Zitto Kabwe awa mbogo, awashukia vikali wanaodai Makamu wa Rais, Dkt. Mpango ni Mrundi

tracebongo

JF-Expert Member
Nov 18, 2018
1,762
2,000
Hoja ya Uraia ni yakisheria siyo yakisiasa. Kwa mujibu wa sheria ya Uraia wa Tanzania Sura 258 kifungu Cha 4 raia wa Tanzania kwa kuzaliwa ni mtu aliyezaliwa ndani ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania mmoja wa wazazi wake akiwa Raia wa Tanzania. Kwa kifungu hiki Dr. Mpango hana utata wa Uraia kwa sababu zifuatazo
Halafu ile siyo ngoma ya Kirundi, ile ni ngoma ya Kiha na pale ni Manyovu wakati wa kampeni ya ubunge 2020.

Wale ndiyo waha and now wameishika nchi so tukae kwa kutulia.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,269
2,000
Zitto enzi za Jk alitumika vilivyo kuvuruga Upinzania, Bahati Mbaya awamu ya JPM wakawa hawamtumii tena kipindi cha JPM CCM waliingia wenyewe front line kuvuruga Upinzano na hata Zitto alivurugwa sana enzi za JPM...
Tatizo kubwa la Zitto ni kukosana na Mbowe halafu bado anadunda kwenye siasa.

Wote waliokosana na Mbowe wamekwisha kisiasa. Zitto alifukuzwa CHADEMA lakini wanaCHADEMA kutwa kucha wanataka kumpangia maisha yake.

Chuki gunia waliyonayo wanaCHADEMA kwa Zitto ni sawa na Chuki nzito ya wanna CCM kwa Tundu Lissu. Wamebakiza Risasi 36 tu.

Lundo la wabunge wa CHADEMA wamehamia CCM, tena vigogo haswa wa vyama kina Dr. Slaa, Mashinji, Katambi, etc lakini sioni chuki kama hii.

Leo Peter Msigwa mwenye undugu na Magufuli yeye anaaminika na CHADEMA kwasababu hajakosana na Mbowe. Yeye hatumiki wala havujishi siri, ila Zitto.

Mtu aliyetumia nguvu kubwa kutuaminisha Zitto ni msaliti, Kubenea leo yuko ACT huko huko na Zitto!!!

Hivi ni lini ninyi misukule wa CHADEMA mtakuwa na akili timamu?

Cult leadership. Tofauti kubwa ikiyopo Kati ya Mbowe na Magufuli ni ukubwa wa madaraka waliyoshika.

Hata Mbowe kaumiza watu wengi sana huku wafuasi wake wakimwona ni mungu mtu asiye na doa.
 

tracebongo

JF-Expert Member
Nov 18, 2018
1,762
2,000
Sijui nini kimetokea
Ila wamasai hawaukani umasai wao
Na wajaluo hawakani ujaluo wao.
Je Mpango anakiri yeye mhutu/mrundi aliezaliwa Tanzania??
We mxe.ge unawajua Waha au unaropoka?

Lini VP amekwambia ni Mrundi? Kwahiyo kwenye ile video alikuwa anawaomba kura warundi!!??? Amakweli siku hizi JF imejaa wapu.mbavu.

Nawaambia sasahivi Kigoma kama Chato, wana VP na wana Katibu Mkuu Kiongozi.
 

tracebongo

JF-Expert Member
Nov 18, 2018
1,762
2,000
Kigoma mungu atupe nini jamani!! Toka uhuru kigoma tulikuwa hatujawahi kupata kiongozi wa ngazi za juu kama leo Dr philipo Mpango ni VP wenye kukelwa endeleeni kukelwa mpaka mpasuka.
Na bado Katibu Mkuu Kiongozi Kigoma pia.
 

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
42,906
2,000
JF, siku hizi ndiyo maana wakongwe wanachugulia na kuondoka bila kuchangia chochote, uzi kama huu kweli utapata wapi watu makini wa kuchangia labda wazee wa mipasho.
 

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
6,401
2,000
Jana nilimuona Abdul Nondo akiongea kwenye media kwa mtindo wa "kufoka foka" huku dada aliyekuwa pembeni akimuangalia kwa mshangao.

Drama za wanasiasa njaa wa enzi za JK zimeanza kurudi kwa mbali!
 

tracebongo

JF-Expert Member
Nov 18, 2018
1,762
2,000
Kwani waha na warundi matamshi yao yanaingiliana au wana vinasaba vinavyoshabihiana, kumbe ndo maana waha ni wabishi sana wakiungana na wale nshomile sisi watani zao wa huku Musoma inabidi tutumie panga kumaliza ubishi....
Waha, Warundi, Wanyarwanda na Wahangaza wanazungumza lugha moja japo kuna tofauti kidogo sana kwenye baadhi ya maneno/matamshi so nawashangaa wanaoshangaa nyimbo zile zilizoimbwa mbele ya VP mpya na wakumbuke kilikuwa kipindi cha kampeni so wale ndo wapiga kura wake na pale ndo kwao.

Waha ni Waha, Warundi siyo kabila ni taifa na wana makabila yao huko so tumuache VP apige kazi lasivyo Waha wataingia mtaani kumpigania mtu wao.

