Zitto Kabwe awa mbogo, awashukia vikali wanaodai Makamu wa Rais, Dkt. Mpango ni Mrundi

Hapana ! wala si hivyo

Dr Mpango ni Raia wa Tanzania.

Je, uraia wake ni wa kuzaliwa au ni wa kupewa? Kwanini watu hawajibu hili tukamaliza ?

Kuna mtu alisemwa na Raia wa kigeni, watu wakabisha . Uchunguzi ukabaini ni kiongozi zanzibar na ni Raia wa kigeni. Si uhamiaji wala chombo chochote kile kilichobaini. Ni udaku tu
Hata kuugua kwa Magufuli ni udaku tu mwisho ikawa kweli. Kifo chake kilisemwa ni udaku tu anachapa kazi.

RC Mbeya akasema ameongea naye leo unajua alikuwa mahututi aiku hiyo
PM akasema Raia anachapa kazi kumbe alikuwa mahututi
VP kasema anakaguliwa lakini anachapa kazi kabla ya kutangaza msiba masaa kadhaa baadaye

Udaku huu unaomhusu Mpango una hoja nzito hasa kwa kuzingatia anatetewa na Ukigoma wake, halafu hakuna anayejibu hoja. Je, uraia wake ni wa kuzaliwa au wa kupewa? Bila hili kujibiwa ni dhahiri wadaku watakuwa na la kusema na kwavile wana hoja basi wanaoficha hoja ndio wadaku.
Mbona na wewe siyo raia wa TZ.
 
Hoja ya Uraia ni yakisheria siyo yakisiasa. Kwa mujibu wa sheria ya Uraia wa Tanzania Sura 258 kifungu Cha 4 raia wa Tanzania kwa kuzaliwa ni mtu aliyezaliwa ndani ya Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania mmoja wa wazazi wake akiwa Raia wa Tanzania. Kwa kifungu hiki Dr. Mpango hana utata wa Uraia kwa sababu zifuatazo;
1 . Amezaliwa Tanzania
2. Wazazi wake wote wawili wakiwa Raia wa Tanzania
3. Hajawahi kuukana Utanzania nakujipatia uraia wa nchi nyingine.

Kujadili hoja hii kisiasa na kwa mihemko nikokosa ueledi nakurukia gari kwa mbele. Sheria hii sikuwahi kuisoma ila nimeikupa mtandaoni nakuisoma ipo straight forward tujikite kwenye maendeleo.

Tuache kutafuta popularity, Kama nikucheza ngoma ya warundi mbona wamasai wa Kenya na Tz wanacheza ngoma moja? Mbona wajaluo wa Tanzania na Kenya wanacheza ngoma moja? Mbona wamakonde wa Tz na Msumbiji wa tamaduni moja?

Tumwache mzee achape kazi.
Tetea kwa nguvu, maana karibu na wewe watakuambia ni Ugandan.
 
Acha upumba-vu basi we Ki- ma. Kigoma kuna kabila linaitwa Waha, watusi na wahutu ni makabila yanapatina Burundi
Hakuna kabila la Wahutu na Watusi. Hao wote kabila moja, lugha moja, na desturi moja. Unamtambua Mtusi au Mhutu kwa "physical features" tu. Mengine yote wako sawa.
 
Humu JF watu walishahoji habari za huyu bwana 10 years ago kabla hatujafika hapa, je ni coincidence?!

Mimi nauliza mama kashauriwa na nani kumchagua bwana huyu? Hapo tuu ukweli wote upo.
 
Nyie akina vero c mnasema kigogo ni makamba, nape, na rizmoko.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
Hiyo ilijulikana siku nyingi. Na hiyo account wanaitumia wote. Kila mmoja yuko huru kuingia huko na kuichafua serkali. Jana nimeona eti Nnape anajipendekeza kumchambua raisi. Nnape ni sehemu ya CCM hawezi kujidai eti ana uchambuzi. Walipojitupa kumchafua JPM, sasa hivi wanajipendekeza. Utaona hata uchambuzi wake ulikuwa unampaka matope marehemu JPM. Nani atakaeuchukuwa huo uchambuzi. Ni muda si mrefu atajikuta hapati chochote, na wataanza machafuzi. Kwenye kujiandikisha wameficha majina yao ya kweli, maana utafiti unaonyesha mwenye kujiandikisha hayupo kwenye vitabu vya serkali, kumbe ni Nnauye, et al.
 
