Zitto Kabwe apendekeza TANESCO wauze hisa(20%) fedha itakayopatikana ilipe madeni, Waziri Makamba atoa maagizo

HORSE POWER

JF-Expert Member
Feb 22, 2015
1,827
2,000
Ushauri wangu kwako Mheshimiwa Waziri kwanza kabisa vunja hiyo bodi na ng'oa menejimenti yote na kusuka safu mpya yenye wataalamu wenye weledi usiotia shaka na uzalendo kindakindaki.Bodi goi goi huzaa menejimenti goi goi na uzembe,wizi,uvivu na kiburi kwa watendaji wa chini na kunajisi ufanisi mzima wa Shirika.

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Hajto

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
4,290
2,000
Hatua ya kwanza kuelekea kubinafisisha utoaji huduma muhimu ya nishati kwa umma. Nishati ni injini ya uendeshaji na ukuzaji uchumi kwa taifa. Umilikishaji wa jumla ya huduma hii muhimu kwa watu binafsi ni mwanzo wa hatari isiyoonekana kwa sasa...! Naanza kuiona SOVIET iliyoanguka.
Kumbuka miaka iyo tuliyokuwepo enzi ya ttcl,na leo hii tupo katika teknolojia gani,ndio utaelewa Tanesco bila ya kupata ushindani umeme bado utatusumbua sana
 
babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,928
2,000
Walianza IPTL kama sikosei
Wameanzia mbali mpaka nimesahau!!
Hasara ya Tanesco kwa asilimia kubwa imechangiwa na mikataba mibovu!

Watu wanajuha bwawa la Nyerere likiisha na kuanza kuzalisha Umeme. Halafu mikataba mibovu ikavunjwa na kuwaondoa wafanyakazi wazembe. Tanesco kupata hasara itakuwa historia.

Sifa atapewa Marehemu!!
 
katitu

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,119
2,000
Kiongozi wa Chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe amemshauri waziri wa nishati January Makamba apeleke DSE 20% ya hisa za Tanesco zikauzwe na fedha itakayopatikana itumike kulipa madeni ya Shirika.

Kipele kimepata mkunaji, anasisitiza Zitto Kabwe katika page yake ya twitter.

Waziri January Makamba amekubali kupokea ushauri huo.

Kwenu wadau, 20% ya Tanesco ni bei gani?

====

Zitto Kabwe amesema: "Kipele kimepata mkunaji! Orodhesha 20% ya Hisa za Shirika kwa Soko la Hisa la Dar es Salaam. Mapato elekeza 1) Lipa Madeni yenye riba kubwa 2) punguza Umeme unaopotea 3) ongeza uzalishaji wa Umeme wa Gesi Asilia ( Kinyerezi 3 and 4 ). LAKINI sio kwa Bodi iliyopo! Sheria ya Umeme?"

Waziri Makamba atoa maagizo TANESCO

Waziri Janauari Makamba amesema;

Jana nimefanya ziara fupi kwenye Kituo cha Udhibiti wa Mfumo wa Usafirishaji Umeme (Grid Control Center - GCC), Ubungo, Dar es Salaam. Ziara hii haikuwa sehemu ya Mpango Kazi wa Miezi Sita niliojipangia bali ni kutokana na malalamiko ya wananchi wengi kuhusu kukatika kwa umeme mara kwa mara katika siku, wiki na miezi ya hivi karibuni.

TANESCO wametoa sababu nyingi za kadhia hii. Lakini nimebaini mambo manne:-

1. TANESCO haina mfumo wa kiteknolojia wa kubaini kwa haraka ukatikaji wa umeme kwenye maeneo mengi ya mitaani (yaliyo katika mfumo wa usambazaji).

2. Wananchi wengi wanakosa namna ya uhakika ya kuripoti kukatika kwa umeme au changamoto nyinginezo ikiwemo kuunganishiwa umeme, na hata pale wanapoweza, hawapati majibu fasaha au majawabu huchelewa kupatikana.

