Zitto Kabwe apendekeza TANESCO wauze hisa(20%) fedha itakayopatikana ilipe madeni, Waziri Makamba atoa maagizo

Mulokozijr12

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
2,367
2,000
Ni
Haiwezekani...labda kama wangeuza 51 wajiondoe kwenye uongozi ..tatizo la mashirika ya imma mengi ni matumizi makubwa kuliko kinachoingizwa..na mbaya zaidi sera wanatungiwa na wanasiasa..ila hili shirika libaki kuwa la serikali ..huwezi kubinafsisha tanesco kwenye nchi masikini kama tanzania
Kweli lakini ili watu waweze kununua shares si lazima wawe well informed au ndio wanaenda kutupa capitals zao, kwa namna yoyote hata kama ni ndogo itabadilisha operational style whether postive or in negative way.
 

Wyatt Mathewson

JF-Expert Member
Dec 22, 2017
12,032
2,000
Relax Brother, hebu soma nilipoanzia 20% haiwezi kuwa na impact yoyote katika maamuzi maana hata board hawataweza kuiunda, angalia juu kabisa hizi ni assumptions zangu ambazo ni kama guessing tuu.
Watu hawapo hata kwenye board,decisions wanazifanyia wapi kuleta change?

Hakuna

Atabakia Makamba na Samia,wanasiasa kupanga hatima ya hela zao za uwekezaji wao...nani ana muda wa kuwekeza kwenye kampuni inayoongozwa na wanansiasa wasiojua lolote?

No one trust government na wanasiasa wake viazi hasara bin hasara!
 

Kilatha

JF-Expert Member
Nov 28, 2018
4,031
2,000
Kwani DSE ni kama soko la Kariakoo?
Nijuavyo, kuna vigezo rundo mpaka kampuni isajiliwe, ikiwemo KUTENGENEZA FAIDA KWA MIAKA 3 MFULULIZO.
Urafiki Textiles walitaka kutumia hii janjajanja ya Zitto kupiga hela, DSE wakawagomea.
Je kuna shirika la umma lililosajiliwa DSE?
Well sina uhakika na sheria za Tanzania on the regulation of issuing IPO (kwa nchi zingine faida sio swala la msingi).

Lakini kumbuka ‘Swala Oil’ (kampuni ya oil and gas exploration ya Mengi) ilikuwa aina ata operations na ikasajiliwa so I don’t know exactly ni nini kilichozuia urafiki.

But the issue hapa how does one justify 20% ya TANESCO shares is enough to pay for their long term debts and leave enough to do other investments (from what evaluation) zaidi ya kujiropokea tu.

Besides TANESCO tatizo lake sio madeni pekee, CoS ni kubwa kushinda revenue; sasa badala ya kuangilia nini shida hapo wanakimbilia solution za baadae tena bila ya hata kujua thamani ya hisa.

Anyway wacha niachie hii mada hapa, just wanted to highlight the thought nonsense in all of this.
 

Tangawizi

JF-Expert Member
Jun 25, 2009
4,182
2,000
Nani anunue hisa za shirika mfu kama TANESCO
Shida ya wana siasa wetu wengi wanataka kutengeneza fursa za kuchukua bure mali za umma. Kubinafshisha Tanesco kwa weledi itasaidia. Nakumbuka TRC nayo ilibinafishwa. Ikaishia kutegemea tena aliyeibinafisha.
National interest ziwe sehemu ya agena zetu na sio kutaka utajiri ambaop ipo siku watanzania watataka kujua mahesabu yake
 

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
4,494
2,000
Wawekezaji wengi Tanzania kwenye umeme wanataka wawe kwenye hpande wa uzalishaji halafu waiuzie Tanesco, kwa nini wasizalishe na kusambaza wenyewe? Jibu ni moja, watanzania hawana tabia ya kulipa madeni hivyo hakuna ambae yuko tayari kubeba hasara.

Ndio maana wao wanawekeza kwenye kuzalisha halafu wanailazimisha tanesco inunue kwao iuze, watu walipe bill wasilipe haiwahusu wao wanamkaba koo tanesco.

Tukiacha siasa, a wao wanawekeza kwenye kuzalisha halafu wanailazimisha tanesco inunue kwao iuze, watu walipe bill wasilipe haiwahusu wao wanamkaba koo tanesco.
Wawekezaji wapo tayari kuzalisha na kusambaza umeme, kikwazo ni sheria iliyotungwa na wanasiasa, kwa sababu wanazojua wao.
 

Roadmap

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
2,486
2,000
Aisee zito Hajui hata biashara zimaendaje huyu jamaa amewahi kuuza hata karanga kweli? Tanesco ikitoa hata robo ya hisa tu mzigo utamrudia mwananchi mana hakuna atakekubali shirika lijiendeshe kwa mauzo ya Luku tu, Yani muondoe connection fee, Monthly Service charge still pawe na faida???, Tanesco iendelee kuwa State owened Entity ni nzuri kiusalama pia, Nishati ni esential tool kwa Nchi tuzicheze na Nishati kabisa.

Afu kwa records za Tanesco nani aweke Mpunga wake Kununua share? Huku shirika halijawahi kutoa Dividend kwa Serikali ambaye ndio main financier

Tanesco iachwe iendelee kumilikiwa na Serikali ili wananchi wapate huduma kuna watu walidai Zitokee kampuni zingine mbadala zicompate na Tanesco kuondoa Monopoly nkawauliza nani anaweza kukufanyia haya kwa bei ya 27000

-Surveying Bure ambayo ina Labour charge na Transport
-Material Bure ambapo accessories kama wire tu ni zaidi 27k
- Connection ambayo ina involve labour charges na transport
Bado mteja huyo huyo awekwe D1 na kuuziwa umeme kwa 122 per unit seriously?
Mteja ashindwe Kuingiza umeme tanesco iwashe gari Km 60 kumfata Bure kabisa
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
123,023
2,000
Unanunua hisa kwenye shirika ambalo kila mwaka ni hasara ya Mabilioni lini shareholders watapata dividends? Ayatollah Zitto KAKURUPUKA!!!


Yaani tununue hisa ili zikalipe madeni?
Kwani sisi wanahisa tulikuwepo wakati shirika likikopa kwa hasara?
Nani atanunua hisa za shirika linaloendeshwa kwa hasara na siasa za CCM?
 

Matrix19

JF-Expert Member
Feb 24, 2020
2,466
2,000
Hawa wangekubali ushandi tangu ile 2006 nchi ingepata heshima..

Haiwezekani nchi ina umri wa kikongwe kabisa inajadili kukatika umeme saa 10 nzima bila sababu ya msingi wala uwajibikaji kwa watu huku hizi hoja ndogo ndogo hazina nafasi tena
 

Roadmap

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
2,486
2,000
Wawekezaji wapo tayari kuzalisha na kusambaza umeme, kikwazo ni sheria iliyotungwa na wanasiasa, kwa sababu wanazojua wao.
Hawa wawekezaji Wakiruhusiwa na Tanesco ikafa kivyovyote basi Jua umeme utakuwa Anasa na sio Huduma kwa jamii, Wataumia wananchi wa chini hakuna investors atataka kuwaungia watu umeme kwa 27k afu awauzie unit 122 hayupo
 

August

JF-Expert Member
Jun 18, 2007
7,319
2,000
Kiongozi wa Chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe amemshauri waziri wa nishati January Makamba apeleke DSE 20% ya hisa za Tanesco zikauzwe na fedha itakayopatikana itumike kulipa madeni ya Shirika.
Kama mwekezaji au Mlipa deni atafanikiwa kurudisha na kupata faida juu ya uwekezaji wake, kwanini Tanesco au serikali usifanye hivyo na kuondoa inefficiency? Au in efficiency inaondolea na uwekezaji na sio sisi wenyewe??
 

Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
16,339
2,000
Kiongozi wa Chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe amemshauri waziri wa nishati January Makamba apeleke DSE 20% ya hisa za Tanesco zikauzwe na fedha itakayopatikana itumike kulipa madeni ya Shirika.

Kipele kimepata mkunaji, anasisitiza Zitto Kabwe katika page yake ya twitter.

Waziri January Makamba amekubali kupokea ushauri huo.

Kwenu wadau, 20% ya Tanesco ni bei gani?

====

Zitto Kabwe amesema: "Kipele kimepata mkunaji! Orodhesha 20% ya Hisa za Shirika kwa Soko la Hisa la Dar es Salaam. Mapato elekeza 1) Lipa Madeni yenye riba kubwa 2) punguza Umeme unaopotea 3) ongeza uzalishaji wa Umeme wa Gesi Asilia ( Kinyerezi 3 and 4 ). LAKINI sio kwa Bodi iliyopo! Sheria ya Umeme?"

Waziri Makamba atoa maagizo TANESCO


Waziri Janauari Makamba amesema;

Jana nimefanya ziara fupi kwenye Kituo cha Udhibiti wa Mfumo wa Usafirishaji Umeme (Grid Control Center - GCC), Ubungo, Dar es Salaam. Ziara hii haikuwa sehemu ya Mpango Kazi wa Miezi Sita niliojipangia bali ni kutokana na malalamiko ya wananchi wengi kuhusu kukatika kwa umeme mara kwa mara katika siku, wiki na miezi ya hivi karibuni.

TANESCO wametoa sababu nyingi za kadhia hii. Lakini nimebaini mambo manne:-

1. TANESCO haina mfumo wa kiteknolojia wa kubaini kwa haraka ukatikaji wa umeme kwenye maeneo mengi ya mitaani (yaliyo katika mfumo wa usambazaji).

2. Wananchi wengi wanakosa namna ya uhakika ya kuripoti kukatika kwa umeme au changamoto nyinginezo ikiwemo kuunganishiwa umeme, na hata pale wanapoweza, hawapati majibu fasaha au majawabu huchelewa kupatikana.

3. Taarifa za awali (advance notice) za kuzimwa kwa umeme katika maeneo kadhaa kutokana na matengenezo yaliyopangwa (planned mantainance), hazipelekwi kwa ufanisi kwa wananchi walio wengi. Hivyo, kupelekea kukosekana kwa maandalizi na hivyo kuongeza malalamiko.
Watanzania hawajasahau Tanesco ilivyouzwa kwa South Africans na Serikali ya awamu ya 4 na kupata hasara kubwa. Wakati sasa Pesa za walipa kodi zimefanya kazi kubwa na JNHPP ipo karibu kwisha wameanza tena mbinu ile ile ili kuwakamua Watanzania.

Watanzania sio wajinga tena, hawa wote (Zito na January) wanaangalia matumbo yao - swala hili halitakubalika vyovyote vile. Kweli kuna watu wana tamaa kama fisi.
 

twende wote

Member
Mar 29, 2021
18
75
Waziri JANUARY MAKAMBA
Ndugu muheshimiwa waziri, nakupa pongezi kurudi ktk safu ya uongozi,

Pili, napenda kutoa maoni na ushauri wangu, imefika wakati shirika la umeme lijiendeshe kibishara na litengeneze faida, mfano soko la umeme liko wazi wateja wanahitaji huduma, lakini kupata huduma ya kuwekewa umeme utafatilia utadhani una kesi ya mauaji,kila siku jalada bado,
USHAURI.
Ktk kuchelewa kufungiwa umeme, Tanesco abaki mzalishaji wa umeme na mkusanya Kodi,msambazaji wapewe makampuni binafsi, hapo itasaidia ushindani, na huduma kufika kwa haraka, mfano unajenga nyumba Kuna wasambazaji 3 kila mmoja atakufata Mimi ntakufungia kwa mkopo, mwingine atasema Mimi ntakufungia nakupa na unit 100 bure, wew mteja utachagua uende kampuni gani,

Ndani ya muda mfupi umeme utaenea kote na suala la kucheleweshewa litakuwa historia,

Kwa Sasa mmeshusha Bei ya kuingiza umeme, lakini sio kwamba umepungua Bali itakuwa mmetengeneza mianya ya kuwaneemesha wafanyakazi wa Tanesco wasio waaminifu l guess.

BWAWA, la nyerere simamia liishe kwa wakati, watanzania wanakumbuka ulikuwa kinyume na mpango huo wakati ule, chonde chonde hutaeleweka, simama kidete utuachie alama sio lawama,,,
Peni imeisha wino, naingia kulea wazee
 

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
43,837
2,000
Basically kabla ujaizungumzia kampuni na kutoa suggestion first you need to read their financial statements.

Conduct various financial analysis on statements, then give an opinion on what is wrong with the company.

Having said that 90% ya michango ya kwenye hii mada ni ujinga.

You can’t talk finances of a company bila ya kusoma their latest available financial statement.

Hiyo ndio namna pekee unaweza analyse kampuni vinginevyo ujinga.

If I were an accountant for TANESCO goodwill pekee ningetaka iwe not less than 5 trillion.

You know what you people need diaspora.

Asilimia 90 ya michango ya maswala ya kodi, business finance and government approach ni ujinga.

Ni watu wachache sana wenye uwezo wa kudadavua hayo mambo (wapo ila wachache tena wakiamua) hila regulars.

Ndio ukweli ata kama una uma; this post wont be deleted kasheshe niamke halafu unijaribu wakati huna uwezo wa maswala ya finance be it mie mwenyewe tia maji tia maji.

Ukweli ni kwamba naweza jigamba ata ukimleta Zitto sio kwamba mie najua vile ila nyie watu hamna uwezo na maswala ya finance; I can live with that.

Sasa lazima tujiulize elimu yetu inafundisha nini.

I am not all that, but don’t quote me unless unajiamini, trust me Zitto sio first class economist; hajui uchumi only kwa watu msiolewa hayo mambo.

Worst of sio finance tu hata energy policies amzijui na mimi pia I am limited hila sio kwa Zitto au January hawajui haya mambo huo ndio ukweli wenyewe.

Tanesco haikukaguliwa na CAG
 

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
1,628
2,000
We kima nadhani huelewi hata maana ya soko la hisa ni nini
Watu wanakurupushwa brother, yaani kuiongoza hii nchi tabu sana; umaskini na ujinga vimetufanya tuwe watu wa wasiwasi tu muda wote. Hoja ya mtu (isitoshe ni pendekezo tu) kabla haijaeleweka tayari watu wamesharukia kwenye malalamiko. Hoja za waziri mwenyewe hata hawazizungumzii
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom