Zitto Kabwe atoa maelekezo mazito kwa wanachama wa ACT Wazalendo na Watanzania kwa ujumla

Hilo tamko limekwenda shule,
Najiuliza Kitu Kimoja, ACT imefanya Juhudi kuwatafuta wenzao wa UKAWA waunganishe nguvu Kulinda Demokrasia lakini Hawajibiwi, Sijui kwa nini Ukawa hususan Chadema wanabehave namna hii!

Tunahitaji nguvu moja katika hili jambo
Inaonekana sasa kama zitto anatuangusha, hawa chadema ni wahuni wanywa viroba,kwanini anawapa kiki?tupambane kivyetu.
 
Zitto my brother, siasa zako ungeweza kuendana na Chadema ungefika mbali Sana mkuu...
Try to compromise......Chadema Na wew mnaunda best team, sijui huwa mnatofautiana wapi.......
Chadem wamekataa kuwashirikisha sasa yeye ajipendekeze? Kwanza Zitto hatokubali kushiriki kwenye ukuta. Na hataki maandamano.
 
Kwa maelezo yako haya Zito, ni wazi kuwa wewe na chama chako hamuendani kabisa na CHADEMA, UKAWA, na UKUTA. Na hauna sababu ya kushangaa kwa nini walikataa kushirikiana na wewe na chama chenu. Kejeli na vijembe vilivyokujaa vinadhihirisha huwezi kwenda nao pamoja.
 
"...Hata hivyo, hakuna Kiongozi
wa Chama chochote kile
ambaye aliona umuhimu
wa kuunganisha nguvu na
hivyo kujikuta kila Chama
kinaendelea na operesheni
zake. Viongozi wetu
akiwemo Katibu Mkuu na
Naibu Katibu Mkuu
walifanya juhudi zote
kuwasiliana na watendaji
wenzao wa Vyama vingine
ili kufanya Kazi pamoja japo
kwa uratibu lakini
hatukupiga hatua yeyote ile.
Hivyo, Sisi sio sehemu ya
operesheni yeyote ile
iliyotangazwa na Chama
kingine chochote kile
isipokuwa Operesheni
Linda Demokrasia ambayo
sasa itaitwa Tamko la
Mbagala la Juni 5, 2016..."
 
Hua najuliza Mara nyingi, Hawa wanasiasa hasa Wa upinzani, wana nia ya dhati kweli ya kushika dola, kwanini wasiunganishe nguvu na kua chama kimoja?

Wapinzani wanatakiwa kua nguvu Moja
Sauti Moja
Sera moja yenye manufaa kwa nchi yetu
 
CHADEMA wamekataa kuungana na ACT katika kulinda demokrasia, sasa kama maandamano ni ya Chadema sio ACT-W. Hata hivyo misingi ya ACT na itikadi haiamini katika siasa za maandamano bila hoja. Kwa muktadha huo ACT haitashiriki wala kufurahia Maandamano yoyote au vurugu zozote za kisiasa. Mh. Magufuli katoa wito wa kutaka utulivu nchini sawa na imani ya ACT. CHADEMA wanajiona kama wanaweza bila ACT sasa tunasubiri wafyokolewe ili tuwaoneshe siasa bora za nguvu ya hoja.
Tunawatakia kufyokolewa kwema.
 
Safi sana Zitto unganeni kumpinga huyu Nduli Idd Amin Dadaa mpya wa Tanzania
Bora hata na iddi amin huyu wa kwetu ni uchwaraaa..hana maono hana prioryty yupoyupo tu anataka kutuletea umaskini wa kudumu kwa vile amekosa priorities!
 
Katika maelezo ya Mh. Zitto hapo juu kuna sehemu imeelezwa kuwa chama chetu yaani ACT-Wazalendo asili ya uundwaji wake ni kupinga tabia za kidikteta tulizokumbana nazo ndani ya vyama tulivyokuwemo. Tafsiri rahisi ni kwamba moja ya chama lengwa hapa ni Chadema kwani chama cha siasa alichowahi kutumikia kabla ya ACT ni Chadema.
 