3. Taarifa za awali (advance notice) za kuzimwa kwa umeme katika maeneo kadhaa kutokana na matengenezo yaliyopangwa (planned mantainance), hazipelekwi kwa ufanisi kwa wananchi walio wengi. Hivyo, kupelekea kukosekana kwa maandalizi na hivyo kuongeza malalamiko.

4. Kwa muda mrefu, matengenezo ya kawaida (repair and maintenance) ya miundombinu ya usafirishaji na usambazaji umeme yamekuwa hayafanyiki kwa kiwango stahiki na hivyo kupelekea miundombinu kuwa chakavu na kusababisha kadhia ya sasa ya kukatika kwa umeme mara kwa mara. Mwaka jana, kwenye repair and mantainace ya miundombinu ya usafirishaji na usambazaji, TANESCO ilipanga kutumia shilingi bilioni 80.5 (ambayo bado ni chini ya kiwango cha kimataifa ki-asilimia ya mapato ya Shirika). Hata hivyo, kiwango kilichotumika ni shilingi bilioni 67 tu.

Ili kukabiliana na kadhia ya kukatika kwa umeme mara kwa mara, nimeelekeza TANESCO kama ifuatavyo:-

1. Kuhakikisha kwamba tatizo hili, hasa pale kunapotokana na uzembe na ucheleweshaji wa matengenezo, linaisha ndani ya wiki mbili. Zaidi ya hapo, tutalazimika kuwaondoa kazini wahusika.

2. Kuimarisha mfumo wa huduma kwa wateja, ikiwemo kuweka mfumo wa kiteknolojia wa kupokea na kutoa taarifa, kwa wakati na kwa ufasaha, kwa wananchi.

3. Viongozi wa Shirika kutokimbia wajibu wa kuwasiliana na umma kuhusu changamoto za huduma ya umeme na kutegemea wanasiasa wawasemee. Kwahiyo, kuanzia Jumatatu, tarehe 20/09/2021, kwa wiki nzima, wawakilishi wa Shirika wajitokeze kwenye vipindi vya moja kwa moja vya vyombo vya habari mbalimbali vya habari na kupokea kero za wateja wao kuhusu huduma ya umeme na kuzitolea majawabu.

4. Kuhakikisha kwamba matengenezo na maboresho yanayopaswa kufanywa kwenye mfumo wa usafirishaji na usambazaji, ili kuondoa vifaa chakavu, yanafanyika bila kucheleweshwa. Na Wizara ipatiwe repair na maintenance plan.

Pamoja na kwamba sikuwa nimepanga kufanya ziara hii kwa wakati huu, nilichukua fursa hii kuwajulisha wafanyakazi wa TANESCO niliozungumza nao kwamba mabadiliko makubwa yanakuja ndani ya Shirika. Mabadiliko hayo yanaweza kuja na machungu, lakini ni uchungu wa uzazi – unaoishia kwenye furaha. Niliwajulisha kwamba tunawaamini na kuthamini na kutegemea utalaam wao katika uendeshaji wa Shirika hili nyeti.

Tunataka kuipeleka TANESCO kwenye ngazi ya kuwa moja ya mashirika yenye thamani kubwa na yanayoheshimika zaidi Afrika Mashariki na Kati. TANESCO ina mapato ya mwaka ya takribani shilingi trilioni 1.8 – zaidi ya shirika au kampuni yoyote ile nchini, ama ya umma au binafsi. Lakini pia matumizi yake ni trilioni 1.8 – na ina deni linalokaribia shilingi trilioni moja. Ni shirika lenye mali nyingi – za thamani ya shilingi trilioni 13 - kuliko karibu kampuni yoyote nchini. Kwa assets hizi, na mapato haya, TANESCO haipaswi kusuasua kama ilivyo sasa. Asilimia 88 ya mapato ya TANESCO (shilingi trilioni 1.6) inatokana na mauzo ya umeme, kwa wateja milioni 3.2 tu. Inawezekana kabisa kutengeneza wateja wapya mara tatu ya hawa. Asilimia 23 ya gharama za TANESCO (shilingi bilioni 412) ni gharama za uchakavu wa mitambo na miundombinu (depreciation).

