Zitto Kabwe amponza Manji kutimuliwa Quality Plaza

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
SAKATA la kati ya Mfanyabiashara Yusuf Manji na mifuko ya hifadhi ya jamii limeendelea na sasa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), umemtaka mfanyabiashara huyo kuhama mara moja katika jengo la Quality Plaza ambalo aliuuzia mfuko huo katika mazingira tata.

Manji anadaiwa na PSPF karibu Sh bilioni 5, ambazo ni malimbikizo ya kodi ya pango.

Kwa muda mrefu sasa Manji amekua akitajwa kufanya biashara zenye utata na mifuko ya hifadhi ya jamii na alifanikiwa kuiuzia PSPF jengo la Quality Plaza na Mufuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuizua maghala kwa shilingi bilioni 46, ambayo aliyajenga kwa mkopo wa Sh bilioni 9 kutoka mfuko huo.

Habari za uhakika kutoka serikalini zinaeleza kwamba, uamuzi huo wa PSPF umefikiwa Ijumaa ya Aprili 1, 2011 baada ya mfuko huo kubanwa na Wabunge wa Kamati Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.

Katika barua ya PSPF kwenda kwa kampuni ya Image Properties & Estate inayosimamia uendeshaji wa Quality Plaza, mfuko huo umeitaka kampuni ya Quality Group Limited kuondoka mara moja katika jengo hilo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

Hivi karibuni, Quality Group Limited iliiomba Mahakama kuzuia kuondolewa kwao katika jengo hilo, maombi ambayo muda wake ulishakwisha lakini PSPF wakawa wanachelewa kuchukua hatua wakati taasisi hiyo ilikua na hali mbaya ya kifedha kiasi cha serikali kuombwa na POAC kulinusuru kwa kuwekeza zaidi.

"Unaelekezwa kuitimua haraka Quality Group Limited kwa kushindwa kutimiza masharti ya mkataba wa pango," inaeleza sehemu ya barua hiyo ya Aprili 1, 2011 iliyosainiwa na Kaimu Mkurugenzi Adamu Mayingu, kwenda kwa Image Properties & Estate.

Jengo hilo liko kitalu namba 182/2 barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam ni mali ya PSPF alipanga baada ya kuliuza lakini akawa halipi kodi.

Katika maelezo ya wakili wa PSPF, Benitho Mandele, ambayo iliwasilishwa mahakamani iilieleza kwamba Manji anadaiwa kodi ya kuanzia Aprili, 2009 hadi Desemba 2010, hivyo jumla ya deni lote ni dola 2,335,189.06 za Marekani, wakati shauri hilo lilipowasilishwa mahakamani na sasa limefikia Sh bilioni 5.

Makampuni mengine ya Manji yaliyomo katika jengo hilo ni pamoja na kampuni aliyoichukua kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mazingira tata ya Gaming Management Limited, Quality Ligistics Co. Limited, International Transit Ivestment Limited na Q-Consult Limited.

Source: Zitto Kabwe amponza Manji kutimuliwa Quality Plaza | Fikra Pevu
 
Manji, RA, Chenge, Mkapa et al ni watu wa kuwekwa ndani na kufilisiwa mali zao kwa sheria ya uhujumu wa uchumi Period!
 
Ni muhimu kuangalia kuwa Bunge halifanyi kazi za watendaji. Ni vizuri kutumia madaraka yake ya kusimamia na kushauri serikali lakini jukumu la kwanza la Wabunge ni kutunga sheria.

Kama kuna matatizo katika sheria hizi ni wao ndio wenye kuzibadilisha. Binafsi nitapata hamasa zaidi nikiona wabunge wanakujana kupigania mabadiliko ya sheria ambazo wanajua zinaleta matatizo. Ndio maana hadi leo hii sielewi kwanini sheria 40 bado zipo vitabuni.

Wabunge wasije kuacha kutimiza wajibu wao.
 
Ni muhimu kuangalia kuwa Bunge halifanyi kazi za watendaji. Ni vizuri kutumia madaraka yake ya kusimamia na kushauri serikali lakini jukumu la kwanza la Wabunge ni kutunga sheria. Kama kuna matatizo katika sheria hizi ni wao ndio wenye kuzibadilisha. Binafsi nitapata hamasa zaidi nikiona wabunge wanakujana kupigania mabadiliko ya sheria ambazo wanajua zinaleta matatizo. Ndio maana hadi leo hii sielewi kwanini sheria 40 bado zipo vitabuni.

Wabunge wasije kuacha kutimiza wajibu wao.

Kuishauri serikali siyo kazi pekee ya Bunge bali na kuisimamia Serikali pia ni kazi mojawapo ya Bunge. kama unadhani POAC imevuka mipaka yake ya utendaji hebu tudokeze wamevuka vipi!.
 
Kuishauri serikali siyo kazi pekee ya Bunge bali na kuisimamia Serikali pia ni kazi mojawapo ya Bunge. kama unadhani POAC imevuka mipaka yake ya utendaji hebu tudokeze wamevuka vipi!.

Nimesema kuishauri serikali ndio kazi "Pekee ya Bunge"? Nimesema ni muhimu "kuangalia" kwamba tusije kujikuta tunatumia shortcut ya Bunge kufanya kazi za watendaji. Sijasema POAC "imevuka mipaka". Nijaribu kujifafanua zaidi?
 
Kuishauri serikali siyo kazi pekee ya Bunge bali na kuisimamia Serikali pia ni kazi mojawapo ya Bunge. kama unadhani POAC imevuka mipaka yake ya utendaji hebu tudokeze wamevuka vipi!.

Kuisimamia serikali ni kuibana ili kujibu hoja au kutoa maelezo, ikiwa ni pamoja na kutunga na kurekebisha sheria. Hii haina maana kuingilia kazi za kiutendaji.

Mfano, kamati ya Mwakyembe iliibana serikali bungeni kwa kuainisha uovu, waliohusika waliwajibishwa, na wale ambao huwakuweza kuwajishwa na bunge Rais alipewa jukumu, ah ! wakasamehewa na kustaafu wapumzike.

Kama bunge liliona upungufu huo lilikuwa na wajibu wa kutunga au kubadilisha sheria ili kutompa rais nafasi ya kufanya anavyotaka bila kuzingatia kanuni za utawala bora.

Hizi kamati siku hizi zinakwenda hadi kutoa maelekezo ya utendaji. Mfano, January anasema kamati ya nishati ifanye hivi na isipofanya....

Haya ni maelekezo ya kiutendaji, alichotakiwa ni kupeleka kesi yake bungeni na mtendaji husika atapambana na wabunge.
Kuanza kuziachia kamati hizi utendaji ndiyo imekuwa chanzo cha watendaji kukwepa majukumu. Angalia suala la umeme, Mkurugenzi Tanesco ni kama hayupo, waziri kaingia mitini, Waziri mkuu yupo bize kuhudhuria hafla za utawazo, rais halisemi.

Yote haya ni mwanya unaotokana na kamati kuwa za utendaji, na waoga wanazitumia kama mwanya na vichaka kuficha rafiki zao.
 
Nitatoa mfano mzuri kwenye hili suala la Endowment Scheme; haya ni mashirika ya umma lakini yameachwa na Bunge yajitungie sheria na taratibu zake kiasi kwamba zimewekwa utata wa wazi. Well... ukitaka kusahihisha unafanya mabadiliko katika sheria (kwa kupitia Bunge) au kwa Rais kutoa Executive Order (Agizo la Rais).

Leo hii Kamati inasimamia sheria kwa kutaka Bodi imuondoe mtu kwenye bodi aliyeteuliwa na Executive. Well.. tunaweza kubishana juu ya hilo lakini binafsi naamini wao kama wabunge walitakiwa walete hiyo hoja Bungeni na kumtaka Waziri Mkuu aeleze kwanini hadi hivi sasa kuna baadhi ya bodi ambazo zina wabunge ndani yake wakati tayari kulikuwa na sheria ambayo ilitaka isiwe hivyo? Then Waziri Mkuu atatoa maelezo na pale pale Bunge linaweza sasa (kwa kuisimamia serikali) kuipa serikali timeline ya kutimiza hilo.

Ninaamini kwenye hilo la uteuzi Kamati ya Bunge ilitakiwa kumuiwa Waziri anayesimamia PPF kutoa maelezo kwanini alimteua mbunge (kama ni yeye mwenyewe au aliyemtangulia sijui) kuwa mjumbe wa Bodi? Tunachosema ni kuwa Kamati ya Bodi kuwakalisha kiti moto watendaji wa mashirika ya umma bila kuwakalia kooni inavyostahili mawaziri, na waziri mkuu ni overkill.

Pamoja na hiyo ni mwanzo mzuri wa kuwajibishana lakini tukiamua kuwajibisha twende mbele zaidi na kuwawajibisha wote. So far its a good start.
 