Mbona hizi oparesheni zinachanganya, ya manyumbu UKUTA ya kwetu LINDA DEMOKRASIA (LIDEM):D nyota ya magufuli kiboko.
 
Nduli Idd Amin mpya akianza kukata vichwa na miguu ya watanzania ndio utajua hasara ya kuwa mnafiki
key words za uwepo wa Chadema ni demokrasia na maendeleo! Maendeleo haisisitizwi
kwenye mikusanyiko ya chama. Mikakati ya kuleta maendeleo haiwekwi wazi !!Demokrasia ndiyo wanahangaika nayo
.Demokrasia inashamiri mkiwa na maendeleo. ..demokrasia inaonekana katika nchi zilizoendelea
kwa sababu walijiendeleza kwanza ndiyo wakaja kupata maendeleo. Ni rahisi kuingiza demokrasia
kwa watu walioendelea. Kumbuka, Demokrasia ni makubaliano ya watu katika eneo linalotambulika mipaka yake ama jamii
inayojulikana rasmi namna ya kujiendesha katika masuala ya kimaamuzi na kiutawala (Courtesy Nguruvi3).
Hivyo maendeleo kwanza demokrasia baadaye. Tushibe kwanza demokrasia baadaye.

==========
Zitto !!!
 
Mbona hizi oparesheni zinachanganya, ya manyumbu UKUTA ya kwetu LINDA DEMOKRASIA (LIDEM):D nyota ya magufuli kiboko.
Siku Nduli Idd Amin huyu wa Tanzania akianza kukata vichwa vya waTu utaacha kushangilia na kuimba mapambio.Kilio chako hakitakuwa na mfaliji wote tutakuwa tunalia
 
Akishindwa kujenga hata kiwanda kimoja atasingizia wapinzani walikuwa wanamsumbua
 
ZITTO KABWE ATOA MAELEKEZO MAZITO KWA WANACHAMA WA ACT NA WATANZANIA KWA UJUMLA

Maelekezo ya Kiongozi wa Chama ( KC ) kwa wanachama wote wa ACT Wazalendo ( KC/01/2016 ).

Mamlaka

Katiba ya ACT Wazalendo toleo la mwaka 2015 Ibara ya 29 inatoa mamlaka kwa Kiongozi wa Chama kutoa maelekezo kwa Viongozi na Wanachama wa Chama kila inapobidi. Maelekezo yafuatayo ( KC/01/2016 ) nayatoa kwa kila mwanachama kufuatia Hali ya Siasa inayoendelea nchini. Maelekezo haya yabandikwe kwenye kila Ofisi ya Chama kuanzia Taifa mpaka Tawi na yasomwe kwenye Mikutano Mikuu ya Chama ya Matawi yote nchini ndani ya Mwezi huu wa Agosti, 2016. Maelekezo haya pia yatumwe kwenye kila ' Whatsapp Group ' la Chama na Ngome zote za Chama.

Maelezo

Tangu kukamilika kwa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 Utawala mpya umekuwa ukifanya kila juhudi kuminya uwezo wa Vyama vya Siasa kufanya Kazi zake kwa kisingizio kuwa huu ni wakati wa kufanya Kazi na kwamba Siasa zisubiri mwaka 2020. Chama chetu kilipinga kwa nguvu zote uzuiaji huu wa shughuli za kisiasa kwani ni kinyume cha Katiba ya Nchi na Sheria ya Vyama vya Siasa, sheria namba 5 ya mwaka 1992 kama ilivyofanyiwa marekebisho Mara kwa Mara.