Kutokana na uchakavu wa mitambo na miundombinu, TANESCO mwaka jana ilipoteza asilimia 16 ya umeme iliosafirisha. Kiwango cha umeme kinachoruhusiwa kupotea kimataifa ni asilimia 5. Kwahiyo, mwaka jana, tulipoteza zaidi ya asilimia 10 ya umeme tuliosafirisha – sawa na takribani Megawati 120, umeme unaotosha kuhudumia mikoa zaidi ya nane (Iringa, Njombe, Ruvuma, Tabora, Manyara, Singida, Lindi, na Mtwara).

Kwa kifupi, kuna masuala mengi ya kuyapitia,ikiwemo namna ambavyo manunuzi yanafanyika. Jambo la msingi ni kwamba tutaliboresha Shirika kwa namna ambayo itawaweka juu na kuwapa thamani kubwa wateja na wafanyakazi wa Shirika. Wafanyakazi ni rasilimali muhimu katika utendaji wa Shirika. Tunataka wawe na ari mpya na kwamba hatutafokeana kama watoto wadogo na kwamba utalaamu wao utaheshimiwa bali uzembe hautavumiliwa. Tutapata siku maalumu ya kuzungumza na wafanyakazi na viongozi wote wa TANESCO na kuelezea kwa kirefu zaidi haya niliyoyagusia hapa, pamoja kuwapa muongozo, dira na mwelekeo mpya.

January Makamba (MB)

Waziri wa Nishati

View attachment 1945273

View attachment 1945271

View attachment 1945272
 
katitu

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
1,119
2,000
Nani anunue hisa za shirika mfu kama TANESCO
Hapa kanatengenezwa kaufisadi kengine.ujue tayari kuna mafisadi wameona huko kuna fursa na baada tu ya kufloat hizo share kataanzishwa kamchezo fulani hivi ili shirika lote liangukie mikononi mwa mafisa na makuwadi wa ubeberu.ni mchezo ule ule kama wa IPTL unaotaka kutengenezwa hapo.subirini tu huu ujinga wetu watz wa kushadadia mambo ck moja utakuja kutucost.NBC pia ilikuwa vile vile ikauzwa kwa bei ya kutupwa baadaye tukaanza kulalamika lkn tulikuwa wa kwanza kushadadia uuzwaji wake.
 
babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,928
2,000

Tujikumbushe alichosema PM Majaliwa wakati alipoenda kuangalia maendeleo ya ujenzi wa bwawa la Nyerere:

Lengo la kuanzisha mradi huu ni moja ya juhudi za Serikali za kupunguza gharama za umeme kwa wananchi kwa sababu uzalishaji wake ni wa gharama nafuu ukilinganisha na vyanzo vingine. Uniti moja ya umeme unaozalishwa kwa kutumia maji inagharimu shilingi 36 hadi shilingi 50 huku umeme unaotumia vyanzo vya mafuta uniti moja inazalishwa kwa gharama ya shilingi 440 hadi shilingi 600.”
 
babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,928
2,000
Bwawa la Nyerere:
Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato ameishukuru Serikali kwa kuwa wakati wote tangu kuanza kwa mradi huo hadi sasa imeendelea kutoa fedha za kugharamia mradi huo kwa wakati na tayari imeshatoa zaidi ya shilingi trilioni mbili. Hadi kukamilika mradi huo utagharimu shilingi trilioni 6.5.
 
babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
4,928
2,000
Mlianza na IPTL, hamkuridhika, mkaja na Richmond hamkuridhika nk. sasa mnataka kuiua kabisa Tanesco. Kumbe ndiyo maana wafanyakazi wa Tanesco wanafanya hayo wanayoyafanya - wanahisi soon tanesco haitakuwepo.
Zitto kumbuka ya NBC, Mwalimu Nyerere alishauri wakaziba masikio - masikini Nyerere, nadhani alikufa akiwa na masikitiko makubwa.
Serikali imewekeza kwenye Ujenzi wa bwawa la Nyerere trilioni 6.5. Na wameshatoa trilioni 2.
Halafu watu wanataka kuja kula kilani!!
I just wonder…how can they sleep at night!!
 
Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,020
2,000
Kiongozi wa Chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe amemshauri waziri wa nishati January Makamba apeleke DSE 20% ya hisa za Tanesco zikauzwe na fedha itakayopatikana itumike kulipa madeni ya Shirika.

Kipele kimepata mkunaji, anasisitiza Zitto Kabwe katika page yake ya twitter.

Waziri January Makamba amekubali kupokea ushauri huo.

Kwenu wadau, 20% ya Tanesco ni bei gani?

====

Zitto Kabwe amesema: "Kipele kimepata mkunaji! Orodhesha 20% ya Hisa za Shirika kwa Soko la Hisa la Dar es Salaam. Mapato elekeza 1) Lipa Madeni yenye riba kubwa 2) punguza Umeme unaopotea 3) ongeza uzalishaji wa Umeme wa Gesi Asilia ( Kinyerezi 3 and 4 ). LAKINI sio kwa Bodi iliyopo! Sheria ya Umeme?"

Waziri Makamba atoa maagizo TANESCO

Waziri Janauari Makamba amesema;

Jana nimefanya ziara fupi kwenye Kituo cha Udhibiti wa Mfumo wa Usafirishaji Umeme (Grid Control Center - GCC), Ubungo, Dar es Salaam. Ziara hii haikuwa sehemu ya Mpango Kazi wa Miezi Sita niliojipangia bali ni kutokana na malalamiko ya wananchi wengi kuhusu kukatika kwa umeme mara kwa mara katika siku, wiki na miezi ya hivi karibuni.

TANESCO wametoa sababu nyingi za kadhia hii. Lakini nimebaini mambo manne:-

1. TANESCO haina mfumo wa kiteknolojia wa kubaini kwa haraka ukatikaji wa umeme kwenye maeneo mengi ya mitaani (yaliyo katika mfumo wa usambazaji).

2. Wananchi wengi wanakosa namna ya uhakika ya kuripoti kukatika kwa umeme au changamoto nyinginezo ikiwemo kuunganishiwa umeme, na hata pale wanapoweza, hawapati majibu fasaha au majawabu huchelewa kupatikana.

3. Taarifa za awali (advance notice) za kuzimwa kwa umeme katika maeneo kadhaa kutokana na matengenezo yaliyopangwa (planned mantainance), hazipelekwi kwa ufanisi kwa wananchi walio wengi. Hivyo, kupelekea kukosekana kwa maandalizi na hivyo kuongeza malalamiko.

4. Kwa muda mrefu, matengenezo ya kawaida (repair and maintenance) ya miundombinu ya usafirishaji na usambazaji umeme yamekuwa hayafanyiki kwa kiwango stahiki na hivyo kupelekea miundombinu kuwa chakavu na kusababisha kadhia ya sasa ya kukatika kwa umeme mara kwa mara. Mwaka jana, kwenye repair and mantainace ya miundombinu ya usafirishaji na usambazaji, TANESCO ilipanga kutumia shilingi bilioni 80.5 (ambayo bado ni chini ya kiwango cha kimataifa ki-asilimia ya mapato ya Shirika). Hata hivyo, kiwango kilichotumika ni shilingi bilioni 67 tu.

Ili kukabiliana na kadhia ya kukatika kwa umeme mara kwa mara, nimeelekeza TANESCO kama ifuatavyo:-

1. Kuhakikisha kwamba tatizo hili, hasa pale kunapotokana na uzembe na ucheleweshaji wa matengenezo, linaisha ndani ya wiki mbili. Zaidi ya hapo, tutalazimika kuwaondoa kazini wahusika.

2. Kuimarisha mfumo wa huduma kwa wateja, ikiwemo kuweka mfumo wa kiteknolojia wa kupokea na kutoa taarifa, kwa wakati na kwa ufasaha, kwa wananchi.

3. Viongozi wa Shirika kutokimbia wajibu wa kuwasiliana na umma kuhusu changamoto za huduma ya umeme na kutegemea wanasiasa wawasemee. Kwahiyo, kuanzia Jumatatu, tarehe 20/09/2021, kwa wiki nzima, wawakilishi wa Shirika wajitokeze kwenye vipindi vya moja kwa moja vya vyombo vya habari mbalimbali vya habari na kupokea kero za wateja wao kuhusu huduma ya umeme na kuzitolea majawabu.