NB: Katibu mkuu kiongozi pia mtu wa Kigoma
 

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
9,928
2,000
Zitto enzi za Jk alitumika vilivyo kuvuruga Upinzania, Bahati Mbaya awamu ya JPM wakawa hawamtumii tena kipindi cha JPM CCM waliingia wenyewe front line kuvuruga Upinzano na hata Zitto alivurugwa sana enzi za JPM...
Zitto sio mnafiki, yeye anapenda haki ifanywe na yeyote yeye ataipenda. Nyinyi ndio wenye matatizo kwani haki au jambo jema likifanywa na mpinzani wako au CCM mnaona halistahili kupongezwa na likipongezwa basi mnanamuona mpongezaji ni adui wa upinzani wenu, hizo ni siasa za maji takataka ndani ya kata ya msata na hazina nafasi katika siasa za kisasa.

Mnyonge mnyongeni bila kumuua lakini stahili zake apewe.
 

tracebongo

JF-Expert Member
Nov 18, 2018
1,762
2,000
Kigogo angekuwa known ingependeza zaidi ili awe liable anapothibitika kumchafua mtu, lakini kujificha kwa fake ID halafu unaropoka ropoka sio fair, Dr. Mpango h...
Alafu sasa wale siyo warundi na kila siyo kirundi. Tatizo ni watu kutokuwa na taarifa za kutosha. Kile ni Kiha na wale ni waha, pale walikuwa katika kampeni za 2020. Wenye lugha yetu tunawashangaa.
 

Payrol

JF-Expert Member
Feb 17, 2018
2,197
2,000
Zito anaweza akawa na hoja kwenye kumlinda Mpango, lakini asitumie ukigoma kumlinda Mpango,
Wanahoji uraia wa Dk Mpango hawahoji kwa ajili ya kigoma. Wanahoji kwa ajili ya Taifa. Yaani Zito anaanza kukopi kwa JPM alivyoliharibu Taifa kwa kutengeneza ukanda. Magufuli alikua akiiangalia Chato zaidi kuliko kuiangalia Tanzania. Je, kwa hoja ya Zito kusema sisi wakigoma tutamlinda Mpango, maana yake Mpango yupo kwa ajili ya kigoma na sio Tanzania. Ngoja tufanye Raisi aiangalie tu Zanzibar na makamu aiangalie Kigoma kinachofuata ni nini?
Kauli ya Zito ni mbaya sana maana inaleta ukabila
 

sem2708

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,639
2,000
Zitto enzi za Jk alitumika vilivyo kuvuruga Upinzania, Bahati Mbaya awamu ya JPM wakawa hawamtumii tena kipindi cha JPM CCM waliingia wenyewe front line kuvuruga Upinzano na hata Zitto alivurugwa sana enzi za JPM.

Ila kwa mbaali naanza kuona Zitto akirudia kazi yake sasa ya Zamani ya kutumika vilivyo kuvuruga Upinzani, huyu jamaa kwa walio karibi naye wanamjua vilivyo alivyo kwanza Mbinafisi sana na mpenda sifa.

Awamu hii ya 6 ameisha anza kujikomba vilivyo kwa watawala wapya, hii alIifanya sana enzi za JK.

Ukizingatia kwamba yuko Juu ya Mawe awamu hii ya 6 lazima awavutuge vilivyo Wapinzani kwa ahadi za Vipande vya Pesa.

Muda utaongea.
Mdini ila hayuko Peke yake
 

tracebongo

JF-Expert Member
Nov 18, 2018
1,762
2,000
Hehehehe!! Nimecheka Sana, nimeikuta u-tube. Kweli kabisa wimbo na ngoma ni tamaduni za kirundi. Nimefanya kazi Kambini miaka ya 90 nafahamu tamaduni zao.
Ngoma za kiha kunatofauti kidogo Ila zinaelekeana.
Warundi wameendelea kutukuza Ngoma yao na kuboresha zaidi hivi nyimbo zao na Ngoma zinavutia Sana hasa Kama unafaham lugha za Kiha,kihangaza,kirundi,kinyarwanda,kishubi- na kwa mbaali kisubi(maeneo hayo ni Kigoma na Ngara na pia karagwe na Tabora maeneo ya Mwese.

Kwakua nyimbo zao zinavutia Basi watanzania wa maeneo hayowanaziadopt na kuzicheza

sasa, swala la kua VP ni mrundi au la, hao watu wa maeneo hayo huwezi watofautisha kwa sura,kuzungumza na tamaduni.

Kwa vyeti na makaburi ya Babu zao, makaburi yasizidi matatu kwa umri wa mpango.

Naomba kuishia hapo.
Wewe ni Muha? Kufanya kazi kambini pekee hakukupi fursa ya kuwajua waha/warundi. Mimi ni Muha na nafanya kazi kambini (RSC) nawajua Waha, Warundi, Wasubi, Wanyarwanda ma Wahangaza na tamaduni zao. Pale alipokuwa VP ni Manyovu katika kipindi cha kampeni, ni mpakani na Burundi na kuna wenyeji (ambao ndo unawaona wanaimba) hakuna kiashiria chochote cha urundi kwa watu wale maana zile nyimbo ni za Kiha na wamevaa nguo za CCM (sidhani kama CCM wana tawi Burundi)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom