Zitto Kabwe aumbuka kuhusu takwimu ya vifo vya mama wajawazito kuongezeka

mamayoyo1

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
1,011
1,019
1552138060705.png

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini kuwa mkweli katika kutoa takwimu za vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi tofauti na takwimu anazozitoa.

Waziri Ummy amelazimika kumjibu Mbunge huyo baada ya kubandika taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti ACT - Wanawake, Chiku Abwao ambaye katika maadhimisho ya siku Wanawake jana alisema kwamba mwaka 2019 idadi ya wanawake wanaofariki kwa uzazi imeongezeka mpaka 11,000 kwa mwaka.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa imeeleza kwamba kipaumbele cha Serikali ya CCM kimekuwa ni kuongeza idadi ya wanawake wanaofariki kwa uzazi badala ya kupunguza jambo ambalo limetafsiriwa kama aibu kubwa kwa taifa.

Akijibu Tuhuma hizo, Waziri Ummy ameandika yafuatayo;"Kaka yangu, kwa nini husemi ukweli kuwa Takwimu hizi ni za TDHS 2015/16. Na kwamba survey nyingine itafanyika 2019/20 ambapo sina shaka kabisa kuwa vifo vitokanavyo na uzazi vitakuwa vimepungua kwa zaidi ya asilimia 50! Sema ukweli tafadhali,".

"Si kweli. Narudia tena kusisitiza TDHS ni ya 2015/16, takwimu hizi zilikusanywa 2015. hakuna Utafiti mwingine wa kitaifa uliofanyika na kutoa MMR. Hivyo tusubiri utafiti mwingine wa 2019/20 na hapo ndio mnaweza kusema ni jinsi gani Serikali imefanikiwa ktk kupunguza Vifo hivi" Amesisitiza Waziri Ummy
 
Sijaelewa Waziri Ummy anabisha kitu gani, anaposema hizo ni takwimu za 2015/16 na takwimu mpya utafiti haijafanyika anataka Zitto atoe takwimu zisizokuwepo? Anapomtaka Zitto aseme ukweli, aseme ukweli usiokuwepo? Waziri Ummy anaposema utafiti mpya utapofanyika, vifo vitakuwa vimepungua kwa asilimia 50, ana uhakika gani? Au ndio wanapika data?

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo kama ukweli haupo ndio Zito anaruhusiwa kupotosha kuwa huo ni utafiti wa 2018 wakati hakukuwa na utafiti mwaka huo?
 
Tayari matokeo ya utafiti anayo.....kwahiyo hamna haja ya utafiti kufanyika tena kwa kweli viongozi wameegemea sana upande wa siasa kuliko utendaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha halafu mleta mada anaweka bango eti Zitto kaumbuka.
Wanadanganya dawa zipo, juzi mkuu wa wilaya huko Lindi alipata ajali akahamiahiwa Muhimbili, kwanini asitibiwe huko huko ikuwa dawa, vifaa tiba na watoa huduma wapo?!
Sijaelewa Waziri Ummy anabisha kitu gani, anaposema hizo ni takwimu za 2015/16 na takwimu mpya utafiti haijafanyika anataka Zitto atoe takwimu zisizokuwepo? Anapomtaka Zitto aseme ukweli, aseme ukweli usiokuwepo? Waziri Ummy anaposema utafiti mpya utapofanyika, vifo vitakuwa vimepungua kwa asilimia 50, ana uhakika gani? Au ndio wanapika data?

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijaelewa Waziri Ummy anabisha kitu gani, anaposema hizo ni takwimu za 2015/16 na takwimu mpya utafiti haijafanyika anataka Zitto atoe takwimu zisizokuwepo? Anapomtaka Zitto aseme ukweli, aseme ukweli usiokuwepo? Waziri Ummy anaposema utafiti mpya utapofanyika, vifo vitakuwa vimepungua kwa asilimia 50, ana uhakika gani? Au ndio wanapika data?

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiona hivyo ujue DHMS ijayo inafanyikia Lumumba. Hapo ndipo tulipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mie mwenyewe ni Shahidi katika hospital za serikali uko wilayani,jamani serikali inajitahidi sana kupitia wauguzi na madktari kupunguza vifo vya mama wajawazito,kama una mpeleka mkeo kujifungua unakuta kwa siku daktari kafanya upaasuaji wa mama wajawazito 6-8 kwa ajiri ya kuokoa mama na mtoto tena bure kabisa,ingekua zamani tungekua na uwezekana wa kupoteza 4-6 kuokoa 2 serikali inajitahidi sana,Msisitizo utolewe lwa wauguzi na madactari kusimamia kwa weredi mkubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1041648

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini kuwa mkweli katika kutoa takwimu za vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi tofauti na takwimu anazozitoa.

Waziri Ummy amelazimika kumjibu Mbunge huyo baada ya kubandika taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti ACT - Wanawake, Chiku Abwao ambaye katika maadhimisho ya siku Wanawake jana alisema kwamba mwaka 2019 idadi ya wanawake wanaofariki kwa uzazi imeongezeka mpaka 11,000 kwa mwaka.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa imeeleza kwamba kipaumbele cha Serikali ya CCM kimekuwa ni kuongeza idadi ya wanawake wanaofariki kwa uzazi badala ya kupunguza jambo ambalo limetafsiriwa kama aibu kubwa kwa taifa.

Akijibu Tuhuma hizo, Waziri Ummy ameandika yafuatayo;"Kaka yangu, kwa nini husemi ukweli kuwa Takwimu hizi ni za TDHS 2015/16. Na kwamba survey nyingine itafanyika 2019/20 ambapo sina shaka kabisa kuwa vifo vitokanavyo na uzazi vitakuwa vimepungua kwa zaidi ya asilimia 50! Sema ukweli tafadhali,".

"Si kweli. Narudia tena kusisitiza TDHS ni ya 2015/16, takwimu hizi zilikusanywa 2015. hakuna Utafiti mwingine wa kitaifa uliofanyika na kutoa MMR. Hivyo tusubiri utafiti mwingine wa 2019/20 na hapo ndio mnaweza kusema ni jinsi gani Serikali imefanikiwa ktk kupunguza Vifo hivi" Amesisitiza Waziri Ummy
Hiyo haina ubishi kuwa vifo vimeongezeka hasa mara baada ya wafadhili wa kfw kujitoa

In God we trust
 
Sijaelewa Waziri Ummy anabisha kitu gani, anaposema hizo ni takwimu za 2015/16 na takwimu mpya utafiti haijafanyika anataka Zitto atoe takwimu zisizokuwepo? Anapomtaka Zitto aseme ukweli, aseme ukweli usiokuwepo? Waziri Ummy anaposema utafiti mpya utapofanyika, vifo vitakuwa vimepungua kwa asilimia 50, ana uhakika gani? Au ndio wanapika data?

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo ndiyo ujue wapo wana zipika hizo data

In God we trust
 
Kwa hiyo kama ukweli haupo ndio Zito anaruhusiwa kupotosha kuwa huo ni utafiti wa 2018 wakati hakukuwa na utafiti mwaka huo?
Alio sema zzk ndiyo ukweli wacheni kuwafanya watanzania kama wajinga

In God we trust
 
Back
Top Bottom