Mnamo tarehe 5 Juni 2016 Chama chetu kilifanya Mkutano wa Hadhara Mbagala jijini Dar Es Salaam na kutangaza Operesheni Linda Demokrasia. Lengo la Operesheni hiyo ( Tamko la Mbagala 2016 ) ni kuhakikisha kuwa Tanzania inaendelea kuwa Nchi ya kidemokrasia na kuepuka mwelekeo wa Utawala wa Imla ambao ni utawala wa kidikteta. Chama chetu asili ya uundwaji wake ni kupinga tabia za kidikteta tulizokumbana nazo ndani ya Vyama tulivyokuwamo. Hivyo ilibidi tuwe mstari wa mbele kupinga dalili zozote za kuielekeza Nchi kwenye Uimla. Vyama unaweza kuunda utakapo, Nchi huwezi kuiunda ndio maana ni LAZIMA Sisi Kama wanachama wa Chama cha Wazalendo kupinga kwa nguvu zote kuminywa kwa Demokrasia na kuilinda kwa nguvu zetu zote.

Kufuatia Tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano kwamba shughuli za kisiasa zimezuiwa kwa niaba yenu nilitaka Vyama vyote vya Siasa nchini na wadau wengine wa demokrasia kuungana kwa pamoja kukataa Tamko hili ambalo linavunja Katiba ya Nchi ambayo Rais ameapa kuilinda na kuitetea. Wito wetu unanukuliwa hapa chini;

" Tunatoa wito kwa Vyama vyote vya siasa nchini kuunganisha nguvu katika kuhakikisha tunapigana vita [ dhidi ya udikteta] pamoja. Huu ni wakati wa vyama vya siasa na wanasiasa kuacha tofauti zao na kupambana kulinda uhuru wa kufanya siasa wakati wowote kwa mujibu wa Sheria."

Hata hivyo, hakuna Kiongozi wa Chama chochote kile ambaye aliona umuhimu wa kuunganisha nguvu na hivyo kujikuta kila Chama kinaendelea na operesheni zake. Viongozi wetu akiwemo Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu walifanya juhudi zote kuwasiliana na watendaji wenzao wa Vyama vingine ili kufanya Kazi pamoja japo kwa uratibu lakini hatukupiga hatua yeyote ile. Hivyo, Sisi sio sehemu ya operesheni yeyote ile iliyotangazwa na Chama kingine chochote kile isipokuwa Operesheni Linda Demokrasia ambayo sasa itaitwa Tamko la Mbagala la Juni 5, 2016.

Akiwa ziarani mkoani Singida, Rais amefafanua agizo lake la kuzuia mikutano ya kisiasa. Rais amesema kwamba hajazuia wabunge na madiwani kufanya mikutano ' KWENYE MAJIMBO YAO'. Kwanza Rais hana mamlaka ya kuruhusu au kuzuia Kazi za Wabunge na madiwani. Haya ni mamlaka ya KATIBA na sheria za Nchi. Hivyo ufafanuzi wake hauna maana yeyote ile.

Jambo la kushtusha ni agizo la Rais kwamba Wabunge hawana mamlaka ya kufanya mikutano nje ya majimbo yao. Hii ina maana hata Viongozi wa kisiasa ambao sio wabunge hawataruhusiwa kufanya mikutano ya kisiasa. Hii HAIKUBALIKI. Anna Elisha Mghwira ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Taifa, anazuiwaje kufanya mikutano na wanachama wake nchini? Anazuiwaje kuongeza wanachama? Lakini mama Anna Mghwira aligombea Urais, kwanini asifanye mikutano kuwashukuru waliompa Kura japo hazikutosha?

Uchambuzi wa kitaalamu

Ni dhahiri Serikali ya Awamu ya Tano na sasa Chama tawala wameamua kubadili mwelekeo wa Nchi kisiasa ( kwa kubana uhuru wa kidemokrasia ) na kiuchumi ( kwa kuelekeza nguvu kwenye uchumi unaoelekezwa/endeshwa na dola ). Udhibiti wa Vyama vya Siasa ni moja ya hatua ya udhibiti wa jamii kwa ujumla wake. Siku za usoni tutaona udhibiti wa waziwazi wa vyombo vya habari na kwa sasa tunaona namna Asasi za Kiraia ( CSOs) zilivyo kimya tofauti na miaka michache ya nyuma. Hizi zimejiweka kimya zenyewe na zitakazoinua sauti zitafuatiliwa na dola. Yote haya yanaturudisha nyuma katika katika kujenga Tanzania ya Kidemokrasia na yenye Maendeleo.

Utawala wowote ' regime ' hutaka kupata nguvu ya wananchi katika kujijengea uhalali. Serikali ya Awamu ya Tano imeamua kuichukua vita dhidi ya ufisadi kama njia ya kujijengea uhalali na kwa kweli wananchi wengi waliochukizwa na vitendo vya kifisadi wanaunga mkono juhudi hizo. Katika ziara yake ya Singida, Rais amenza kutumia maneno kama ' mabeberu ' na ' Maadili ya Mwalimu Nyerere ' maneno ambayo hayajawahi kutamkwa na kinywa chake. Hii inaonyesha kuwa Rais anaanza kukua/kukuzwa kiitikadi na hii itampa uhalali zaidi mbele ya jamii. Hata Uamuzi wake wa kutekeleza maamuzi ya kuhamia Dodoma, na iwapo atatekeleza, itamjengea zaidi uhalali. Rais atautumia uhalali huu kujikita katika utawala na kuminya zaidi Demokrasia.

Maelekezo ya Kiongozi wa Chama ( KC )

1. Chama cha ACT Wazalendo kiliundwa kwa madhumuni ya kurejesha Nchi kwenye misingi. Kupitia Azimio la Tabora linalohuisha Azimio la Arusha tumeeleza misingi hiyo kwa kina. Naelekeza kwamba wanachama wote wa ACT Wazalendo wasome, kuelewa na kujadili Azimio la Tabora na kuchambua muktadha wake katika mazingira ya sasa ya Siasa za Nchi yetu.
2. Kila Mwanachama wa ACT Wazalendo asione aibu kuunga mkono maamuzi yeyote ya Serikali au Chama kingine cha Siasa yanayoendana na Azimio la Tabora hususan vita dhidi ya ufisadi na kurejeshwa kwa Miiko ya Uongozi.
3. Kila Mwanachama wa ACT Wazalendo akatae kwa namna anayoweza lakini kwa Amani mbinu zozote za kuminya Demokrasia nchini. Tamko la Mbagala la kulinda Demokrasia litumike kuongoza juhudi hizo. Chama chetu hakijatangaza maandamano na hivyo wanachama wetu wasiingie katika mambo hayo. Hata hivyo kila mwanachama wa Chama chetu aandike barua kwa Rais Magufuli kwa namna anavyoona yeye kumtaka aache kuingiza Nchi kwenye utawala wa Imla. Chama chetu kina wanachama 431,120 wenye kadi. Ikulu ikipata barua 200,000 kutoka kila kona ya Nchi itafunguka macho.

Mwisho

Nawataka wanachama wa Chama Cha ACT Wazalendo kukumbuka kuwa uasili wa Chama chetu ni kupinga kuburuzwa, ufisadi na Siasa za ujanja ujanja. Tujitahidi kwa nguvu zetu zote kutofanya yale ambayo Sisi tumeyakataa. Viongozi wa kuchaguliwa kwenye vyombo vya uwakilishi Kama madiwani na wabunge wawe makini sana kutii Chama na misingi ya chama. Tuwe mstari wa mbele kupinga ufisadi kwani rushwa ni adui wa Haki. Tuwe mstari wa mbele kutaka kurejeshwa kwa Miiko ya Uongozi. Sisi ndio Chama pekee chenye itikadi iliyo wazi. Tusiammie itikadi yetu popote tulipo na bila woga wala aibu.

Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kiongozi wa Chama

30/7/2016
Zitto maandamano mhm sana ila na wewe uje kwenye maandamano ukiwa na familia yako aka mkeo
 
Back
Top Bottom