4. Kuhakikisha kwamba matengenezo na maboresho yanayopaswa kufanywa kwenye mfumo wa usafirishaji na usambazaji, ili kuondoa vifaa chakavu, yanafanyika bila kucheleweshwa. Na Wizara ipatiwe repair na maintenance plan.

Pamoja na kwamba sikuwa nimepanga kufanya ziara hii kwa wakati huu, nilichukua fursa hii kuwajulisha wafanyakazi wa TANESCO niliozungumza nao kwamba mabadiliko makubwa yanakuja ndani ya Shirika. Mabadiliko hayo yanaweza kuja na machungu, lakini ni uchungu wa uzazi – unaoishia kwenye furaha. Niliwajulisha kwamba tunawaamini na kuthamini na kutegemea utalaam wao katika uendeshaji wa Shirika hili nyeti.

Tunataka kuipeleka TANESCO kwenye ngazi ya kuwa moja ya mashirika yenye thamani kubwa na yanayoheshimika zaidi Afrika Mashariki na Kati. TANESCO ina mapato ya mwaka ya takribani shilingi trilioni 1.8 – zaidi ya shirika au kampuni yoyote ile nchini, ama ya umma au binafsi. Lakini pia matumizi yake ni trilioni 1.8 – na ina deni linalokaribia shilingi trilioni moja. Ni shirika lenye mali nyingi – za thamani ya shilingi trilioni 13 - kuliko karibu kampuni yoyote nchini. Kwa assets hizi, na mapato haya, TANESCO haipaswi kusuasua kama ilivyo sasa. Asilimia 88 ya mapato ya TANESCO (shilingi trilioni 1.6) inatokana na mauzo ya umeme, kwa wateja milioni 3.2 tu. Inawezekana kabisa kutengeneza wateja wapya mara tatu ya hawa. Asilimia 23 ya gharama za TANESCO (shilingi bilioni 412) ni gharama za uchakavu wa mitambo na miundombinu (depreciation).

Kutokana na uchakavu wa mitambo na miundombinu, TANESCO mwaka jana ilipoteza asilimia 16 ya umeme iliosafirisha. Kiwango cha umeme kinachoruhusiwa kupotea kimataifa ni asilimia 5. Kwahiyo, mwaka jana, tulipoteza zaidi ya asilimia 10 ya umeme tuliosafirisha – sawa na takribani Megawati 120, umeme unaotosha kuhudumia mikoa zaidi ya nane (Iringa, Njombe, Ruvuma, Tabora, Manyara, Singida, Lindi, na Mtwara).

Kwa kifupi, kuna masuala mengi ya kuyapitia,ikiwemo namna ambavyo manunuzi yanafanyika. Jambo la msingi ni kwamba tutaliboresha Shirika kwa namna ambayo itawaweka juu na kuwapa thamani kubwa wateja na wafanyakazi wa Shirika. Wafanyakazi ni rasilimali muhimu katika utendaji wa Shirika. Tunataka wawe na ari mpya na kwamba hatutafokeana kama watoto wadogo na kwamba utalaamu wao utaheshimiwa bali uzembe hautavumiliwa. Tutapata siku maalumu ya kuzungumza na wafanyakazi na viongozi wote wa TANESCO na kuelezea kwa kirefu zaidi haya niliyoyagusia hapa, pamoja kuwapa muongozo, dira na mwelekeo mpya.

January Makamba (MB)

Waziri wa Nishati

View attachment 1945273

View attachment 1945271

View attachment 1945272
Vacuum would suck everything in motion!
 
Sixmoth

Member
Sep 11, 2021
11
45
A
Wanataka kuibinafsisha TANESCO haki ya Mungu familiya za JK na Makamba zitakuwa na mwisho mbaya sana, Tamaa na ubinafsi itawaangamiza
Acha kulani watu wewe toambinu tofauti nahiyo huduma iboreke ndio dhamira kinyume nahapo nunua wewe hizo hisa ilituwe salama nafamilia ulizo zitaja zifevizuri
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom