jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 35,053
- 28,245
- Thread starter
- #41
Hapo awali nilishasema kuwa "Mbwa Kumng'ata mtu sio habari kwani ndio kawaida yake ila Mtu akimng'ata Mbwa inakuwa ni habari " Tafsiri ni kwamba tumezoea kumsikia Zitto akikosoa kila uchao na kila jambo kinalofanywa na Serikali kiasi kwamba haiwezi kuwa ni jambo la kushangaza lakini leo hii tunasikia akiipongeza Serikali na haswa kiongozi mkuu..hii lazima iitwe habari na ina maana kubwa sanaKupongeza penye jambo jema ni mojawapo ya tabia za kistaarabu,kiwerevu na kibusara. Kukosoa penye makosa pia ni jambo jema na ni tabia ya kistaarabu,kiwerevu na kibusara.
Kupokea ushauri,pongezi,ukosoaji na changamoto nako ni jambo jema na la kistaarabu,kiwerevu na kibusara. Tatizo lipo kwako unayeangalia pongezi tu na bila kujali wala kuyaweka yale yaliyokosolewa. Wewe ulichofanya ni propaganda kama za wale aliosema mdau hapo juu kuhusu "hakuna Mungu".
Umenukuu "hakuna Mungu" badala ya kunukuu "Mpumbavu asema hakuna Mungu".