda Serikali.
Jana, imeripotiwa humu JF (nimesoma tu humu) kuwa Zitto amesema kuwa ACT-Wazalendo ipo tayari kushiriki uchaguzi wa marudio huko Zanzibar. Iko wazi kuwa muafaka bado haujafikiwa huko Zanzibar. Wakati CCM wakitaka uchaguzi urudiwe, CUF wanataka mshindi atangazwe.
Kama muafaka bado haujapatikana, kwanini Zitto hakuendelea kuusimamia msimamo wake wa kutangazwa hali ya hatari au kutangazwa mshindi na badala yake ameonyesha utayari wa kushiriki ushaguzi wa marudio ambao ni msimamo wa CCM pekee hadi sasa? Kwanini umebadilika? (kama ilivyoripotiwa humu JF ni kweli)