Ni 'overkill' na pia ni kukosa kitu kinaitwa 'check and balance'. Haiwezekani kwenda kutoa maelezo ya kiutendaji halafu kamati irudi bungeni kumbana waziri! Moja kati ya madhara yake ni kuenea kwa rushwa na pengine ndio maana tunaona vikumbo kugombea ujumbe wa kamati.

Kuhusu wabunge kuwa katika bodi za mifuko, inatatiza sana. Mfano, mbunge atawezaje kuidhinisha malipo ya milioni 200 kwa mtu halafu arudi bungeni kuhoji uhalali wa malipo ?(conflict of interest). Ikumbukwe hawa wanaovuna ni watu wanaojua vema taratibu na kabla ya kwenda benki watahahakikisha kuwa eneo lao la uchezaji lipo salama!
 
Nini kilishababisha tatizo hili.

Je,kamati ya zitto bunge liloisha alikuona hilo na zitto alikuwa mnykt wa kamati hiyo.

Kuna nini hapa.?
 
Hii list ya watu 10 itatusumbua sana watanzania tusipochukua hatua!

Jengo ameuza kulipa kodi hataki halafu kisha jenga jengo jingine jirani si ahamie huko kwake? Pale Zain alimwingiza mkenge katibu UWT aliyegombea ubunge Ubungo 2010 akapewa jengo hakutoa hata senti mfukoni, NBC wakajenga, yeye anakula cha juu tuu sasa. TANROADS nao wamehamia pale wameacha jengo la serikali Maktaba Complex wameenda kumpa pesa Manji
 
Nini kilishababisha tatizo hili.
Je,kamati ya zitto bunge liloisha alikuona hilo na zitto alikuwa mnykt wa kamati hiyo.
I think zitto was busy with CDM, which to me is just a capitalist party trying to get votes from a socialist society.

Now that he is working under a socialist government (because I believe he is socialist), he is getting attacked by CDM members who think their party is socialist together with CCM members/fans who hate that their party is socialist....

Think about it!
 
Ni muhimu kuangalia kuwa Bunge halifanyi kazi za watendaji. Ni vizuri kutumia madaraka yake ya kusimamia na kushauri serikali lakini jukumu la kwanza la Wabunge ni kutunga sheria.

Kama kuna matatizo katika sheria hizi ni wao ndio wenye kuzibadilisha. Binafsi nitapata hamasa zaidi nikiona wabunge wanakujana kupigania mabadiliko ya sheria ambazo wanajua zinaleta matatizo. Ndio maana hadi leo hii sielewi kwanini sheria 40 bado zipo vitabuni.

Wabunge wasije kuacha kutimiza wajibu wao.

Sasa hapo naona unataka kusema Zitto kaingilia kazi za kiutendaji.Wewe na Saed Kubenea lenu moja.
 
Hii list ya watu 10 itatusumbua sana watanzania tusipochukua hatua!

Jengo ameuza kulipa kodi hataki halafu kisha jenga jengo jingine jirani si ahamie huko kwake? Pale Zain alimwingiza mkenge katibu UWT aliyegombea ubunge Ubungo 2010 akapewa jengo hakutoa hata senti mfukoni, NBC wakajenga, yeye anakula cha juu tuu sasa. TANROADS nao wamehamia pale wameacha jengo la serikali Maktaba Complex wameenda kumpa pesa Manji

Mimi kilichonishangaza ni kwamba halipi kodi kwa miaka kadhaa halafu anakwenda mahakamani kuzuia asifukuzwe na mahakama inatoa amri kama hiyo! Jamani labda kama kuna siri fulani humo ndani hatuambiwi ukweli lakini haiingii akilini hata kidogo. Inaonyesha dhahiri kwamba kidogo kimetembea ndiyo maana ukatoka uamuzi kama huo.

Leo shirika linakufa hivi hivi, Manji anaendelea kutanua tu na sisi tunamwachia, halafu tunakuja kulalamika kwamba shirika limekufa, jee sisi Watanzania pamoja na srikali yetu tumerogwa na huyu Manji?

Aaaaaaaaaaaaaaaaaagh! natamani kutapika nikisikia jina la Manji.
 
hivi inakuwaje watu ambao wanakuwa na uzalendo na nchi yao waonekane maadui kiasi hiki? Coz kuna watu humu jf na nje pia ambao wanawashambulia sana mwanakijiji,kubenea na wengineo sababu ya kutoa elimu ya uraia kwa watz.kazi itaendelea tu hata mkipiga vita kiasi gani
WHapa
 
Nuclear unatetea nn hapa? Dont waste our valuable tym to read negative posts
 
Back
Top Bottom