ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
ZITTO KABWE AREJEA NCHINI KUTOKA INDIA
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Mh. Zitto Kabwe.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Mh. Zitto Kabwe, aliyekuwa amelazwa hospitali nchini India kwa zaidi ya wiki tatu kwa matibabu, amerejea nchini baada ya kupata nafuu na anatarajiwa kuanza kuhudhuria vikao vya Bunge linaloendelea hivi sasa mjini Dodoma, kuanzia leo.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, aliyekuwa amelazwa hospitali nchini India kwa zaidi ya wiki tatu kwa matibabu, amerejea nchini baada ya kupata nafuu na anatarajiwa kuanza kuhudhuria vikao vya Bunge linaloendelea hivi sasa mjini Dodoma, kuanzia leo.
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alithibitisha kurejea kwa Zitto nchini alipozungumza na NIPASHE jana.
Dk. Kashililah alisema Zitto baada ya kurejea nchini, anatarajia kwenda bungeni siku yoyote kuanzia leo kwani ana hoja, ambayo ipo bungeni.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda, aliliambia NIPASHE jana kuwa Zitto aliruhusiwa na daktari wake kutoka baada ya hali yake kuendelea vizuri.
"…Nina taarifa za (Zitto) kuruhusiwa kutoka hospitali alikokuwa anapatiwa matibabu kutokana na hali yake kuwa nzuri na madaktari kumruhusu," alisema Waziri Mponda.
Kuhusu hali ya Waziri wa Maji, Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Cyril Chami, Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, hali zao zinaendelea vizuri na hivi karibuni wataruhusiwa kurudi nchini.
Akizungumza na NIPASHE, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa, alisema hali za viongozi wanaotibiwa nchini India, zinaendelea vizuri na kwamba wamekuwa wakiwasiliana nao mara kwa mara.
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, alithibitisha Zitto kurejea nchini.
Alisema anazo taarifa kuwa Zitto aliingia nchini Oktoba 13, mwaka huu (Jumapili).
"Nimepatiwa taarifa kuwa amewasili juzi (Jumapili), ila bado sijaonana naye kwa kuwa tupo Dodoma bungeni. Ila hali yake nimeambiwa inaendelea vizuri. Sijajua ni kwanini hapokei simu yake labda hakupenda kuzungumza na vyombo vya habari," alisema Kafulila.
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Taifa, John Heche, alisema taarifa za kurejea Zitto ni za kweli kwani naye aliambiwa amewasili na anaendelea vizuri.
"Sijajua ni siku gani amerejea nchini, ila nilipatiwa taarifa kuwa amerudi na kwa sasa nipo njiani natokea Dodoma naelekea Dar es Salaam nitakapofika nitajua vizuri," alisema Heche.
Zitto alipotafutwa jana na NIPASHE, hakupatikana na hata alipopigiwa simu yake ya mkononi, mara zote ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Kabla ya kupelekwa India, Zitto alilazwa katika Hospitali ya Aga Khan akisumbuliwa na homa pamoja na maumivu makali sehemu ya kichwa.
Baadaye, afya yake ilibadilika na kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=35440
Akiwa hospitalini hapo, ilibainika kuwa mbunge huyo ana vijidudu 150 vya malaria na kuwekwa katika wodi ya magonjwa ya dharura kwa siku mbili.
Ilipofika Oktoba 28, mwaka huu, alisafirishwa kwenda India kwa ajili ya kupatiwa matibabu ambayo yalihusu upasuaji ndani ya pua.
SOURCE: NIPASHE