Zitto Kabwe atoa mawazo yake juu ya namna ya uwekezaji bora Simba SC

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Habari wanaJF, mwanasiasa na mpenda michezo nchini Zitto Kabwe akiwa kama mpenzi wa Klabu ya soka ya Simba ametoa mawazo yake juu ya biashara anayotaka kuifanya Mo Dewji ya Uwekezaji.

==================

20bn tshs endowment fund for Simba SC ni moja ya pendekezo bora zaidi kutolewa na Mwanamichezo nchini kwetu. Mohamed Dewji anapendekeza kuwa yeye atatoa tshs 20bn na kuziweka kwenye Endowment Fund kisha riba kutumika kuendesha Club. Tutakuwa na club matata sana nchini. Vyuo vikuu vikubwa duniani Kama Harvard vinaendeshwa kwa Mfumo huu anaopendekeza MO. Tukiwa na usimamizi mzuri wa Fedha tutakuwa timu bora kabisa na tutaweza hata kuwa na academy ya Simba Kama ilivyo kwa club kubwa duniani.

Hata hivyo, nashauri kwenye muundo wa umiliki, mtu mmoja asiwe na Hisa zaidi ya 40%. Ushauri wangu ni mgawanyo ufuatao;

- Mwekezaji ( MO ) 40% ( mkataba wake wa uwekezaji uonyeshe kuwa kwa kupewa Hisa hizi atafungua endowment fund ya thamani ya tshs 20bn na atakuwa na uhuru wa kuteua trustees wa Fund hiyo. Mwekezaji atakuwa na uhuru wa kuifunga fund iwapo asiporidhishwa na matumizi Fedha zinazotokana na Endowment Fund ).

- Wanachama wote wa Simba wagawiwe sawa 40% ( kuwe na cut off ya siku ya mwisho Mwanachama kujiunga kuweza kufaidika na kugawiwa Hisa hizo. Hisa za Simba SC zikishaorodheshwa kwenye soko la Hisa, Mwanachama atakuwa na uhuru wa kuuza Hisa zake freely.

- 20% ya Hisa ziorodheshwe kwenye Soko la Hisa la Dar Es Salaam kwa ajili ya 1) kuvutia wawekezaji wengine 2) kukuza mtaji wa Kampuni 3) kuwezesha uwazi kwenye uendeshaji wa kampuni kwani Wanachama wote watakuwa wanajua kila kinachoendelea kwenye kampuni na club kwa sababu soko la Hisa Lina ' disclosure rules '.

Kwanini MO asiwe na 51%? Sio MO tu, Memarts za Simba ziwe wazi kwamba hakuna mtu mmoja au kampuni moja au taasisi yeyote moja itakayoruhusiwa kuwa na zaidi ya 40% ya Hisa za kampuni. Hii itamfanya MO au mwekezaji mwingine yeyote kuhakikisha anatafuta 11% zaidi ili kupitisha maamuzi. Kuna hatari ya kumpa mtu mmoja uwezo wa kufanya maamuzi peke yake. Lazima kumfanya ashawishi japo 11% ya wenye Hisa ili kuboresha maamuzi. Leo ni MO anaipenda Simba, kesho unaweza kuwa na mtu asiye MO. Nadhani 40% ni kiwango cha kutosha kwa Mwekezaji.

Nashauri wana Simba tusicheleweshe haya MABADILIKO. Tufanye sasa hivi ili msimu huu unaoanza tuwe na timu imara yenye uhakika wa kushiriki Premier League. Mpango wa MO wa Endowment Fund ni Mpango bora na tusipoteze nafasi hii.
 
Hawa ndio wanachama wenye mawazo mazuri juu ya uwekezaji wa Mo utakavyonufaisha timu yetu ya Simba Sc. Ila viongozi wa Simba Sc wakiongozwa na Evance,wanaonekana kuwa kinyume na mabadiliko
 
Tatizo sidhani kama Mo atakubali hiyo 40 %. Inaelekea anataka kuwa na sauti kubwa na ya mwisho pale Simba. Mengine yatakuwa na maoni tu lakini yeye atakuwa mwamuzi wa mwisho.

Tusubiri tuone kama Mo atakubali wazo lenye kupunguza nguvu yake !
 
Napendekeza huu ushauri ufike moja kwa moja kwa uongozi na haya yawe ndo maoni wanasimba nimeipitisha hii hoja...!!!
 
Napendekeza huu ushauri ufike moja kwa moja kwa uongozi na haya yawe ndo maoni wanasimba nimeipitisha hii hoja...!!!
kuna watu wengi wana maoni tofauti hivyo wazo la mtu mmoja lisischukuliwe kama ndio maoni ya wanasimba wote.
nimezungumza na wanachama na wapenzi wengi wa simba nilichogundua wengi hawana ufahamu wa mambo ya hisa, wengine wanasema tunampa mo 51% kwa mkataba baada ya hapo timu inarudi kwetu.Nimewaambia sasa hv mnampa mo hizo hisa za 51% kwa bilioni ishirini baada ya miaka mtakayokubaliana arudishe simba kabla ya kurudisha atapiga hesabu timu ina thamani gani hivyo atawarudishia kwa thamni ya wakati huo kitu ambacho cha uhakika simba hawatakuwa na uwezo wa kurudisha.
Huu mjadala umefanywa kwa ushabiki mno, thamani ya simba sio majengo au uwanja wa bunju bali pia na kujumlisha na idadi ya wapenzi ilionao ambao ni zaidi ya milioni nne ambazo ukigawanya kwa bilioni ishirini inamaana kila mpenzi thamani ni shilingi elfu 5 hilo nimechukua kisio la chini kabisa na wanachama hao wakiuziwa jezi kwa elfu kumi tayari hiyo pesa itarudi mara mbili.
katika ule mkutano kulikuwa na taarifa ya fedha ya simba ambayo ilionyesha kuna wapangaji hawana mikataba,baadhi ya mapato ya mechi hayaonekani na hata mauzo ya jezi hayaeleweki lakini badala ya wanachama kujadili vitu hivyo wao wakakimbilia kumjadili mo na bilioni 20.
Ni vizuri ikafanyika tathimini ya kina ya thamani ya simba kabla ya kurupuka pia waelewe simba ina wanachama elfu 6 hao wanachama 600 wasijidanganye kuwa wana uwezo wa kufanya maamuzi kama hayo kama tunataka kuweka timu sokoni tupate thamani yake halafu tushindanishe watu wenye uwezo
 
Napendekeza huu ushauri ufike moja kwa moja kwa uongozi na haya yawe ndo maoni wanasimba nimeipitisha hii hoja...!!!
Zitto aliwahi kuwa kwenye kamati moja wapo ya Simba hivyo nadhani atayapeleka mapendekezo yake na itakuwa ni akili mgando kama viongozi wa Simba watashindwa kuwatumia wanachama wenye elimu ya uchumi kama Zitto...
 
Mimi napendekeza klabu akabiziwe tajiri wa TP Mazembe, ukweli ni kwamba sina imani na wahindi, sio watu wampira, wako radhi kuhujumu timu ili wao waonekane bora.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom