Daimler
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 556
- 973
Aliyekuwa Katibu wa Ngome ya Wanawake wa ACT, Ester Kyamba
Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe mna o tarehe 28.10.2018, anadaiwa kumvua uongozi, Katibu wa Ngome ya Wanawake wa ACT-Wazalendo, Ester Kyamba kwa madai ya kuhoji uhalali wa Dorothy Semu kukaimu nafasi ya Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo kwa muda mrefu.
Inaelezwa kuwa, Dorothy Semu amekaimu nafasi ya a Katibu Mkuu wa ACT-Wazalendo tangu Mwezi Juni 2016, kinyume na Katiba ya Chama hicho inayoeleza kuwa, mtu yeyote anaweza kukaimu nafasi hiyo kwa muda usiozidi mwaka mmoja.
Hata hivyo, Dorothy amekaimu kitu cha ukatibu mkuu kwa muda wa miaka miwili na robo.