Acha upumba-vu basi we Ki- ma. Kigoma kuna kabila linaitwa Waha, watusi na wahutu ni makabila yanapatina Burundi
Hakuna kabila la Watusi na Wahutu Burundi, kuna kabila la Warundi. Hata Waha wana Watusi na Wahutu. Soma historia, na muulize Zitto Kabwe atakueleza. Kama hujui usiparamie.
 
Hivi hii issue kwanini ni kwa watu wa Kigoma sana?
Kwa sisi wengine tuliobahatika kutembea mikoa ya pembezoni mwa Tanzania hasa ukizingatia desturi na hulka ya watanzania kwa majirani kumekuwa na mwingiliano mkubwa wa jamii na koo mbalimbali.
Nenda kule Kilimanjaro,Nenda Mbeya,Nenda Mara ,Nenda Mtwara ,Nenda Tanga ,Nenda Arusha ,Nenda Katavi na hata Kagera ni jambo la kawaida koo moja kuwa na nasaba pande zote mbili .

Sasa kwanini kwa upande wa Kigoma inakuwa ni “Issue” kuna agenda gani ya siri ?
Hao watu wana roho mbaya usiombe
Huoni wanauana wenyeww kwa wenyewe pamoja na uchache wao kila leo
 
Ifike mahali hii nchi tuwe na viongozi wanaotokea Zanzibar mana ndio watanzania halisi isije ikawa hawa wanao tokea huu ukanda wamepandikizwa na aliyetangulia ,


Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona nilisikia huko nako kuna Waarabu, Wamalawi, Wanyamwezi, Wanyarwanda, Wasukuma, Wakurya, Warundi, Awazambia, n.k. ila hakuna anaongea lugha ya asili yake.
 
Kuna pande mbili za suala hili
1. Upande wa kwanza umeonyesha hata kwa jina la 'Dr..' ambalo linaonekana kuwa la Burundi
2. Upande wa Pili ni ule unaotumia Ukigoma kama kinga ya kutohojiwa

Ikumbukwe, Uraia una maeneo mawili, kwanza wa kuzaliwa na pili wa kufikia au kupewa

Dr Mpango ni Raia wa Tanzania iwe alizaliwa au alipewa, hilo halina mjadala

Pamoja na yote , Dr Mpango ana wajibu wa kueleza nature ya Uraia wake ili kuondoa mashaka kwamba hana uraia wa kuzaliwa au kupewa. Bila kufanya hivyo itakuwa ni halali kusema Dr Mpango si Raia

Hivyo basi Dr Mpango anapaswa ajitokeze kama kiongozi wa umma kuthibitisha aina ya Uraia wake.

Haitoshi kusema katoka Kigoma basi ni Raia, inatakiwa kwenda mbali zaidi ya hapo.

Abdul Nondo ambae sote tunajua ni kijana au mtoto alituhumiwa si Raia.

Tulijua ni uongo lakini Nondo alikwenda mbali na kuonyesha Babu yake alimpokea Nyerere, hilo tu lilimaliza ubishi kuwa kwavyovyote iwavyo wazazi wa Abdul wamezaliwa Tanzania na yeye pia na ni raia wa kuzaliwa na mjadala ulifungwa daima milele

Dr Mpango ajitokeze kama Askofu aliyetuhumiwa na ambaye alitoa uthibitisho wake.

Hii system iliundwa na akina Mpango wakiwa Baraza la Mawaziri la Magufuli kwa chuki, dhulma na ukatili

Wazungu wanasema '' Chicken are coming home to roost''

Dr Mpango anawajibika kuondoa shaka kwa vithibitisho vinginevyo hoja kwamba si Raia inamuondolewa nguvu ya kutumikia Taifa , inamuondolewa uadilifu na itia mashaka kama kweli ni Mtanzania anayepaswa kupewa dhamana na usalama wa Taifa letu.


JokaKuu Mag3 tindo The Boss Zitto
Yaani mtu apoteze muda wake kujieleza. Kigogo ni nani akihoji kitu unajieleza. Ni srerkali tu, yenye haki kukutaka ujieleze kwa lolote. Kama Kigogo anataka Dr. Mpango ajieleze, afungue kesi mahakamani yakuhoji kupewa umakamu wa raisi raia wa kigeni. Wale wote wanaomuunga mkono pia mna haki ya kufungua kesi kusitisha kuteuliwa kwake, kwa sababu si raia. Kama hamuwezi kuthubutu kufunguwa kesi ya kupinga kuteuliwa kwakebasi nyie wote ni waongo, maana mnajuwa hamuwezi kuthibitisha yeye kutokuwa raia. Hata hivyo hakimu au jaji gani atakaye kubali ushahidi wa kucheza ngoma! Enzi zetu shuleni tulikuwa tunacheza ngoma za kizulu biala kuwa Wazulu.
 
Wewe Zwazwa kwelikweli, wewe unadhani Kigoma imejaa Waha tupu??---- Zitto siyo Muha lakini ni mtetezi wa Wana kigoma WOTE. Hata mimi siyo Muha lakini sipendi kusikia Mtanzania yeyote wa Kigoma wa kabila lolote akidhulumiwa.

Awe, Muha, Muhutu, Mtutsi, Mmanyema, Muhaya, Mchaga, Msukuma, Mnyamwezi, Mjita, Mfipa nk, Kutoka Kigoma sipendi kuona akinyanyaswa na kudhulumiwa kisa Kabila lake.

Wazungu hawana mambo ya ukabila ila sisi ngozi nyeusi tuliobaguliwa na mipaka walioiweka hao wazungu bado tuko katika Utumwa wa ukabila.
Ni kweli Wazungu hawana ukabila, lakini sababu kubwa ya wazungu kutokuwa na ukabila ni kwa sababu nchi zao ziligawanyika kikabila. Zile ambazo bado zina makabila kwenye nchi zao, makabila yamepewa uwezo wa kujiamlia mambo yao wenyewe (Uingereza). Zile ambazo zilikataa kutoa autonomy zilikuja sambaratika (Yugoslavia). Nchi nyingi za Ulaya zilizobaki ni nchi zenye kabila moja, ndiyo maana hazina hivi viugomvi vya kikabila. Hata Urussi nayo ilisambaratika zikapatikana nchi kwenye misingi ya kabila. Nchi za Afrika zilizo kwenye misingi ya kikabila ni Botswana, Lesotho, na Eswatini. Sina hakika kama hizi nchi tatu za Afrika zina matatizo ya ukabila kama sisi.
 
mbona kenya mambo haya hayapo mpaka waziri wa utalii mwarabu mkuu wa majeshi alikuwa msomali mkuu wa polisi alikuwa msomali
Huko Kenya waliyo na vyeo hivyo ni Wakenya, si wakimbizi au wageni.
 
Mkuu nashukuru kwamba kuna watu wanaoelewa hoja yangu

Mpango alikuwa senior minister na passport ya Tanzania tena ya kidiploamasi! Ni Raia hadi hapo

Tunachohoji ni je, uraia wake ni wa kuzaliwa au kupewa?
Hili si tatizo kwa mtu wa kawaida, ni tatizo kwa VP ambaye anytime anakuwa Rais wa JMT

Ikiwa hana uraia wa kuzaliwa basi nafasi hiyo ina matatizo kwasababu likitokea lisilotarajiwa tutakuwa na mgogoro wa kikatiba. Kumbuka wakati huo

Trump na wafuasi wake walimwandama Obama kwa hoja kwamba si Raia wa kuzaliwa . Jambo hilo lingemuondolea sifa ya kuwa Rais.
Rais Obama aligundua ni jambo lenye public interest na akaruhusu nyaraka zake zote z kuzaliwa, Hopsitali na magazeti ziwekwe wazi

Kwa hili la Mpango, utetezi hauwezi kuwa eti ni kwasababu ni mtu kutoka Kigoma.
Hii ni hoja isiyo na mashiko kwasababu hakuna anayehoji kabila lake, wanaohoji nature ya uraia wake

Kadiri watu wanavyokuwa mbogo ndivyo hofu inaongezeka na bila Mpango kusafisha hali watu watamtazama si kama VP bali Mrundi aliyevamia na hana uhalali. Hatutaki hilo, ajitokeze na kuondoa shaka.
Unaongelea katiba ya USA au TZ!
 
Wanaohoji uraia wake hawahoji kabila, dini, kijiji au mtaa alipotoka

Wanakubali kuwa ni Raia wa Tanzania kwasababu hadi sasa anamiliki passport ya Tanzania. Ni raia

Hoja iliyopo ambayo wengi hawataki kukabiliana nayo ni hii
Je, ni raia wa kuzaliwa ndani ya ardhi ya Tanzania?
Je, ni raia aliyepewa uraia na kuwa raia wa Tanzania?

Haya ndiyo yanatakiwa kujibiwa na yana public interest kwasababu ni VP

Akiwa VP halafu akaitwa VP mrundi siku tutakapomhitaji kwa dharura yoyote kutakuwa na tatizo
Itabidi athibitishe uraia wake atake asitake. Kabla ya kufika huko Dr Mpango ana nafasi ya ku clear air.

Watu waelezwe nature ya uraia wake! si kumtetea kwa ukigoma! hapana!
Peleka kesi mahakamani, ukweli utapatikana.
 
Hapana, ukigoma wake hauna uhusiano kabisa na hoja.

Kuna habari kuhusu yeye kama ilivyokuwa kwa yule wa Zanzibar,
Ni ngumu kupuuzia habari hizo kwa kuzingatia kuwa utetezi unaoletwa ni kuhusu Ukigoma

Kwamba anakingiwa kifua si kwa nature ya uraia wake bali ni mtu kutoka Kigoma.

Hapa panatia shaka hata wale tuliokuwa hatuna shaka. Kwanini hoja ya uraia inajibiwa na ukigoma?

Nimeeleza kuhusu Abdul Nondo ambaye amezima hoja ya uraia kwa vithibitisho
Tulijua ule ulikuwa upuuzi wa serikali ya mwendazake iliyotumia vyombo vya dola hovyo , kwa chuki n.k.

Kitu kimoja, Abdul Nondo alizima hoja ile na haitarudi tena maishani mwake

Tunakubali Dr Mpango ni raia. Tunachotaka kujua ni asili ya uraia wake
Je, ni wa kuzaliwa?
Je, ni wa kupewa?

Kadri hoja hiyo inavyozimwa kwa ukigoma kuna kila sababu ya kutia shaka hasa tukizingatia ni VP

Kwani kuna tatizo gani ku clear hali ya hewa kwa vithibitisho?
Kwa nini unahangaika huku mahakama ipo! Nenda mahakama, utajuvwa.
 
Ni raia wa Zanzibar ambayo ni sehemu ya JMT! kama kuna hoja na iletwe tutahoji.

Je, uraia wa VP Dr Mpango ni wa kuzaliwa au wa kupewa?
Mbona yeye mwenyewe keshasema kuwa alizaliwa wilaya ya Buhigwe [ambayo zamani ilikuwa sehemu ya Kasulu, nadhani], mkoani Kigoma, kabla hata Tanganyika haijapata uhuru.

Hujamsikia yeye mwenyewe akisema alipozaliwa?

Btw, ziwa Tanganyika liko wapi vile?

Kazaliwa Buhigwe. Kasoma shule kuanzia ya msingi hadi shahada ya pili nchini.

Baada ya kumaliza kidato cha sita alienda jeshini kama ilivyokuwa ada kipindi hicho.

Huko jeshini walijifunza uzalendo na ukakamavu.

Leo mtu huyu mnapata ujasiri wa kuhoji uraia wake?
 
Back
Top Bottom