Zitto Kabwe ampongeza Rais Magufuli kupunguza PAYE

Njaro

JF-Expert Member
Mar 19, 2016
356
787
Anaandika Zitto Kabwe..

Hatua kubwa sana kupunguza kima cha chini cha kodi ya mapato ( PAYE) . Tumshukuru Rais kwa hatua hii. Hata hivyo tusisahau, hii inatokana na juhudi kubwa zilizofanywa vyama vya upinzani nchini. Kwa mara ya kwanza suala hili liliibuliwa Bungeni Mwezi Juni, 2011 na Kambi ya Upinzani Bungeni katika Bajeti Kivuli

https://zittokabwe.wordpress.com/…/bajeti-mbadalakivuli-ya…/

Imechukua miaka 5 kufikia azma hii ya kuwasaidia wafanyakazi wa ngazi za chini za mishahara. Vyama vya upinzani visichoke kuwaonyesha watawala mambo mema kwa wananchi hata kama wanayatekeleza bila hata kutambua chanzo chake. Mapambano yaendelee.
 
Mbona sikuona mwakilishi wa vyama vya upinzani pale uwanjani??
 
Zito tunza akiba ya maneno mshikaji,hiyo PAYE imepungua kiasi gani na kwa wanaopokea bei gani.ndo mana mimi najitoa kukandia kila kitu coz maraia hawa wanatupiga sanaa tu
Fuatilia 2005 hii paye ilikua ni kiasi gani ndio umwambie zzk kwamba aweke akiba ya maneno.
 
Hiyo 9 .% ni wale wa mshahara kiasi kipi au ni kwa wote kuna jambo haliko wazi mwenye kufahamu anielezee
 
Hiyo 9 .% ni wale wa mshahara kiasi kipi au ni kwa wote kuna jambo haliko wazi mwenye kufahamu anielezee
d3689d0613b6da931e09aa9e5e99d1a0.jpg
pitia hii
 
Back
Top Bottom